Na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima. Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
Zakaria 3:1
Yoshua
alikua ni mtumishi wa Mungu na alisimama ili kuifanya kazi ya Mungu lakini
shetani nae akasimama mkono wake wa kuume ili ashindane nae.
Kwanini
shetani amesimama mkono wa kuume na sio
wa kushoto?
Mkono wa
kuume maana yake ni mkono wenye nguvu, ndio maana tunasoma Yesu ameketi mkono
wa kuume wa Mungu baba, kwa maneno mengine Yesu ndie ameshikilia nguvu za Mungu
baba na kama unahitaji nguvu za Mungu baba unatakiwa kuwa kumpata Yesu.
Hapa
tunaanza kuona shetani anashindana na mtu wa Mungu, na katika mashindano kuna
kushinda au kushindwa kwasababu ni mashindano.
Ziko sababu
kwanini shetani alipata nafasi ya kushindana na kuhani wa Mungu Yoshua, shetani alipata nafasi
kwasababu Yoshua alikua na nguo chafu.
Shetani
huwa hawezi kuanza kumshambulia mtu bila kuwa na kitu kinachompa uhalali wa
kushambulia, kwa Yoshua kuhani mkuu alipata nafasi kupitia maisha yake, maisha
yake hayakua mazuri na ndio yanawakilishwa na nguo za uchafu. Hii ndio sababu
maandiko yanasema wala msimpe ibilisi nafasi (waefeso 4:27)
Kumbe
ibilisi huwa hatendi kazi mpaka apate nafasi, ukimnyima nafasi huwa anakosa
nguvu kabisa. wakati shetani anataka kushindana na shetani alikuwako pia
malaika wa Bwana mahali hapo.
shetani ni
roho na kwakua ni roho huwezi kumgusa, kumuona, kumuhisi wala kumshika ila
anachofanya anapotaka kutenda kazi anaingia ndani ya mtu na wewe unaweza
ukaanza kumlaumu mtu kumbe ndani ya huyo mtu yuko shetani.
Hapa
malaika wa Mungu alikua amesimama ili kumtegemeza Yoshua na shetani alisimama
ili kushindana nae, hii inatuonyesha kumbe wako viumbe wa rohoni wanaosimama
ili kututegemeza na wako wanaosimama ili kushindana nasi, hapo ulipo wapo
wanaosimama ili kukusaidia usonge mbele na wako wanaokusaidia ili kurudi nyuma.
kwakua
shetani ni roho anaweza akaingia ndani ya mtu aliye karibu yako ili kuleta
uharibifu maishani mwako,anaweza akaingia ndani ya mume/mkeo, anaweza akaingia
ndani ya rafiki (shetani akaingia ndani ya Yuda aitwaye Iskariote ili amsaliti
Yesu) na anaweza akaingia hata ndani ya
mnyama( Yesu aliwaamuru mashetani wakaingia ndani ya nguruwe na nguruwe
wakaangami abaharini)
Shetani
aliingia ndani ya Yuda baada yakufungua mlango wa kutaka fedha katika maisha
yake, kwa maana nyingine kwa namna ya rohoni sio yuda aliyemuangamiza Yesu bali
ni shetani aliyekua ndani ya Yuda, Yuda alitumika kama chombo.
Shetani
hawezi kutenda kazi mpaka apate mahali pa kuingilia, ndio sababu kuna watu
wanakupinga bila sababu lakini ni kwasababu shetani anatenda kazi ndani yao.
na shetani
anaamua kukaa kwenye mkono wako wa kuume au mkono wakjo wenye nguvu, eneo lile
unalolitegemea likutoe katika umasikini ndio shetani anakaa hapo, au unakua na
mtoto wako unategemea afanye vizuri katika masomo hapo ndipo shetani
anashambulia.
Hii ndio sababu
kuna watu baadhi ya mambo wanaweza kufanya, anaweza kuhudhuria harusi, ndoa
anaweza kufunga lakini hata afanyeje nyumba hawezi kujenga, hii inamaana lile
eneo unalolitegemea analikalia kwa nguvu kutokana na mavazi ya uchafu yaliyo
katika maisha yako.
zamani
palikua na watu waliokua wakimtegemeza mfalme na wao walikua wakiiitwa mkono wa
kuume, mfalme alikua akitaka kufanya jambo kwa kumtumia mtu huyo anakua na
uhakika jambo litafanyika vizuri. Nae shetani anapoliona eneo hilo la maisha
yako anakuja na kulikalia, Mungu anaweza akawepo na malaika wake wanaweza
kuwepo lakini bado shetani akapata nafasi ya kuendelea kukaa hapo kwasababu ya
mavazi ya uchafu ambayo ndio mlango.
ukitaka
upenyo huyu aliye mkono wa kuume anasimama ili apingane nawe, ndio sababu Mungu
alipomuona mtumishi wake anapigwa akaamuru avuliwe nguo zake za uchafu, hakuna
namna ya kumuokoa, na yule aliye mkono wa kuume amepata nafasi kwasababu ya
nguo zenye uchafu.
