MBUNGE KIJANA DAVID KAFULILA AFUNGA NDOA.

David Kafulila na mkewe Jessica, wamefunga pingu za maisha leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Uvinza.
David Kafulila na mkewe Jessica, wakivalishana Pete kama ishara ya kufunga pingu za maisha leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Uvinza.


Kafulia na mkewe wakati wa ibada Kanisani.


Msimamizi wa bwana harusi  Deo Filikunjombe Kushoto,  bwana harusi Davidi Kafulila, Zito Kabwe pamoja  David Silinde, Mimi binafsi nimependa sana ushirikiano huu na umoja huu maana maana hawa ni wabunge wa vyama vitatu tofauti  lakini wameonyesha umoja mzuri.
Kafulila bungeni.
Kafulila hakika ni mfano wa kuigwa, aliandika hivi jumamosi jana.

Leo(Jumamosi) nafunga ndoa. Uvinza. Jimboni. Bestman ni Deo Filikunjombe. Lakini kwa kuwahi mjadala wa Escrow nafunga ndoa leo na kesho naanza safari kuelekea Dom kuwahi mjadala wa Escrow. Honeymoon ni baada ya Escrow."
Unaweza kuona jinsi ambavyo mtu huyu alivyoamua kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kutetea rasilimali za nchi hii. Anaamua hata kuahirisha fungate ambayo ni wakati muhimu sana kwa kumbukumbu ya ndoa yake na maisha yake kwa jumla kwa sababu ya Escrow... Maana ndoa ni maisha. 


Pia Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe nae amemtaka Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR Mageuzi, David Zacharia Kafulila, ambaye leo amefunga pingu za maisha na Bi.Jessica kuahirisha kwenda kula fungate (Honeymoon), badala yake warudi bungeni kumalizia sakata la Escrow.

Hongera sana David Kafulila.

 Zitto

Comments