HESHIMA NA UTAJIRI VINATOKA KWA BWANA

Na Frank Philip

"Naye BWANA alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute mabaali; lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli. Kwa hiyo BWANA akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele. Ukainuliwa moyo wake katika njia za BWANA; na zaidi ya hayo akapaondoa mahali pa juu, na maashera, katika Yuda" (2 Mambo ya Nyakati 17:3-6).
Pamoja na kazi, jitihada na maarifa mbalimbali, kuna nafasi ya Mungu katika mafanikio yetu ambayo ukiitunza na kuiheshimu, siku moja utakiri kwa kinywa chako kama Daudi ukisema, "nilikuwa kijana na sasa ni mzee sijaona mwenye haki ameachwa, wala watoto wake kukosa chakula".
"Mwenye haki" tafsiri yake ni "mwenye imani", kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki. Na tunajifunza kwamba si kwa haki yetu wenyewe tunasimama ila kwa BWANA na Mungu wetu ambaye tunamtumaini na kumwamini. Kwa Huyo kuna nguvu na uweza, nasi tukimwamini na kumwishia tutaitwa watakatifu si kwa sababu ya matendo yetu tu, bali kwakuwa Yeye ni mtakatifu.
Basi kwa maneno haya, KILA alitajaye jina la BWANA na auache uovu wake akasafishwe kwa DAMU ya Yesu. Na akiisha kusafishwa ajivike vazi jeupe la MATENDO mema ambayo ni matendo ya watakatifu; kisha kudumu katika NEEMA.
Kudumu katika Neema si kuwa na magari na kufanikiwa kwa mali za dunia hii tu, na kuwa na afywa njema, bali ni PAMOJA na kukubali FUNDISHO la neema ambalo "linatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu (Tito 2:12-13). Huko ndiko kuishi katika neema!
Kwenye NEEMA lazima kuwe na MATENDO kwa maana hakuna IMANI pasipo MATENDO, na kama tunaokolewa kwa IMANI na HATUENENDI (kuwaza, kunena na kutenda) katika neno; twajidanganya bure na kujilisha upepo. Imani yetu inahesabiwa kwa mwatendo yetu, na kudumu latika fundisho la neema (Tito 2:12,13).
Frank Philip.

Comments