JINSI YA KUUSHINDA ULIMWENGU HUU TULIONAO. NA SABABU YA YAKE


Bwana Yesu asifiwe!
Tunapo zungumzia ulimwengu tunazungumzia dunia inayokaliwa na watu, na ndani yake yumo adui aitwae shetani (mungu wa dunia hii ) 2 Korintho 4: 4"AMBAO MUNGU WA DUNIA HII AMEPOFUSHA FIKRA ZAO WASIOANI...)
KWA NINI TUNAAMBIWA KUUSHINDA ULIMWENGU?
Kwa sababu kuna adui(shetani) ambaye siku zote anaweka matatizo kwa wanaomfuata Yesu hapa duniani, shetani hawasumbui watu wake ambao hajaokoka bali waliookoka tu.
Ndiyo maana Yesu anawaambia wanafunzi wake,
Yohana 16:33 "Hayo nimewaambia mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu".

Maneno haya anayasema Yesu kwa wanafunzi wake baada ya kuwafunilia wazi jinsi alivyo, na wakapata NGUVU ya kumpenda zaidi na kumwamini, na ndipo akawauliza "JE! MNASADIKI SASA? maana yake hapo mwanzo walikuwa na mashaka na Yesu. Ndipo anawambia..."TAZAMA, SAA YAJA, NAAM, IMEKWISHA KUJA, AMBAPO MTATAWANYIKA KILA MMOJA KWAO KWAO, NA KUNIACHA MIMI PENGE YANGU...."
Maana yake ni nini?..Ni wakati ambao atakamatwa ili auwawe na wanafunzi wake watakimbia na kumuacha Yesu pekee yake.
Na kukamatwa kwa Yesu ili auwawe. (HII NI VITA KATI YAKE NA SHETANI) ndipo shetani anaihamishia vita hii kwa waliookoka.

Kwa nini Yesu anawambia wanafunzi wake.."...MPATE KUWA NA AMANI NDANI YANGU" Alisema maneno hayo akijua shetani atawatafuta baadaye, hivyo WAKAE NDANI YAKE, ili wawe KAMILI NA KUJIAMINI. "I have told you these things, So that in me you may have [perfect] peace and confidence.John 16:33 a. (Amplified Bible) "Nimewaambia mambo haya yote, kwa hiyo katika mimi mtakuwa [wakamilifu] na amani na kujiamini"
Maana yake tunaposema Yesu ameushinda ulimwengu maana yake AMEMSHINDA SHETANI.
Basi wale wanaokaa NDANI YA YESU wanakuwa "WAKAMILIFU" au "WANAKAMILISHWA" na Yesu kwa kupewa "KUJIAMINI" ili waushinde ulimwengu, ndiyo maana ya kusema kaeni ndani yangu. Je! ulimwengu una nini ili waushinde? maana huwezi kuushinda ulimwengu kama hakuna kitu wanashindana nacho ulimwenguni kinacho achiliwa na shetani mungu wa dunia hii ili wamuache Yesu.


TUNASHINDANA NA DHIKI

Mdo 14:22 " Wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia ufamle wa Mungu kwa njia ya dhiki"

DHIKI NI NINI? 

Kuna maana mbili ya dhiki japo zipo nyungi.Tuzungumzie mbili.
Na Emmanuel Kamalamo.
1 .DHIKI YA UGUMU WA MAISHA
."...and [telling them] that it is through Many hardship and tribulations we must enter the kingdom of God" Act 14:22.(Amplified Bible) Mdo 14:22. 7:11.
2.DHIKI INAYOTOKANA NA
MATESO KWA WANAO MWAMINI YESU. Mdo 11:19 " Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano...".

Kama hujaokoka Yesu anaokoa hata sasa na kusamehe.
MUNGU AKUBARIKI.
By Emmanuel Kamalamo.

 

Comments