WAZAZI WANAOISHI NA MAHOUSEGIRL WACHAWI AU WASHIRIKINA.

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

Katika huduma zangu nimekutana na kesi za baadhi ya wazazi waliokuwa wanaishi na wasichana bila kujua historia zao za nyumba na baadaye wakaja kugundua kwamba wanaishi na mchawi ndani ya nyumba moja na housegirl huyo akawa anawafundisha watoto wa mabosi wake uchawi bila ya wanafamiliya kujua. Kumbe umechukua agent. Na shetani amemwaga maagent wengi kila mahali. Kumbe watoto wengine wanarithi mikoba ya kichawi na ushirikina toka kwa wazazi wao ili wakisha kuwa wakubwa wawe wataalamu zaidi katika kutekelza matakwa ya Shetani ya kuneza miroho ya kichawiwi na kishirikina.
Hawa wanapewa kazi maalum, special assignment wewe unabeba spirit ya uchawi na ushirikina. Kwa hiyo wanaambiwa kuwa kila wanapoenda wahakikishe hizo roho wanazitumia kuvuruga hizo familia. Kwa walokole kuwaingilia inakuwa shida sana. Kwa hiyo kinachofanyika ni kuleta agent akae ndani akae ndani ya mji alete taarifa zote. Kuna watu walikuja ofisini kwangu walikuwa na shida kutoka na housegirl. Niliwauliza mlimpata wapi wakasema tuliletewa. Watu hawa uwezo wao ulikuwa wa kawaida. Sasa house girl waliye kuwa naye alikuwa ana uwezo wa kuwaletea nyama kila siku. Yeye alichotaka ni kununua nusu kilo ya nyama. Ikisha nunuliwa watakula nyama wiki nzima. Nyama haipungui hadi wanjivunia kuwa housegirl huyo anjua bajeti. Maisha yanakuwa rahisi, vitu kidogo nyama kibao. Wakajiuliza nyama mbona haziishi kumbe housegirl analeta nyama kutoka huko anakokwendaga usiku wa manane.
Nyumba ya hawa watu ilikuwa ina vyumba viwili. Kimoja analala baba na mama kingine analala housegirl na katoto kao ka miaka kama mitatu mine hivi. Siku moja katoto kaligoma kwenda kulala na housegirl. Wakakalazimisha kakataa kabisa. Baba akaja akalazimisha akakachapana fimbo kakataa. Kakaenda kulala subuleni kwenye kochi. Baba akaenda kulala amekasirika kwamba mtoto amekataa kumtii. Mama akakafuata katoto sebuleni na kukauliza kwa upole kwa nini unakataa kwenda kula na dada. Kakasema mimi naogopa nikienda kulala dada atawaleta watu weusi tena. Mama akashtuka akasema njoo. Akakahoji, katoto kakaanza kueleza kuwa kila siku huwa watu wanakuja kutuchukua usiku tunaenda huko,tunavua nguo tunakula nyama na bibi Yule wa ile nyumba pale. Wazazi ndo wanshangaa huku housegirlwamekaa naye mika miwili. Katoto kadogo kameshaanza kufundishwa ushirikina. Wachawi huwa wanfundisha watoto wakiwa wadogo masuala ya kichawi. Hawafundishi watu wazima. Wachawi wote waliandaliwa wakiwa watoto wadogo. Ukiona mchawi kaacha uchawi kabisa ujue kakutana na neema ya Mungu. Kama wachawi wanaandaa watoto wao wakiwa wadogo kwa ajili ya shughuli zao, walokole wanshindwa nini kuwaandaa watoto wao katika Mungu? Watoto wengi wa walokole wanamjua Mungu kwa juu juu sana maana hawaandaliwi. Hebu angalia vile wachawi walivyo bize kuwaandaa watendakazi wao tokea wakiwa wadogo.Wazazi wa wakikristo wanasubiri watoto wakiwa wakubwa na wameshindikana wakiwa sekondari,ndipo wanaanza kuwakimbiza kwenye maombezi, jamani niombeeni mwanangu.

Hebu fikiria katoto kakiwa kadogo kameshafundishwa kula nyama mbichi, kukalia watu. Huyo akisha kuwa mtu mzima hawezi kuacha pasipo neema ya Yesu Kristo. Wachawi tunakaa nao majumbani na hata makanisani. Binti huyu walipomchunguza wakakuta vitu vingi vya kichawi, walikuta nywele za watu kwenye begi lake, wakakuta kucha, vibuyu, ngozi ngozi za wanyama na makorokoro mengi ambayo hata hayakufahamika kwa urahisi. Wazazi wakawa waoga wanogopa uchawi. Walimuita housegirl kwa nidhamu kuwa dada tumeishi nawe vizuri na tulikuwa tunakuhitaji wakati mtoto akiwa mdogo, na hali ya kipato chetu sio nzuri, kwa hiyo tunakuomba sasa urudi nyumbani, mshahara wako huo na nauli pia hela hii uwapelekee wazazi zawadi na leo hii uondoke. Binti alikwishajua akawafyonya akawaangalia kwa dharua akachukua begi lake akaondoka. Wazazi wakadhani amenda kijijini kumbe yupo mtaa wa tatu kwa bibi mmoja. Akawa anakuja hapo nyumbani na kuwasanifu akisema mnaendeleaje hapa. Wazazi wanasema toka siku ile hadi leo mtoto wao hayuko sawa. Akili yake haitulii, mara anaona maluweluwe, usiku kanashtuka, wanataka kuja kukafuata usiku. Hayo ni baadhi ya kuchukua wasichana wa kazi pasipo kuwa unawafahamu historia yao.
JIPATIE NAKALA YA KITABU HIKO SASA!


wasiliana na Mchungaji Peter Mitimingi kwa ajili ya kukipata kitabu hiki  kwa namba   0713 183939.

Comments