IFIKE MAHALI SASA TUJITAMBUE! TUACHE KUWA KAMA WATOTO WADOGO!



1Yoh 5:18-20

Maana kwa kutokujitambua kwa mtoto mdogo ndiko kunakompelekea yeye kuwa na amani na furaha hata kucheza akiwa uchi, lakini akiwa mkubwa kidogo na kujitambua hatodhubutu tena kucheza akiwa uchi!

NI KWA KUTOJITAMBUA TUU, NDIYO INALETA SHIDA KATIKA FAMILIA!

=> Wazazi wanajinyima, hata wakati mwingine wanakopa fedha au kuuza baadhi ya rasilimali zao ili kumlipia Mwanaye ada, LAKINI kwa kutokujitambua kwa yule mwanafunzi, anaenda shule kuponda raha na marafiki zake huku akibadili wanaume/wanawake kama nguo! Amesahau andiko hili
Mithali 4:13

=> BABA NAYE ktk familia, amesahau majukumu yk kama baba(KICHWA), badala yk amekuwa anamtegemea mwanamke awe kichwa ktk familia(Kwa kuitunza familia)! Amesahau andiko hili;-
Mwa 3:17-19

Wanaume wengine wameenda mbali zaidi, fedha wanao, uwezo wanao lkn wameacha kuzitunza familia zao, wanatunza nyumba ndogo (MAKAHABA)! SHAME APON OF U

=> MAMA NAYE; Amesahau jukumu lake la kulea family badala yk amegeuka kuwa kujiwe cha story kwa mashoga zake! Kwa kuzitoa siri za ndani kwake kibarazani!
Amesahau andiko hili;-
Mithali 14:1

=> WALOKOLE WA SASA NAO; MMMH
BAATHI YETU TUMEPOTEZA MWEZEKEO

Maana utakuta mtu ameokoka lkn anafanya vituko vya ajabu! Na kusahau maandiko haya;

Eti naye anakunywa kidogo asilewe ha ha haaa..., Efe 5:18
Kwenye matambiko naye yupo, eti hawezi kuacha asili ya mababu zake Isaya 57:3-8
Eti na wao wanawakumbuka marehemu na kuwaombea (IBADA ZA WAFU) Mhu 9:4-6
Kwenye masengenyo nako yupo Zab 1:1
Uzinzi usiseme! Efe 5:3
Ushirikina ndo mama mama mama uuwiii... ni shida (Hata kwenda kwa waganga wa kienyeji ni ushirikina pia usifikiri ni kupiga tuguli tuu.. la hasha)
Isaya 8:19-20

Ni maombi yangu kwa Bwana, kwamba atusaidie TUJITAMBUE sisi ni akina nani katikati ya watu ambao hawajamjua Yesu! Na kuishi maisha matakatifu sawa sawa na Kristo,kwa kuwa sisi ni watt wa Kristo lzm tumfananie baba Yetu Ili; TUWE NA HUO USHUHUDA!
Ameen!

MUNGU ATUSAIDIE, TUJITAMBUE JAMANI!
Mbarikiwe sana sana.

By Lucy Marandu.

Comments