IJUE THAMANI YA UTUMISHI ULIOPEWA NA YESU KRISTO KWA AJILI YA WENGINE.


Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu kwa mara nyingine tena kunipa ujumbe huu ili kuzidi kujengana na kuwakamilisha watakatifu, lengo ni kanisa lifikie cheo cha kimo cha Kristo.

Na Emmanuel Kamalamo.
Jambo la muhimu kwako kulifahamu ni hili, Mungu alikuokoa UMTUMIKIE, Na si kukaa kanisa na kupasha viti joto. Yesu alikuwa na uwezo wa kukuokoa na kukupeleka mbinguni, lakini alisema..."MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU; BALI UWALINDE NA YULE MWOVU" (Yohana 17:15)

Hivyo usipoijua thamani ya wito wa UTUMISHI wako katika wokovu na kusudi lililoko ndani ya utumishi huo utapoteza TAJI YA UZIMA uliyoandaliwa, maana utachezea wokovu.

Tuangalie Neno linalotuongoza katika somo hili. 2 Timotheo 2:19-21"Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake.
Na tena, kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu....Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki na imani, na upendo, na amani, pamojs na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi"


Msingi ni kanuni za Mungu ambazo kila anayetaka kukaa juu ya msingi huo lazima afuate kanuni hizo (muhuri) na Bwana atakujua wewe ni wake na utauacha uovu. THAMANI ya utumishi wako mbele za Mungu ni kule kujitenga na mambo ya ya dunia hii.
Kuna maneno Paulo amesema"CHOMBO KIMFUACHO BWANA" Haya maneno utayaona mstali (20) akimaanisha wewe chombo chake kwa matumizi ya kutumiwa na yeye.
Petro anatwambia.."Yeye asiye jua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu,ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bule." (2 Wakorintho 5:21)


Anglia lile neno linalosema.."NASI TUKITENDA KAZI PAMOJA NAYE" Neno hili linamaanisha Mungu anapotaka KUPONYA, KUOKOA, NK. huku duniani anatafuta mtu aliyeokoka amtumie kama chombo chake. Kama tumeokolewa kwa Neema, sikia nikwambie mpendwa hatukuitwa tuipokee NEEMA ya bule lazima tutende kazi pamoja naye bwana, ndiyo maana akatoa wengine Kuwait..MITUME, MANABII, WAINJILISTI, WACHUNGAJI NA WALIMU, Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya Huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe...oh! haleluya..haleluya Glory to God.

Usijaribu kusema.." Mimi nimeokoka nasubiri kwenda mbinguni" sawaaaa, utakwenda ndiyo, lakini TAJI ya utumishi huna na kiwango chako cha UTUKUFU kitakuwa kidogo kwa sababu hukumtumikia Bwana ulikaa kanisa kama mtoto wa ndege anayelishwa pole pole.
MAMBO MUHIMU YAKAKAYO
KUSAIDIA ILI UWE CHOMBO
KIMFAACHO BWANA.

Fuatana nami katika sehemu ya pili. Mungu akuribiki Amen.
Waweza kuomba pamoja nami kwa simu na ukaokoka sasa.
0712-660766
0758-103103.

KAMA HUJAOKOKA OKOKA LEO
BAADA YA KUFA NI HUKUMU
( Waebrania 9:27)


By Emmanuel Kamalamo.

Comments