FADHAIKO NI ADUI MKUBWA WA IMANI.

Na Godfrey Miyonjo.

BWANA YESU asifiwe sana wana wa aliye juu,
Ashukuriwe Mungu atuwaziaye yaliyo mema kila iitwapo leo,
Ni kwa neema yake tu tunaishi, na kwa upendo wake kwetu, ametuokoa.
Wapendwa, ninatamani sote tuliomwamini YESU tuendelee katika imani hii ya kweli hata ije siku ile ya kumlaki BWANA YESU mawinguni.
Pia ninatamani na wale ambao bado hawajamwamini YESU nao wamwamini, kwa maana YESU ndiye njia, na kweli, na uzima. YOHANA 14:6.
Ewe ndugu uliye na YESU tambua kuwa, shetani hapendi kabisa kusikia kuwa mtu anakiri wokovu hapa duniani,
Hutumia nguvu nyingi ili tufadhaike, mwisho wa siku tukate tamaa katika imani, kwa maana wanaoshindwa wote katika imani chanzo chake na fadhaa.
HII NI SILAHA KUBWA YA SHETANI KWA WANA WA MUNGU.
Kuna wakati alimtumia Sanbalati na Tobia ili kuwadhoofisha Wayahudi.
NEHEMIA 4:1-3 “Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.
Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma?watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?
Basi Tobia, mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbwaha, angeubomoa ukuta wao wa mawe”.
Shetani kupitia vinywa vya watumishi wake hutumia maneno ya dhihaka, kashifa na matusi ili kuwadhohofisha wana wa Mungu,
Wakati mwingine huleta shida mbalimbali ili wana wa Mungu wafadhaike, kisha wamkane Mungu wao, wamnenee mabaya⁄wamkufuru Mungu wao.
MPENDWA KATIKA YOTE TUNAYOPITI HATUPASWI KUFADHAIKA,
Kwa maana yupo wa kumtwika mizigo yetu, ZABURI 56:22 “Umtwike BWNA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele”
TUJIPE MOYO KATIKA YOTE ILI TUPATE KUSHINDA “Haya nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu, Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” YOHANA 16:33.
MUNGU akubariki sana 
By Godfrey Miyonjo.

Comments