JINA BANDIA, UMRI BANDIA, ELIMU BANDIA, KAZI BANDIA, CHEO BANDIA, SUBIRI MBINGU BANDIA.

Na Godfrey Miyonjo

BWANA YESU asifiwe sana,
Wapendwa katika Kristo Yesu, ninatambua kuwa tulio wengi tunatamani kuingia ndani ya mji ule mtakatifu (Yerusalemu mpya).

Wengi tumejizuia katika mengi, tumejifunga mikanda na kusimama kiume, tukijitahidi kwa msaada wa BWANA tusimtende Mungu dhambi, ili siku ile ikifika tusikataliwe.
Ni jambo jema, tena lakubalika kwa Mungu.
Leo nina neno moja tu ningependa kuwakumbusha wapendwa; ninyi mlio na nia ya kumpendeza YEHOVA, imeandikwa:

“Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo, na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo” UFUNUO 21:27.
Mji ule siyo mji wa waovu, siyo mji wa waongo, siyo mji wa watu wa mataifa, ni mji wa watakatifu.
Ni mji kwa ajili ya wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha Mwana-Kondoo, ili kuingia ndani yake, kila mmoja ataitwa kwa jina lake la kweli.
Wote walio na majina bandia (majina ya uongo) ninadhani watakuwa wameandikwa ndani ya kitabu cha baba wa uongo,
Baba wa uongo hana mbingu, yeye hajaandaa chochote, ameandaliwa moto, kwahiyo waongo wote ataingia nao jehanam (mbingu bandia).
WAPENDWA, HUU NDIYO WAKATI UFAAO KWETU SISI KUAMBIZANA UKWELI, UONGO UWAO WOTE NI MACHUKIZO MBELE ZA MUNGU, TUWE WAKWELI KATIKA YOTE.
“Inunue kweli wala, wala usiiuze; Naam, hekima na mafundisho, na ufahamu” MITHALI 23:23.

MUNGU akubariki .
By Godfrey Miyonjo

Comments