NI BARAKA KUMTII YESU KRISTO NA NI LAANA KUBWA KUMTII SHETANI.


BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kulitii neno la MUNGU, Ukilitii Neno la MUNGU umemtii MUNGU.''Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.-Zaburi 119:9''
Watu Wengine Hawalitii Neno La MUNGU. Husikiliza Neno Na Kusahau. Watu Hawa Wanafananishwa Na Jengo Kubwa Lililojengwa Kwenye Mchanga, Na Upepo Ukija Huliangusha. 
 ''wala msimpe Ibilisi nafasi.-Waefeso 4:27''
Ndugu Yangu Hata kama Utapigwa Na Mawimbi Ya Maisha kiasi gani Lakini Usikubali Kumuacha BWANA YESU. Tena Litendee Kazi Neno La MUNGU Hutayumba Miaka Yote. Biblia Inakushauri Hivi " Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. - Yakobo 1:22".

 Wewe Ni Wa Muhimu Sana Kwa MUNGU, Kalvari Inathibitisha Kwamba Wewe Ni Wa Muhimu Sana Kwa MUNGU, Na MUNGU Ni Muhimu Sana Kwako. Hakika Wokovu Ulikuja Kwa Sababu Ya Upendo Usio Na Kipimo Wa MUNGU. " Si Kwamba Twatosha Sisi Wenyewe Kufikiri Neno Lolote Kwamba Ni Letu Wenyewe, Bali Utoshelevu Wetu Watoka Kwa MUNGU- 2 Kor 3:5" 
 Kwa YESU Kuna Uzima Sasa Kisha Uzima Wa Milele. 
Twende Kwa YESU Mimi Na Wewe.
Kwa YESU kuna shangwe kuu
''Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. -Mithali 28:13'' 
Ndugu yangu usifiche dhambi zako maana hazitakufikisha kwenye uzima bali kimbilia kwa BWANA YESU na umpokee na yeye atakusafisha dhambi zako zote na utakuwa huru huku jina lako likiandikwa kwenye kitabu cha uzima mbinguni.
 Kuna Shangwe Ya Milele Katika YESU KRISTO. " Ni Nani Atakayetutenga Na Upendo Wa KRISTO? Je! Ni Dhiki, Au Shida, Au Adha, Au Njaa, Au Uchi, Au Hatari, Au Upanga? Lakini Katika Mambo Hayo Yote Tunashinda, Na Zaidi Ya Kushinda, Kwa Yeye Aliyetupenda - Warumi 8:35, 37
Ndugu Zangu Ni Raha Sana Kumpa BWANA YESU Maisha Yako. Kuna Kushinda Wachawi Na Tena Kuna Zaidi Ya Kuwashinda. MUNGU anasema
''Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama.-Walawi 25:18''

Kama Unashindwa Kulala Vizuri Kwa Kuwaogopa Wachawi. Hakikisha Una Kunywa Damu Ya YESU KRISTO Ndipo Wachawi Watakukimbia. Kunywa damu ya YESU ni kufanya maombi kupitia jina lake na adui hawatakuweza siku zote.''Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.-Zaburi 20:7''

 YESU KRISTO Ametuahidi Kwamba Tukimkiri Hapa Duniani Mbele Ya Watu, Na Yeye Atatukiri Mbinguni Mbele Ya MUNGU. Ni Jambo La Ajabu Sana Hili. Kumkiri Maana Yake Ni Kumtetea Katika Matendo Na Kwa Yale Tuyasemayo. 
 ''Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya MUNGU inamkalia.-Yohana 3:36''
Je Ndugu Yangu, Unawaeleza Watu Wengine Jinsi Alivyokufanyia Wewe Hata Ukapata Wokovu? Tukimuonea Aibu YESU Kwa Kutomtetea Mbele Za Watu Maana Yake Tunamkana Na Tukimkana Maana Yake Hatufai Na Kama YESU Hatufai Sisi Maana Yake Na Sisi Hatufai Kwenye Uzima Wa Milele Maana Ni Yeye Tu Anayewapa Wanadamu Uzima Wa Milele(Yohana 14:6 Na Matendo 4:12)
Ndugu unayepitia kwenye magumu jipe moyo maana MUNGU atakushindia. maana ahadi ya MUNGU kwako ni kukushindia, Tumia Mamlaka ya BWANA YESU aliyokupa siku unampokea.

''Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.-Luka 10:19''
 Jipe Moyo Utashinda. Maadamu Unaye YESU Utashinda, Kwa Kuwa Unaye Mwamba Wa Milele Utashinda.''Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia-1 Yohana 4:4''. 
-Ndugu utamshinda shetani kama tu hutakuwa upande wake.
-Utamshinda shetani kama tu KRISTO atakuwa sehemu ya maisha yako.
-Utamshinda shetani kama tu utamtii BWANA.
-Utamshinda shetani kama tu utalitii neno la MUNGU na kuliishi.
-utamshinda shetani kama tu utakuwa upande wenye nguvu yaani upande wa BWANA YESU. 

''atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.-Yohana 3:8.
Ndugu usiishi kwa sababu tu unaishi bali ishi kwa sababu KRISTO aliye hai anaishi ndani ya maisha yako.

Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292


 

Comments