MAOMBI MAKALI YAKUOMBA NA KUFUNGULIWA.

Na Peter Michael Mabula
*MUNGU akukumbuke.
BWANA akutendee muujiza mkuu.
MUNGU ayakumbuke machozi yako.
Kwa jina la YESU KRISTO umeshinda.
BWANA YESU alisema kwamba kila tutakalolifunga duniani na mbinguni limefungwa Mathayo 18:18. Hivyo tunawafunga wachawi wanaokusumbua na watakimbia wenyewe.
Kwa jina la YESU KRISTO.
umeshindaaaaaaaaa kwa jina la YESU KRISTO.


 *Nakuombea Masikio yako yafunguke, kifungo cha ulimi wako kilegee uisemee haki yako. Mwili, nafsi na roho yako vifunguliwe na kila aina ya vifungo vya mawazo, maneno na matendo kwa jina na damu ya YESU KRISTO na kwa neno la MUNGU kama lilivyoandikwa katika Marko 7:34-35 '' YESU akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.''
MUNGU akubariki.



* Jiwe lililokuwa kizuizi cha kumzuia BWANA kutoka kaburini, liliondolewa na malaika.
Na leo wapo watu wengi leo mawe yamewakalia katika maisha yao, kuna mawe yamekalia biashara zao, kuna mawe yamekalia ndoa zao na kuna mawe yamekalia mchumba wako lakini kwa Kumwamini BWANA YESU aliye fufuka kutoka kwa wafu na kumpokea kama BWANA na MWOKOZI, Mawe yote yanaondoka, jiwe na litoke katika masomo yako, ndoa yako, mchumba wako, biashara yako kwa jina kuu ya la YESU KRISTO aliye hai.
Amen


* MUNGU akubariki kama IBRAHIM,akulinde kama DANIEL katika tundu la simba,akupe moyo wa uelekevu kama AYUBU,akufanye baraka kila uendako kama YUSUFU,akuokoe na baya kama NUHU wakati wa Gharika,akutangulie na kukulinda kama MUSA,akupe ushindi kwa adui kama DAUDI,akupe hekima kama SULEMANI,akupe ujasiri mbele za watu kama PETRO,akutumie katika injili kama PAULO.Zaidi ya yote MBINGUNI NI MAHALI PAZURI AMBAKO HATUTAKIWI KUKOSA UZIMA ULIO KATIKA KRISTO YESU. MUNGU akubariki sana na nakutakia usiku mwema.

* MUNGU wetu,na Baba wa BWANA wetu YESU KRISTO, tunakushukuru kwa ulinzi wako kutwa nzima ya leo. Tunakusihi Ee Bwana, wakati huu, tunapoelekea kulala, uzidi kuonekana kwetu, usituache, wala usiende mbali nasi Ee ngao yetu. Tupiganie dhidi ya adui zetu wanaolenga kutushambulia kupitia ndoto chafu, ugomvi, chuki, kutokulewana kwenye nyumba zetu!Kwa jina la Yesu Kristo.

Tupe amani na kupendana siku zote. Tujalie furaha yako Ee Baba, na shagwe itawale muda wote. Uweza wa Roho wako Mtakatifu,uwe kiongozi wetu; Kwa Jina la Yesu Kristo.

Tupe maono mapya, tupe kukupenda, tupe Roho ya kukutumikia, tupe ujasiri na uweza wa kuitambua na kuishinda dhambi. Tupe hekima ya kuzijua njia zidanganyazo na ibada za kipepo, Kwa Jina la Yesu Kristo.

Tupe ufunuo mpya juu ya kazi yako,zidi kutukumbusha kulisoma neno lako na kulitafakari daima, tupe muda wa kukuomba na kukuambudu kama upendavyo Ee Mungu wetu. Rehema zako na Neema yako, iwe juu yetu; Kwa Jina la Yesu Kristo.

Kwa wingi wa hekima yako, tujalie kadri upendavyo, kupitia Roho Mtakatifu, anayetuombea mbele zako daima tena kwa kuugua, hata zaidi tuombavyo. AMEN.



*KATAA MAGONJWA NA KILA MPANGO WA SHETANI JUU YA MAISHA YAKO KWA KUOMBA MAOMBI HAYA.

Ninaamuru kwa jina la YESU KRISTO kwamba bakteria, virusi na viumbe vyote wa magonjwa hamna uwezo juu yangu kwa jina la YESU KRISTO. Hamna mamlaka juu ya Tanzania. Ninawatiisha viumbe wote wanaoonekana na wasioonekana wasababishao magonjwa kwa jina la YESU, hamtaingia ndani ya Tanzania kwa jina la YESU KRISTO. Kwa mamlaka niliyonayo ninawafunga virusi wote wa mafua ya ndege, virusi wa mafua ya nguruwe, ebola nje ya Tanzania kwa damu ya YESU KRISTO. Kemikali zote, bakteria, protozoa wote ninawatiisha kwa damu ya YESU KRISTO. Kwa mamlaka ya damu ya mwanakondoo, viumbe wote wa magonjwa ninaupiga ule uweza uliowekwa ndani yenu juu ya Tanzania, juu ya Afrika, juu ya maisha yangu, juu ya familia yangu; ninaamuru kuanzia sasa hamtaingia ndani ya nchi ya Tanzania kwa jina la YESU KRISTO.Ninavimiliki na kuvitiisha viumbe vyote vinavyokaa kwenye anga, bahari, na nchi. Mimi ni mtawala wenu, hamna mamlaka ya kunitawala haikuwa hivyo tangu zamani. Ninawaseta mrudi kuzimu mlikotoka kwa jina la YESU KRISTO. Ninaamuru kuanzia sasa hamtanidhuru kwa damu ya YESU KRISTO. Viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekana hamna uwezo wa kunitawala kwa jina la Yesu KRISTO. Ninabeba mamlaka kama mtawala, ninawateketeza na uwezo wenu wa kudhuru kwa damu ya mwanakondoo. Nimepewa amri juu ya pepo wachafu na viumbe vyote, ninaangamiza kila nguvu iliyo juu yenu ninyi viumbe wa kishetani na kichawi na waganga wa kienyeji, ninawakausha kwa damu ya YESU KRISTO. Niwaondolea ule uwezo wa kuidhuru Tanzania kwa mamlaka ya damu ya mwanakondoo. Ninaiachilia damu ya mwanakondoo kwenye mipaka yote ya Tanzania, damu inenayo mema, ninainyunyizia kwenye mipaka yote ya Taifa la Tanzania na juu ya watu wake wote. Iwalinde dhidi ya magonjwa yote kwa jina la YESU KRISTO. Kwa mamlaka ya Jina la YESU KRISTO ninatawala viumbe vvyote vilivyomo baharini, angani na kwenye nchi kwa damu ya YESU. Ninatawala uchumi wa nchi, utajiri wa nchi; ninautawala kwa jina la YESU KRISTO. Ninatawala kwa jina la YESU KRISTO, ninatawala na kuvitiisha viumbe vyote vya magonjwa kwa jina la YESU KRISTO.
AMEN!


 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments