NAPENDA KUKUTIA MOYO.



Peter Michael Mabula katika maombi.

NAPENDA KUKUTIA MOYO KWA MAANDIKO YAFUATAYO.

Natumai u mzima, pole sana kwa Mapito unayoyapitia.
-ISAYA 49:14-16 MUNGU hawezi kukusau kamwe.
-ZABURI 91:1-16 MUNGU atakuwa na wewe katika kila hali, cha
muhimu tu ni kwamba usitende dhambi tena, na kama ulitenda basi Tubu upesi
maana Yeye MUNGU ni MUNGU Mtakatifu hawezi kukaa wala kuwa ndani ya wenye
dhambi .
-1 WAKORINTHO 10:13 Katika hilo jaribu MUNGU atafanya na
mlango wa kutokea.
-UFUNUO 2:8-11 Usiogope mambo yatakayo kupata, maana Yeye
YESU yupo pamoja nawe.
-1 WATHESALONIKE 5:16-22 Mshukuru MUNGU kwa kila jambo, Omba
pamoja na kusoma Biblia bila kukoma, Jitenge na Uovu wa kila namna na Ishi
maisha Matakatifu yenye kumpendeza MUNGU, Pia katika hilo Jaribu Ruhusu kwa kadri uwezavyo Roho wa Msamaha ndani
mwako,
-Wasamehe Watu wote waliyo kukosea ‘WAEBRANIA 12:14’ 



-‘MATHAYO 18:21-22’ usiwasubirie waje kukuomba Msamaha. Vilevile acha kuwalaumu Watu
katika hili Haijalishi Wazazi na Marafiki wamekutenga na kila Mtu anakuona
haufai, wewe Mtazame YESU aliye kufa Msalabani na Kufufuka siku ya Tatu kwa ajili
Yetu sote Duniani maana YEYE Atakuwa kila KITU ndani ya Maisha yako yote kwa
sababu Binadamu wanaweza badilika ila YESU hawezi badilika YEYE ni Jana Leo na
hata Milele WAEBRANIA 13:8.
-ISAYA 41:10- Usiogope maana MUNGU yupo pamoja Nawe,
Usifadhaike maana Yeye ni MUNGU wako atakutia Nguvu na Kukusaidia.
MUNGU akubariki sana dada Tatu Abdi. Jaribu ni mtaji wa Kuongeza Imani. Kuna madhara makubwa sana yatakayo kupata
pindi tu Utakapomwacha YESU, soma MATHAYO 12:43-45 na 2 PETRO 2:20-22. Ukisoma maandiko hayo utaelewa kuwa hakuna
namna nyingine isipokuwa ni Kuomba, Kusoma Neno, Kusonga mbele na kufumilia
majaribu, kumbuka hayo Mapito ni ya mda mfupi sana na baada ya kuyashinda Imani
yako itaongezeka zaidi na Utaimarika katika Maisha ya Kiroho.
Endapo utakuwa na Maswali au Hitaji usisite kunitumia Ujumbe
kwa njia ya facebook katika Inbox yangu, nipo pamoja na wewe katika Kukuombea
uweze kushinda maana Sisi ni Washindi kwa sababu BABA Yetu ni Mshindi. Pia jaribu kutafuta Kanisa la ‘Kiroho’
linalofundisha Neno la MUNGU kwa usahihi na Ukaabudu hapo.
MUNGU akubariki sana.

Comments