Nguo za
uchafu zilipotolewa ndipo likamjia neno kuwa yeye ni kinga( kaa la moto kutoka
madhabahuni kwa Bwana) cha Bwana.
Ni maombi
yangu leo Mungu akuondolee vazi lako la uchafu na uwe kama moto kwa wale adui
zako na wale wanaokuwazia mabaya washindwe kukugusa kwa jina la Yesu.
NINI MAANA
YA NGUO ZA UCHAFU?
Nguo za
uchafu ni yale mambo yasiyompendeza Mungu mtu anayotenda nayo yanampa shetani
nafasi katika maisha yake. Hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kusema shetani
karibu ndani ya moyo wangu uwe muharibifu wa maisha yangu.
Shetani
anatumia milango ambayo tunafungua katika maisha yetu na anapoingia ndani ya
maisha yetu anasababisha matatizo ambayo yanakua vigumu kujitoa mpaka tuondoe
milango hiyo.
MILANGO
SHETANI ANAYOTUMIA KATIKA MAISHA YA WATU
1) Mlango
wa Mila
Mila ni
desturi ambazo watu wamezoea kuzitenda kil asiku na zikawa sehemu ya maisha
yao. Kuna mila nyingi sana zinazotengeneza milango ya shetani maishani mwao.
mf. Mila ya
kumaliza msiba. Kwenye tamaduni za kawaida kumaliza msiba ni siku ya arobaini
tangu marehemu afariki watu wanatumia kusherekea na kucheza,
mf.2. Ni
kunyoa nywele wakati wa msiba, nikupe historia kidogo utaratibu wa kunyoa
nywele ulitokea mashariki ya kati kutoka sehemu inaitwa mesopotamia, kwasababu
watu walianzia hapo kuwa na tamaduni za kuishi pamoja( Socialization) na
kutokea hapo watu wakaanza kusambaa duniani.
Ndio sababu
watu wa Ethiopia wanafanana na watu wa Rwanda na wairaki wa Tanzania kwasababu
wote wanaasili moja, na hizo tamaduni walitoka nazo huko walikokua.
Watu
walikua wakinyoa nywele na kuziweka katika makaburi na kusema mahali huko
ulikokwenda na sisi tutakuja huko huko, walikua wanaamini mtu anapokufa anaenda
mahali panaitwa Sheol(Kuzimu)
Hii ndio
sababu unakuta familia inakua na vifo vya kufanana, wote wanagongwa na magari,
au ugonjwa wa aina moja.
nilikutana
na baba mmoja akaniambia mchungaji tarehe 3/8 ambayo ni kesho nafariki,
nikashangaa sana nikamuuliza kwanini,
akasema nilikua na kaka yangu mmoja alifariki tarehe 3/8 kwa ajali ya gari,
baada ya miaka mitatu mingine dada yetu mkubwa akafa tarehe 3/8 kw aajali pia,
kaka yetu mwingine alikua uingereza baada ya miaka mitatu mingine ilipofika
tarehe 3/8 akafa katika ajali ya ndege, nimebaki mimi tu na imepita miaka
mitatu tayari nakesho ni tarehe 3/8. nisaidie mchungaji.
Laana haiji
katika maisha ya mtu isipopata nafasi. Mithali 26:2. Laana ni ya rohoni lakini
inadhihrika mwilini.
Milango
hiyo ndio nguo za uchafu
Kuna mambo
yanayofanana katika familia, mfano Ibrahimu alipokua mtu mzima akaenda Misri na
alipofika huko akadanganya mkewe ni dada yake, na Isaka nae alipokua na mke
njaa ilipotokea wakakimbilia nchi ya jirani nae akadanganya kuwa mkewe ni dada
yake.
Ndio sababu
Daniel na wenzake walikataa kula chakula cha mfalme nebukadneza kilichotolewa
kwa sanamu, waliacha kufuata mila zisizofaa.
ITAENDELEA
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NASI:
0714729805
0716671440
0718104333
0717727206
Comments