Wakatoliki wakataa kuwatambua mashoga


Makundi ya kikatoliki yanayopigania haki za wapenzi wa jinsia moja yameelezea ghadhabu yao kutokana na hatua ya maaskofu wa kanisa hilo ya kukataa mapendekezo ya kutangaza msimamo kuhusu mashoga, wasagaji pamoja na watu waliotalakiana na wanaoana.
Wakati wa kumalizika kwa mkutano wa maaskofu wa kanisa katoliki, Vatican ilishindwa kupata theluthi mbili ya kura za maskofu wa kuunga mkono maoni yao kuhusu masuala hayo.
Kundi la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Marekani la New Ways Ministry limesema kuwa hatua ya maskofu hao kuamua kujadili suala hilo ni matumaini ya siku za usoni.
Masuala hayo yanatarajiwa kuzungumziwa tena baada ya mwaka mmoja.
CHANZO: BBC SWAHILI

Comments