JE UNATAKA KUMWABUDU MUNGU KATIKA KWELI YAKE?





BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze.
Wateule wa MUNGU tuko safarini hapa duniani, hatujafika bado kule tuendako. Tuendako ni mbinguni ambako yako makao yetu aliyotuandalia BWANA YESU. Nampenda sana BWANA YESU maana alisema ‘’  -Yohana 14:2-3, Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.’’
-BWANA YESU kwenye maandiko hayo anaongea na wale waliompokea.
-Waliompokea YESU wana kibali cha kuishi mbinguni.
-Hawahitaji visa card maana Visa card yao ni kumpokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wao.
-Hawa ndio waabuduo halisi, waabuduo halisi tayari makao yao ya milele yako mbinguni yameshaandaliwa na BWANA YESU.
-Biblia inawashauri wateule hawa kuendelea tu kumwabudu MUNGU BABA katika roho na kweli, wasiyumbishe na dunia, wasiogope wanavyoviona kwa mwili bali wavae nira ya BWANA YESU siku zote.

JE UNATAKA KUMWABUDU MUNGU KATIKA KWELI YAKE?

Yohana 4:24 ‘’ MUNGU ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. ‘’
Kama unataka kumwabudu MUNGU katika kweli yake yote hakikisha unafanya yafuatayo.
-Waabuduo halisi humwabudu MUNGU katika Roho na kweli.
-Humwabudu MUNGU katika utakatifu.
-Humwabudu MUNGU katika ukweli.
-Humwabudu MUNGU katika KRISTO YESU pekee.
-Humwabudu MUNGU peke yake.
-Humwabudu MUNGU BABA siku zote za maisha yao.
-Humwabudu MUNGU bila dhambi.

Je unataka kumwabudu MUNGU BABA katika ukweli wake?
1.  Okoka. Yohana 1:12-13 ‘’ Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. ‘’  
BWANA YESU alikuja kukutafuta wewe ndugu ili tu akuokoe Luka 19:10 ‘’ Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. ‘’
      2.  Liishi neno la MUNGU. Zaburi 119:105 ’’ Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. ‘’ 
Ni baraka kubwa kulisikia neno la MUNGU na kulishika Luka 11:28 ‘’heri walisikiao neno la MUNGU na kulishika. ‘’
  3. KRISTO aishi ndani yako siku zote na wewe kaa ndani ya KRISTO siku zote.Warumi 8:10-11 ‘’ Na KRISTO akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa ROHO yake yeye aliyemfufua YESU katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua KRISTO YESU katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa ROHO wake anayekaa ndani yenu. ‘’ 
Mabadiliko hutokea baada tu ya kumpokea BWANA YESU, Hukumu zote za nyuma zinafutwa 2 Kor 5:17 ‘’Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ‘’
4.  Uwe mwanamaombi siku zote. Yohana 14:13-15 ‘’ Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu. ‘’ 
Ndugu maombi humkimbiza shetani, maombi huwadhuru wachawi, kwa maombi utakuwa huru siku zote na utapona kila ugonjwa na kila udhaifu Yakobo 5:16 ‘’Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. ‘’  
Maombi ni maisha. 1 Thesalonike 5:16 ‘’ ombeni bila kukoma;‘’
5.  Ongozwa na ROHO MTAKATIFU.Warumi 8:9‘’ Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake. ‘’,
6.  Usifanye dhambi.1 Yohana 2:1-2 ’’Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa BABA, YESU KRISTO mwenye haki,  naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. ‘’,  
 dhambi ni mbaya sana na dhambi huleta mauti na dhambi ni mama wa jehanamu maana dhambi huzaa jehanamu 1 Yohana 3:8 ‘’ atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. ‘’
 
7.  Uwe na imani thabiti. Waebrania 11:6 ‘’Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. ‘’   
Waliookolewa wana imani thabiti na walio na imani thabiti wako ndani ya KRISTO , Wamezaliwa upya kwa ROHO 2 Kor 5:7 ‘’Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ‘’

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
 
              mabula1986@gmail.com
  MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
  MUNGU Akubariki.

Comments