TAMANI KUJAZWA ROHO MTAKATIFU

BWANA YESU asifiwe!
Karibu tujifunze.

Kama Kuna Jambo Muhimu Kwa Kila Mwamini Ni Ujazo Wa ROHO MTAKATIFU. Mithali 1:23 Inasema " Geukeni Kwa Ajili Ya Maonyo Yangu; Tazama, Nitawamwagia Roho Yangu, Na Kuwajulisheni Maneno Yangu" Na Tena Biblia Inaendelea Kusema Katika Matendo 2:38 Kwamba " Tubuni Mkabatizwe Kila Mmoja Kwa Jina Lake YESU, Mpate Ondoleo La Dhambi Zenu, Nanyi Mtapokea Kipawa Cha ROHO MTAKATIFU" 

-Tunatubu Kwanza 
-Na Kubatizwa 
-Na Kupata Ondoleo La Dhambi 
-Na Kuwa Safi
 Ndipo Tunakuwa Tumetoa Nafasi Ya Kumpata ROHO MTAKATIFU. 

ROHO MTAKATIFU Ni Muhimu Sana Kwa Watu Wote, Watumishi Kwa Waumini Maana Hauwezi Kushinda Dhambi Bila Msaada Wake.
 Warumi 8:14  ''Kwakuwa wote wanaoongozwa na Roho wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''

Kazi Za ROHO MTAKATIFU Ni 

1.   KUTUKUMBUSHA, 
2.   KUTUONYA, 
3.   KUTUOMBEA, 
4.   KUTUFARIJI, 
5.   KUTUHIMIZA, 
6.   KUTUELEKEZA, 
7.   KUTUONYESHA MIPANGO YOTE YA shetani,
8.   KUTUPA KARAMA ZAKE 9 KAMA VILE YEYE APENDAVYO KUMGAWIA KILA MTU, 
9.   KUTUPA HUDUMA ZAKE 5 KAMA VILE APENDAVYO YEYE, 
10.  KUTUOKOA KUTOKA KWENYE MIKAKATI MIBAYA YA shetani 
11.  KUTUFUNULIA MAFUMBO YA MUNGU. 

Ndugu ni muhimu pia kujua kwa mwanadamu yule ambaye hana ROHO wa KRISTO huyo sio wa KRISTO na huyo ROHO wa KRISTO ndiye ROHO MTAKATIFU, hivyo unaona ni jinsi gani ROHO MTAKATIFU alivyo muhimu sana kwa kila mtu. Ndugu yangu ukimpokea ROHO MTAKATIFU, huo ni muujiza mkuu na tunza sana muujiza wao huo. Usimhuzunishe ROHO na mtii ROHO wa MUNGU.

Ndugu Yangu Tamani Sana Kuwa Na ROHO MTAKATIFU.

 Kazi Mojawapo Ya ROHO MTAKATIFU Ni KUTUKUMBUSHA. Unajua Anatukumbusha Nini? 
- Anatukumbusha Yaliyopita, 
-Yaliyopo 
-Na Yajayo. 

Ni Muhimu Sana Kuwa Na ROHO MTAKATIFU.
 Biblia Inatushauri Kwamba Katika Katika Waefeso 5:18-21 " Tena Msilewe Kwa Mvinyo, Ambamo Mna Ufisadi; Bali Mjazwe ROHO ; Mkisemezana Kwa Zaburi Na Tenzi Na Nyimbo Za Rohoni, Kuku Mkiimba Na Kumshangilia BWANA Mioyoni Mwenu; Na Kumshukuru MUNGU BABA Siku Zote Kwa Mambo Yote, Katika Jina Lake BWANA Wetu YESU KRISTO; Hali Mnanyenyekeana Katika Kicho Cha KRISTO."  

Ndugu Yangu Ni Muhimu Sana Kuwa Na ROHO MTAKATIFU. 
Na Mkristo Bila Kuwa Na ROHOMTAKATIFU Ni Kama Gari Bila Usukani, Na Hata Kama Wewe Ni Dereva Mtaalamu Kiasi Gani Kama Unaendesha Gari Ambayo Haina Usukani Lazima Tu Ukifika Kwenye Mataa Ya Ubungo Utagonga Magari Mengine, Lazima Tu Ukifika Kariakoo Utagonga Nyanya Za Watu, Nakuambia Ukifika Mlima Kitonga Lazima Uanguke Na Hata Ukifika Mlima Sekenke Lazima Gari Lako Lirudi Nyuma Na Kupata Ajali. Hivyo Tamani Sana Kuongozwa Na ROHO MTAKATIFU.

