BOMU ULILOLIKUMBATIA KIUSTADI, UKIJIDHANIA MJANJA SIKU MOJA LITAKULIPUKIA TUU!

Na Lucy Marandu.

Katu; Nyuki hakumbatiwi! Pamoja na utamu wa asali yake lakini jino lake utaliona tuu kwa hakika!
Mwanadamu kujifanya hajielewi (kujiondoa ufahamu) Na kumheshimu mwanadamu mwenzie kuliko Mungu! Ni ajabu sana!

Yer 17:5 ''
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. ''

Eti unakuta kijana ana mchumba wake wanapendana, wanaishi maisha waliyoyachagua wao! Kuvaa watakavyo( Nusu uchi) Lakini ikifika wakati wa kwenda kutambulishana kwa wazazi/walezi; Utawasikia wakishauriana wao kwa wao,,,,,
"Mpenzi tukienda kwa wazazi usivae hivi... Mvulana atamshauri msichana asivae vazi la kuacha kitovu nje, matiti nje, skin lady nk






Msichana naye atamshauri mvulana asivae kata 'K' ikiwa nywele amesuka atashauria kunyoa,ikiwa anavaa hereni atamwambia avue, wakijua kabisa inaweza kuwasababishia vikwazo katika uchumba wao! Hapa tunaona ULE UFAHAMU WALIOJIONDOA, WANAURUDISHA KWA MUDA

Ni kweli kwamba watafaulu kuwadanganya wazazi/walezi wako kwa mavazi yao bandia ya kitambo tuu ili kukidhi haja yao, lakini jee Mungu aonaye sirini mmefaulu kumdanganyaa??

Wapendwa; kwa nini kuishi maisha ya jinsi hii jamanii?? Ikiwa umeweza kumheshimu/kumwogopa Mzazi wako kwa kutambua kuwa haya mavazi ni machukizo na yanaweza yakakukosesha mchumba umpendaye kwa nini usione na kwa Mungu ni machukizo zaidii?? Tena unajiita umeokoka! Nini sasa kulitukanisha jina la Mungu wakoo??

Kumbuka ndugu, Mungu wetu hadhihakiwi, chochote apandacho mtu hakika atakivuna Galatia 6:7-8 ''Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. ''

Umepanda mbegu ya uongo kwa wazazi wako bila haya na bila kumwogopa Mungu; tarajia kuvuma KUDANGANYWA na huyo mkeo au mumeo! Ukianza kusikia nilichelewa kikao, safari zisizo na kikomo nk usishangae..UJUE TUU KWAMBA ILE DHAMBI YA KUJIFANYA MJANJA INAKUTAFUNA!

Ushauri; kuliko kuwa mnafki mnafki ni bora kuwa huru! Maana Mungu wetu ameweka uwiano sawa mtu mwenyewe achague moja! Ufu 22:11-12 '' Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.   '',  
Kumb 30:15 ''Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; ''

Hakuna haja ya kujibana bana! Ukiamua kutenda mema tena kwa bidii, ukiamua kutenda mabaya fanya hivyo kwa bidii zaidi! Kwa sababu hakuna mbingu ya wanafki/ vuguvugu! Ufu 3:15-17 ''
Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.   '', Ufu 21:8 ''Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. ''
Mbarikiwe!
By Lucy Marandu.

Comments