HIVI NDIVO ILIVYOKUWA KATIKA TAMASHA LA NYIMBO ZA INJILI ZANZIBAR.

Mchungaji Daniel Kolemba ikihubiri katika tamasha hilo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita lilifanyika tamasha la nyimbo za injili Zanzibar
.Baada  ya tamasha  kufunguliwa  kwa  maombi  MCHUNGAJI  DANIEL  hapo  juu  alitoa  neno  liliokuwa  na  ujumbe  ufuatao:.
MAKANISA  YOTE  ZANZIBAR  TUDUMISHE  UMOJA  WA  KWELI :






Umoja  wa  kweli  katika  makanisa  yote  hauna  madhara  yoyote, kwa  masilai  ya  mtu  mmoja  au  kundi  lolote.

ROHO  YA KUBAGULIWA :

1: Roho ya kubaguliwa  inatawala sana  hapa ZANZIBAR  na inaumiza sana kwa watoto wa Mungu na inawanyanyapaa  na hivyo uwakosesha uhuru  wa kuabudu  na kusifu  Mungu aliye hai.Kwani wakati wa kusifu na kuabudu utishiwa kuchomewa makanisa .Waamuzi 11:1-11.

2:  Usimbague  mtu aliye umbwa na MUNGU   ( Mwanzo 4:6)

3:  Aliendelea  kusema kuwa roho ya kukataliwa   inauwa  sana  na  inaweza  kusabisha  magomvi  na  uwaduwi.

4: Kaini  kwasababu   alikataliwa  na  MUNGU  roho  ya  kukataliwa  ilimsumbua  sana  kila  alipokuwa  akienda.

             Mwisho  alihitimisha  kwa  kufanya  maombezi  makubwa  dhidi  ya  kisiwa  cha  ZANZIBAR.

Na  baada  ya  hapo  tamasha  rasmi  la  kumtukuza  MUNGU  lilianza.




  1. Hao  ni  waimbaji  wa kwaya  ya Full pentecoste  Tomondo  Zanzibar  wakimtukuza  Mungu  aliye  hai.
    2: Hiyo ni kwaya  ya KKKT MWANAKWEREKWE   walioungana  na  kwaya  nyingine  nyingi  katika  kusifu  na  kuabudu  yaliyofanyika  kwenye  tamasha.
    3: Picha hiyo  hapo juu ni MRS MABUMBA akimwimbia  Mungu kwa  wimbo  wa mbegu  zilizopandwa  kwenye   shamba.

    4:Mwimbaji  wa  nyimbo  za  Injili  Hapo  juu  aliyevaa  kaunda  suti ni   Mwano Emiliano  akimwimbia  BWANA wimbo  wa  MWANADAMU.
    5:Bumbusudi   kwaya  hapo  juu  na chini  wakimtukuza  BWANA  kwa   wimbo  uitwao   BWANA  YESU NDIYE  UZIMA.
    6: Picha   hizo hapo  juu  ni  waimbaji  wa  kwaya  ya  TAG Kariakoo  Zanzibar  wakimtukuza  BWANA  kwa  wimo  wao  unaotamba  kwa  sasa  uitwao TULETE  MAVUNO  KWA  YESU    .

Comments