ASKOFU ZACHARIA KAKOBE AMPONGEZA GWAJIMA KWA KUKUNUA NDEGE YA KUHUBIRIA INJILI.



Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Kanisa la Ufufuo na Uzima chini ya Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima ambae ni Mhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja. 

Kanisa hilo ndio linaloongoza kwa idadi ya watu ambao wanakutana sehemu moja katika kumwabudu MUNGU, Kwa siku za jumapili wanasali pamoja pale Tanganyika Packers zaidi ya watu 70,000. Huku pia huduma hiyo ikifanikiwa kufungua huduma katika maeneo mengi Tanzania na nje ya Tanzania.

  Kwa upande mwingine Mhubiri mwenzake na Gwajima, Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati akimpongeza Mchungaji Gwajima kununua  Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’ 

‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’  Alisema Askofu Kakobe.
Hata mimi Peter Mabula nalipongeza sana kanisa la Ufufuo na Uzima kwa hatua nzuri ya ushindi dhidi ya shetani.
IENDE MBELE INJILI YA YESU KRISTO TENA NI KWA UTUKUFU WA JEHOVAH MWENYE NGUVU. 
Baadhi ya wachungaji kutoka Japani ambao walifanikisha ununuzi wa helikopta hiyo . Pembeni mwenye Mic ni Mchungaji Josephat Gwajima, hapa ilikuwa ni katika ibada ya kumshukuru MUNGU kwa kupatikana kwa Helkopta hiyo.

Kwa upande mwingine kanisa la Askofu Kakobe yaani FGBF wanasherekea miaka 25 ya kumzalia BWANA YESU matunda kwa maelfu ya watu kumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yao.

Ni miaka 25 ya Tanzania kwa YESU.




Askofu Zacharia Kakobe ambaye ni mbeba maono wa huduma ya Full Gospel Bible Fellowship(  FGBF), Kulia na kushoto ni maaskofu wa kanisa hilo kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania. Hongereni sana FGBF kwa kazi nzuri ya BWANA na hakika mmemzalia BWANA YESU matunda mengi. Ni miaka 25 ya mafanikio.

Comments