Utukufu apewe BWANA |
Watumishi wa MUNGU Amos Omela Fumbuka na Lucy Daniel Wamefunga ndoa katika kanisa la Kawe Pentecostal Church(KPC) Kawe.
Ndoa hiyo aliifungisha Askofu wa jimbo la Dar es salaam kanisa P A G(T) Thomas Dige.
Askofu Dige aliwasifu maharusi kwa uaminifu wao kwa MUNGU na kuwataka vijana wengine kuiga mfano huo. Kiongozi wa ibada hiyo alikuwa ni Mchungaji Kiongozi wa KPC Mchungaji Elly Boto ambapo kabla ya kumkaribisha askofu Dige alisema kuwa vijana hao wamekamilisha taratibu zote ambazo zinatakiwa na hata Darasa la ndoa wamejifunza na kufanya vyema sana na wanahitaji pongezi.
“Apataye mke (mume) apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA “-Mithali 18:22.
pia kumbuka Amos ndiye aliyetoa ushuhuda huu wa ajabu na MUNGU alimtetea na sasa amempa baraka mpya kama hukusoma ushuhuda huo FUNGUA HAPA
Lucy akiwa tayari kuingia kanisani. |
ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIKITENGANISHE. |
Amos akiingia agano la ndoa takatifu na Lucy |
Ni kama Lucy anasema hivi ''Nimekuchagua Amos ili uwe wangu wa maisha'' |
Lucy akisaini cheti cha ndoa. |
Kwa YESU ni raha sana |
Baada ya kufunga ndoa, hapa wakiwa na ndugu na marafiki nje ya kanisa. |
Mambo mazuri sana |
Hakika wamependeza sana. |
Nakurudisha nyuma kidogo '' Hapa ni kipindi Amos na msimamizi wake wakiingia kanisani kanisa zima walitoka nje ili kumsindikiza.'' |
Amos anasema kwamba ''WEWE LUCY NDIO MKE WANGU'' Na Lucy naye anasema ''AMOS WEWE NDIO MME WANGU'' |
Wakijiandaa kwenda beach kupiga picha |
Tunafurahi na wanaofurahi. |
Ukumbini |
Keki |
BWANA YESU awafunike, awape watoto na awape familia njema. mbarikiwe sana tena sana watumishi wa MUNGU. |
Comments