ALAMA 6 ZA KUKUTHIBITISHA MTU KUWA NI MTOTO WA MUNGU.



 

BWANA YESU asifiwe sana.
Karibu tujifunze alama ya kuwa mtoto wa MUNGU. Si kila mtu ni mtoto wa MUNGU na ili wewe uwe mtoto wa MUNGU lazima uwe na hizi alama 6 nitakazozitaja hapo chini.
Karibu.
1 Yohana 3:10a ‘’Katika hili watoto wa MUNGU ni dhahiri, na watoto wa ibilisi nao. ‘’
Kumbe kuna watoto wa MUNGU aliye hai na kuna watoto wa shetani. Ndugu swali kwako ni hili, Je wewe ni mtoto wa MUNGU au ni mtoto wa shetani?
Kama ni mtoto wa MUNGU ubarikiwe sana na kama ni mtoto wa shetani jitoe huko na uzaliwe upya roho yako na MUNGU.
Unakuaje mtoto wa MUNGU?
Wagalatia 3:26 inajibu, inasema ‘’Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa MUNGU kwa njia ya Imani katika KRISTO YESU ‘’
Unakuwa mtoto wa MUNGU kwa njia hiyo lakini swali kwako ni hili, je wewe ni mtoto wa kweli wa MUNGU?
Je una hizi alama 6 za kukufanya uwe mtoto wa kweli wa MUNGU?
ALAMA 6 ZA KUMTHIBITISHA MTU KUWA NI MTOTO WA KWELI WA MUNGU.

1.   ANAMWAMINI YESU KRISTO.
Matendo 16:30-31 ‘’ kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini BWANA YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. ‘’
Kumwamini YESU KRISTO ni alama ya kwanza  ya kuwa wewe ni mtoto wa MUNGU aliyeahidiwa uzima wa milele.
1 Yohana 5:1 ‘’ Kila mtu aaminiye kwamba YESU ni KRISTO amezaliwa na MUNGU. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. ‘’
Kumwamini YESU KRISTO ni uzima na ni ufunuo muhimu sana ukiupata.
Yohana 3:15 ‘’ ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye(YESU). ‘’
Uzima wa milele uko katika KRISTO pekee.

2.  HUZALIWA NA ROHO NA ROHO MTAKATIFU.
Yohana 1:12-13 ‘’Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. ‘’
Hii ni alama muhimu sana kwa kila mtoto wa MUNGU. Kuzaliwa kwa ROHO MTAKATIFU ndio sababu kuu inayoweza kukufanya uushinde ulimwengu na mambo yake yote.
Warumi 8:16 ‘’Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa MUNGU; ‘’
ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana, akiingia ndani yako unakuwa mtoto wa MUNGU na unaanza kuenenda vizuri kama ukimtii.
2 Kor 5:17 ‘’ Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ‘’
Ni raha sana kuwa ndani ya KRISTO na kufanyika mtoto wa MUNGU. MUNGU anakusamehe dhambi zako na ya kale yote yanafutwa, unasamehewa hata kama ulifanya dhambi kubwa kiasi gani.

3.  HUUSHINDA ULIMWENGU.
1 Yohana 5:4-5 ‘’ Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na MUNGU huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.  Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba YESU ni Mwana wa MUNGU? ‘’
Ukiwa na KRISTO ndani yako, Ukawa na ROHO MTAKATIFU ndani yako na ukakubali kuongozwa na maonyo ya MUNGU BABA hakika utaushinda ulimwengu. Mtoto wa MUNGU huushinda ulimwengu maana kwa njia ya kumtii ROHO MTAKATIFU lazima ashinde. Ndugu Kataa dhambi, ogopa dhambi, Usitende dhambi na ikimbie dhambi hakika utakuwa una alama nzuri ya kukuthibitisha kwamba wewe ni mtoto wa MUNGU uliyezaliwa upya.
4.   HUMTII YESU KRISTO.
Yohana 14:23 ‘’YESU akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na BABA yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. ‘’
Ndugu mtii YESU KRISTO siku zote za maisha yako.
Waebrania 5:8-9 ‘’na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; ‘’
Ndugu mshike YESU KRISTO, mfuate YESU KRISTO, Mtii YESU KRISTO na msikilize na kumtii YESU KRISTO kupitia neno lake ‘BIBLIA’’
2 Thesalonike 2:10 ‘’na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. ‘’
5.  HUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.
Watu wengi huzaliwa na ROHO MTAKATIFU lakini hushindwa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU. ROHO wa MUNGU alikuzaa ili akuongoze, ndugu kubali kuongozwa na ROHO MATAKTIFU siku zote za maisha yako.
Warumi 8:14 ‘’Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU. ‘’
Je wewe ni mtoto wa MUNGU? Watoto wa MUNGU huongozwa na ROHO wa MUNGU. Je wewe unaongozwa na ROHO wa MUNGU. Ndugu kama huongozi na ROHO MTAKATIFU hakikisha unazaliwa na ROHO na kuongozwa na yeye.
Mathayo 5:9 ‘’Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa MUNGU. ‘’
6.  HUJITENGA NA ANASA ZA KIDUNIA.
2 Kor 6:16-18 ‘’ Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai; kama MUNGU alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, ‘’

MUNGU anasema tutakuwa wanae wa kiume na wa kike.Ni upendo mkuu sana huu wa MUNGU kutupenda sisi.
Ndugu jitenge na dhambi, jitenge na mambo ya kidunia, jitenge na miziki ya kidunia, jitenge na machukizo yote.
Waefeso 5:1,11 ‘’ Hivyo mfuateni MUNGU, kama watoto wanaopendwa; Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; ‘’
Dhambi ni mbaya na haifai, tujitenge na dhambi na machukizo yote.

Tito 2:11-12 ‘’ Maana neema ya MUNGU iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; ‘’
Mtoto wa MUNGU hujitenda na mambo mabaya ya dunia.
 1 Yohana 2:15-16 ‘’Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. ‘’
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.


Comments