Ushuhuda Huu Ukusaidie Na Mungu Akupe Ufahamu.




Siku Moja Nikiwa Nimeenda Kufanya Huduma Mahali Fulani, Mkoani Dodoma. Nilikutana Na Mama Mmoja Ambae Alinielezea Matatizo Yake. Kwa Kifupi Ni Kwamba Ardhi Ilimkataa Kila Alipo Lima Hakufanikiwa Na Alipofuga Mifugo Ilikufa Na Hakupata Faida Kutokana Na Kazi Ya Mikono Yake.

Siku Nilipokutana Nae Aliniomba Nimuombee Ili Mungu Amfungue Katika Vifungo Vinavyomsumbua. Nilipotaka Kuomba Mungu Aliniambia Nisimuombee Ila Alinipa Maelekezo Kwa Ajili Yake Na Maelekezo Yake Yalikuwa Hivi,

Kwanza Akubali Kumkabidhi Mungu Njia Zake Na Pia Amuahidi Kita Atakachomfanyia Mungu Pindi Atakapomfanikisha Katika Kazi Ya Mikono Yake Nami Nilimpa Maelekezo Kama Nilivyoelekezwa Naye Akayapokea, Na Akaweka Nadhiri Kwa Mungu Nami Nikiwa Ni Shahidi, Kisha Nilimshukuru Mungu Na Nikaondoka.

 Baada Ya Muda Fulani Nilifika Eneo Hilo Tena Kwa Ajili Ya Kufanya Huduma Na Nilipofika. Baada Ya Kuwa Nimemaliza Huduma Niliyoiendea Alinitaka Kwenda Nyumbani Kwake Na Nilipofika Aliniambia Kuwa Baada Ya Kumwekea Mungu Nadhili Yake Mungu Amemfanikisha Na Alikuwa Akiishi Kwa Nyumba Ya Kawaida Ila Sasa Amepata Faida Kubwa Na Ameshapata Matofali Na Mabati Ya Kutosha Kwa Ajili Ya Kujenga Nyumba Kubwa. 

Tulimshukuru Mungu Kwa Kuwa Kila Alilotuahidi Lilitimia.
Ushauri Wangu Kwako Ni Huu Kama Unaona Mambo Yako Hayaendi Usikimbilie Tu Kuomba Bali Utafute Uso Wa Mungu Kisha Mwambie Haja Ya Moyo Wako Ili Musemezane Na Usikilize Maelekezo Na Kuyafanyia Kazi Nakuahidi Kuwa Kwa Kufanya Hivyo Utafanikiwa Kwa Jina La Yesu Aliye Hai.

By Amin Yesu Utaokoka.

Comments