YAJUE MAKUNDI MATATU YA WAKRISTO KATIKA KANISA LA LEO




Katika Kanisa kuna aina tatu za Wakristo. Iwapo na wewe ni wa Kristo, chunguza, utagundua kuwa uko kwenye kundi mojawapo kati ya makundi haya yafuatayo.
1. Wakristo wa Rohoni
2. Wakristo wachanga
3. Wakristo wa Mwilini

1. WAKRISTO WA ROHONI
Hawa ni Wakristo waliomwamini Kristo na kudumu katika Neno la Mungu, likabadilisha maisha yao yakafanana na Neno (Yesu)
- Hata kabla hajasema habari za Yesu, utamtambua kama ni wa Yesu.
- Hakuna kitu anacholinda kama Wokovu wake.
- Huwezi kuona mizaha kwake.
- Ni mwaminifu katika yote,
- Hutasikia akisengenya wala kunung’unika.
- Kipaumbele chake ni kufanya Mambo ya Mungu
- Ndiye Yule mwenye kumzalia Mungu matunda (Math 13:23)
- Huongozwa na Roho Mtakatifu, na hamuuzunishi Roho. (Rum 8:14)
- Biblia ni rafiki yake mkubwa
- Bora kutoa kuliko kupokea

2. WAKRISTO WACHANGA
Hawa ni Wakristo waliomwamini Yesu karibuni, wanashauliwa wayatamani maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili waukulie wokovu. (1Petro 2:1-2)
- Uwezo wa kupambanua jema na baya ni mdogo
- Chakula kigumu hawakiwezi. (Uwafundishe wema wa Yesu, habari za majaribu kama kipimo cha imani, usiziseme kwanza) (1Kor 3:1-2)
- Usishangae kuona utu wa kale
- Hupenda kupewa kipaumbele na kutendewa.
- Wokovu ni kwa faida yake lakini hutaka kubembelezwa.
- Kusoma Neno na kuomba ni mpaka akumbushwe.
- Mabadiliko huweza kuwa ya haraka katika kukua kutokana na jitihada ya kumtafuta Mungu aliyonayo mtu.

3. WAKRISTO WA MWILINI
Hawa ni wale waliookolewa siku nyingi, lakini maisha yao hayabadiliki kutokana uvivu wa kujifunza. (Ebr 5:11-12)
- Ana sura mbili, ya Kanisani na ya mitaani.
- Akiwa na watu wengine wasiomjua Yesu, haionekani tofauti.
- Huona aibu kujitambulisha kama ni wa Yesu.
- Ukishika simu yake kuangalia vitu alivyohifadhi utashangaa!
- Ni mtu wa mizaa.
- Akitukanwa hurudisha matukano.
- Mwepesi kukasirika
- Hujisifia kwa miaka waliyonayo kwenye wokovu.
- Hapendi kukemewa akikosea.
- Kusema uongo si tatizo
- Ni kikwazo kwa wanaotaka kuingia kwenye Ufalme wa Mungu.
- Mungu bado anawapenda, ingawa hawako moto wala baridi, nisawa na Kanisa la Sardi na Laodikia. Anawavumilia ili watubu, wasipotubu hukumu ya kutisha inawangoja. (Ufunuo 3:1,19)

MARAN ATHA! BWANA YU AJA!

MUNGU akubariki sana.
By Alex Emmanuel Bubelwa

Comments