 Ukiwa Na ROHO MTAKATIFU Katika Ujazo Mkubwa Uko Salama Sana, Atakujulisha Mambo Makubwa Sana. 
Hata Saa Ya Kuondoka Kwako Duniani Ikikaribia Atakuambia " Mwanangu Kaa Tayari Kwa Kuondoka". 

Kuna Watu Wana ujazo Kidogo Tu Wa ROHO MTAKATIFU Na Huona Mambo Madogo Lakini Wapo Waliofurika ROHO Huona Mambo Makubwa Sana. Kuna Watumishi Wamepatwa Na Mafuriko Ya ROHO MTAKATIFU Hadi ROHO Huzungumza Nao Kwa Sauti Kama Vile Ndugu Anaongea Na Rafiki Yake. Natamani Nifikie Hatua Hiyo Na Nibaki Kwenye Hatua Hiyo Siku Zote. 

Mara Chache Niliisikia Sauti Ya Moja Kwa Moja, Siku Moja Niliona Roho Ya Mauti Ikimfatilia Dada Mmoja Wa Kanisani Kwetu, Nikaambiwa Nimuombee, Nikaomba Kama Dk 2 Nikalala, Baadae Tena Nikaambiwa Nimuombee Mtu Yule Maana Yuko Kwenye Hatari Kubwa, Nikaomba Tena Kama Dk 5 Huku Nasinzia Sinzia Maana Siku Hiyo Nilikuwa Na Usingizi Mzito Sana Lakini Baadae Kama Nusu Kupita Nikasikia Sauti Ya Moja Kwa Moja Ikiniambia Nimuombee Yule Dada, Ndipo Nikaamka Na Kuanza Kuangalia Nani  yuko jirani yangu ananiambia jambo hilo. maana mwanzo nilisikia sauti ya ndani kwa ndani lakini wakati huu sauti ilikuwa nje tena ina msisitizo mkubwa, Nikiwa nashangaa tena nikasikia tena ile sauti ikiniambia ''Omba'' Nikaanza Kuomba. Nikaanza kuomba na kesho yake nilipomuona yule dada nikamuuliza jana usiku ilikuwaje akasema aliumwa ghafla hadi kuzimia na hakika ailijua amekufa ila MUNGU akamponya Ghafla, kumbe muda ule naomba ndio muda ambao alikuwa kwenye vita kali. Natamani sana ROHO MTAKATIFU aseme nami juu ya kila jambo linalotaka kutokea.


Ndugu zangu Wateule Wa MUNGU Tutamani Sana Ujazo Wa ROHO MTAKATIFU Maana Yeye " Ni MUNGU Atendaye Kazi Ndani Yenu Kutaka Kwenu Na Kutenda Kwenu, Kwa Kulitimiza Kusudi Lake Jema- Wafilipi 2:13" 

Na Tena "Tukiongozwa Kwa ROHO MTAKATIFU Hatuko Ndani Ya Sheria- Wagalatia 5:20". 

Kila Mtu Atamani Kuwa Na ROHO MTAKATIFU, Na Kila Mmoja Ajue Kwamba " Waabuduo Halisi, Imewapasa Kumwabudu MUNGU Katika ROHO Na Kweli - Yohana 4:24'' 

Na Kila Mteule Ni Muhimu Kutambua Kwamba "au Hamjui Ya Kuwa Ninyi Mmekuwa Hekalu La MUNGU, Na Ya Kuwa ROHO Wa MUNGU Anakaa Ndani Yenu? Maana Mlinunuliwa Kwa Thamani, Sasa Basi Mtukuzeni MUNGU Katika Miili Yenu-1 Kor 3:16, 6:2. 

 ROHO MTAKATIFU Hutufunulia Na Kutusaidia Hata Tusiyoyajua. Siku 1 Nilikua Nasafiri Ghafla Nikawa Rohoni Na Kuona Gari Ndogo Baloon Imesimama Katikati Ya Barabara, Nikaanza Kuomba Nikivunja Mipango Ya Adui, Baada Ya Dk 10 Kupita Ni Kweli Gari Ndogo Ilitokea Nyuma Yetu Na Kufika Mbele Dereva Ikamshinda Kidogo Tupate Ajali, Watu Walimshukuru Dereva Lakini Nilijua ni MUNGU Katuokoa. Baada ya kumkwangua huyo mwenye gari ndogo tukashuka na kumkuta amelewa huku anaendesha gari, baadae tukaondoka. Namshukuru MUNGU BABA kupitia ROHO MTAKATIFU maana aliinionyesha na mimi nikasimama katika zamu yangu ya maombi.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments