Baraka kutoka mlima pa Sayuni

Saarnaajaseminaari Mbeyassa
Teuvo Kopra  na Linnea Korpa kutoka Finland wakiwa na watumishi wa MUNGU nchini Tanzania.

  Na Teuvo Kopra, Finland.


ZABURI 133
    Tusome Zaburi mia moja, thelathini na tatu. Ina mistari mitatu tu.
  Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele. (ZAB 133:1-3)
  Hii ni Zaburi fupi. Daudi ameandika Zaburi hii. Biblia ina jumla ya Zaburi sabini na tatu zilizoandikwa na Daudi. Zaburi ni nyimbo. Zilizoimbwa nyumbani na katika sherehe.
  Wimbo huu unasema ni vizuri tukiishi katika mapatano. Halafu tunaelezwa juu ya baraka tukiishi katika mapatano. Katika mstari wa mwisho kuna wazo, kwamba kuna umande wa Hermoni. Umande huo unakwenda mpaka milima Sayuni. Kwani Mungu ameahidi baraka milimani pa Sayuni. Baraka hizo ni za milele, hata milele. Na baraka hizo zina uzima wa milele. Tusome tena mstari wa tatu.
  Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, naam, uzima hata milele. (ZAB 133:3)
  Biblia ina mifano mingi. Ni hivyo hata katika Zaburi mia moja thelathini na tatu. Hapa inazumgumzia milima mingi ya Sayuni. Kama tungetafuta ni jinsi gani Biblia inazungumzia Sayuni, tungepata mambo mengi.
  SAYUNI
  Biblia inaita sehemu ile ya hekalu ya Yerusalemu Sayuni. Katikati ya Yerusalemu kuna eneo kubwa ambapo Sulemani alijenga hekalu. Siku hizi kuna misikiti miwili ya Kiislamu. Biblia inapaita sehemu hii Sayuni. Pia Yerusalemu nzima inaitwa Sayuni. Hata Israeli nzima inaitwa Sayuni. Biblia inazungumzia pia mlima Sayuni wa Mbinguni.
  Tulisoma kwamba Mungu ameahidi baraka za milele juu ya milima Sayuni. Inafananishwa na umande wa Hermoni. Umande wa Hermoni ni nini? Hermoni ni mlima mrefu katika Kaskazini ya Israeli. Wakati wa baridi theluji inanyesha nyingi. Theluji zinaweza kunyesha mita mingi, mita saba, au mita kumi. Halafu kuna wakati wa joto na theluji inabadilika kuwa maji. Maji yanafuata mto Yordani kuelekea kusini. Maji yanaingia ziwa la Genesareti na kutoka hapo yanatolewa na bomba nchi nzima. Hivyo Hermoni inatoa maji kwa Israeli nzima.
  Zaburi mia moja thelathini na tatu inafananisha hayo kwa mambo hayo, kwamba baraka zitatoka milima Sayuni, yanayoleta baraka, naam, uzima hata milele. Kama vile maji ya Hermoni yanayoenea Israeli nzima, ni sawa na baraka za milima Sayuni yanasambaa nchi nzima. Baraka hizi zinasambaa kwa mataifa yote. Baraka za Sayuni zimefika pia Afrika na hata kwetu pia  BARAKA NNE
  Tukisoma Biblia, tunagundua kwamba baraka nyingi kutoka Sayuni.
Biblia ina baraka nne tofauti zinazoitwa baraka za milima Sayuni. Baraka ya kwanza kutoka milima Sayuni imekwisha kabla ya Kristo. Wakati wa baraka ya pili kutoka milima Sayuni inaendelea. Ya tatu na ya nne zitakuja.
  BARAKA YA KWANZA
  Baraka ya kwanza katika Biblia ilioanza mlima Sayuni Yerusalemu ni wakati ule Sulemani alipojenga hekalu la Sayuni. Sulemani alikuwa mfalme wa Israeli kama miaka elfu tatu iliopita. Baba wa Sulemani alikuwa mfalme Daudi aliyenunua sehemu ya kiwanja kwa ajili ya hekalu. Sehemu hiyo inaitwa Sayuni. Iko Yerusalemu. Nimeenda huko mara chache na kuona mlima Sayuni. Sulemani alijenga hekalu katika mlima huyo. Hekalu lilitumika miaka mia tatu, sabini na tano, halafu ikabomolewa. Baadaye likajengwa tena. Wakati wa Yesu hekalu ilirekabishwa na kupanuliwa.
  Tulisoma Zaburi mia moja thelathini na tatu kwamba Mungu amepanga baraka inayoleta kwa watu maisha ya milele, yaani uzima hata milele. Baraka hizi zilikuwa za aina gani wakati wa Sulemani na baada yake? Baraka hizi za milele zilipatikanaje toka hekaluni?
  Biblia inaeleza, kwamba watu wote wamefanya dhambi. Tumefanya dhambi mbali mbali. Dhambi zinamtenganisha mtu na Mungu. Lakini Mungu anampenda mtu mwenye dhambi. Anataka mtu asamehewa dhambi zake na apate mawasiliano na Mungu. Ndivyo Mungu alitoa njia ya kutoa dhabihu ya Agano la Kale. Biblia inazungumzia dhabihu mbali mbali. Dhabihu ilipotolewa, dhambi ilihukumiwa na mwanadamu alipata msamaha wa dhambi. Biblia inaelezea aina tano za dhabihu za watu walipofanya dhambi na jinsi walivyomkaribia Munbu nazo. Kila dhabihu ina ujumbe wake. Mambo ya Walawi inaeleza dhabihu hizi.
Tunatumia jina: Dhabihu, lakini Biblia inatumia pia jina: Sadaka. Kuna ”Sadaka ya kuteketezwa, Sadaka ya unga, Sadaka za amani, Sadaka ya dhambi na Sadaka ya hatia.”
Ujumbe wa sadaka, yaani dhabihu ni mfano wa agano aliyolifanya Yesu. Na mfano wa upatanisho. Yesu alipokuwa msalabani ina maana nyingi. Zaidi tunasema kwamba Yeye alipeleka dhambi zetu msalabani. Ndiyo, Alifanya hivi.
  Tulisoma Zaburi mia moja thelathini na tatu, kwamba Mungu ameamuru baraka kwa mlima Sayuni kupitia hiyo watu wanapata maisha ya milele. Maisha ya milele watu walipata kwa njia ya dhabihu ya Agano la Kale. Hayo yalitolewa katika Hekalu alilolijenga Sulemani.
  Tusome kuhusu Sadaka ya Hatia. Biblia inasema mtu alipotaka kusamehewa dhambi na kuwasiliana na Mungu, ilimbidi kutoa Sadaka ya Hatia.
  Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa Bwana, ni kondoo mume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani; na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana, naye atasamehewa; katika jambo lo lote alifanyalo hata akapata kuwa mwenye hatia kwalo. (LAW 6:6,7)
  Kuna sadaka zingine.
Kama mtu alikuwa maskini sana na hakuwa na kondoo, aliweza kuleta sadaka ya mtu maskini. Hiyo ni njiwa au watoto wa njiwa. Tunakumbuka, wazazi wa Yesu walileta sadaka hizo, mwezi moja baada ya kuzaliwa kwa Yesu. Walikuwa maskini na hawakuweza kununua kondoo. Mungu anataka maskini na matajiri waweze kumkaribia. Ndiyo maana kuna sadaka za maskini. Biblia ina maelezo mengi kuhusu kutoa sadaka. Nitaeleza hayo kwa ufupi.
MUNGU akubariki.
ITAENDELEA........
bY Teuvo Kopra.
 

Comments