MAOMBI YA KUVUNJA LAANA YA NDOA NA MAAGANO, PAMOJA NA MAOMBI MENGINE.



Omba Maombi Haya Wewe Kijana Ambaye Unataka Kuoa Au Kuolewa, Muongozo Tumia Ayubu 22:28, Mathayo 16:19, Wafilipi 2:10-11, Marko 11:22:26, Na Isaya 53:4-6.

BWANA MUNGU, Nakuabudu Na Kulibariki Jina Lako Takatifu, Usifiwe Milele Yote Katika Jina La YESU. BWANA Imeandikwa " Hata Imekuwa Mtu Akiwa Ndani Ya KRISTO Amekuwa Kiumbe Kipya; Ya Kale Yamepita Tazama Yamekuwa Mapya" 2 Kor 5:17. Kwa Hiyo, Nakataa Kila Laana Na Maagano Yote Niliyoingia Au Kuingizwa Pasipo Kujua, Katika Jina La YESU KRISTO. Kila Laana Katika Maisha Yangu Inayonizuilia Kuoa/kuolewa, Naivunja Na Kuibatilisha Kwa Damu Ya YESU KRISTO. Kila Kipingamizi Kinachozuia Ndoa Katika Familia Yangu Ninakiharibu Leo Na Kukiondoa Kwa Jina La YESU KRISTO. Ninaalika Kibali Cha Kimbingu Mbele Ya Watu Wote Nitakaokutana Nao Katika Jina La YESU. Kila Laana Iliyo Ndani Yangu Naiharibu Na Kuifukuza Kwa Jina La YESU KRISTO. Asante MUNGU Kwa Kuniweka Huru. Katika Jina La YESU. Amen.


 FUNGA MAPEPO YOTE YANAYOZUIA MAOMBI YAKO.

Katika Jina La BWANA Wangu YESU KRISTO Ninakemea, Ninafunga Na Kuyaangamiza Mapepo Yote Yanayozuia Maombi Angani, Katika Nchi Na Baharini. Pia Naharibu Kila Pepo Anayening'inia Kila Pepo Arukaye Na Wale Mapepo Walionyimwa Chakula, Katika Jina La YESU KRISTO. Ninawatupa Hadi Anga La Giza Katika Jina La YESU. Ninaharibu Vipingamizi Vyote Vya Maombi Yangu Na Kuwatupa Katika Giza La Milele, Ninawafungia Huko Hata Siku Ya Hukumu Ya BWANA. Pia Ninakemea Na Kufunga Na Kuharibu Mapepo Yote Yanayozuilia Ukombozi Wangu, Maendeleo Yangu, Mafanikio Yangu Na Miujiza Yangu, Kwa Jina La YESU KRISTO. Ninaharibu Kazi Zenu Zote Dhidi Ya Maisha Yangu, Ninawatupa Wote Katika Giza La Milele Na Kamwe Msiweze Kuinuka Hadi Siku Ya Hukumu Ya BWANA. Nawatumia Moto Wa ROHO MTAKATIFU Kuwateketeza Wote Katika Jina La YESU KRISTO.

Amen.



 Kwa Wadada:MAOMBI KWA AJILI YA KUTAFUTA MATAKWA YA MUNGU KWENYE NDOA YAKO IJAYO.

Mwongozo Wako Wa Maombi, ni Mithali 18:2, Isaya 55:6, Yeremia 33:3 Na Zaburi 25:14.

JEHOVAH MUNGU, Muumba Wa Mbingu Na Nchi, Ninasema Asante Kwa Uzima Ulionipa, Utukuze Milele BWANA. BABA, Ninaleta Ombi La Kuchumbiwa Na Kijana Huyu(mtaje) Kwa Ajili Ya Ndoa, Mbele Ya Kiti Chako Cha Rehema Nikiomba Usema Nami BWANA. Naamini Kuwa Utatimiza Mapenzi Yako Kuhusu Ndoa Yangu, Nakuomba BWANA Usiruhusu Nifanye Makosa Katika Ndoa Yangu kwa Jina La YESU. Nifunulie Jambo Hili Kwa Ndoto, Maono, Ufunuo Au Kwa Namna Yeyote Ile, Mimi Niko Tayari Kukutii. Kama Sio Mapenzi Yako Kwa Mimi Kuolewa Na Kijana Huyu, Nikoseshe Amani Nikimuona Mahali Popote, Kama Ni Mpango Wako, Ruhusu Amani Na Furaha Yako, Nakuomba Pia BWANA Unisaidie Kutofautisha Kati Ya Upendo Na Tamaa Ya Mwili. Asante MUNGU Kwa Kunijibu Maombi Yangu. Ni katika jina la YESU KRISTO Nimeomba AMEN AMEN.


 
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments