NURU YA UZIMA.

Na Kabalama Masatu

Bwana Yesu asifiwe mpendwa wangu katika kristo Yesu.
Karibu tujifunze habari zake Mungu kupitia jina la mwana wake,jina lenye nguvu kuliko majina yote,jina lenye kuokoa na kuponya,nalo ni jina la Yesu Kristo.

Somo la leo linaitwa NURU YA UZIMA.
NURU‬-ni mwanga ambao unaweza kumwezesha mtu kuona mahali fulani wakati wa giza.
Hapa duniani kuna mianga ya aina nyingi sana ambayo watu wengi wanaiendea/wanaitumia.
Wakati wa giza watu wengi wanatumia vyanzo vya mianga walivyonavyo;wengine wanatumia tochi ya kawaida,wengine wanatumia tochi za simu,wangine wanatumia taa za kandili(chemli),wengine umeme,solar n.k.
Vyanzo vyote hivyo hutupatia mwanga ambao unatusaidia sana na hata tunakuwa na ujasiri wa kufanya jambo au shughuli yoyote hata kama ni wakati wa usiku maana tayari tuna mwanga.
Lakini pamoja na mambo yote hayo bado iko nuru moja ambayo ukishaipata hakuna kuwaza tena kwamba mbona giza limeingia,na kuanza kusumbuka kutafuta chanzo cha mwanga.

Nuru hii ni Yesu Kristo.

Yohana8‬:12 imeandikwa:-
"Basi Yesu akawaambia tena akasema,Mimi ndimi nuru ya ulimwengu,yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,bali atakuwa na nuru ya uzima".
Umeona maandiko haya?
Maandiko yanasema wazi kwamba "mimi (Yesu) ndimi nuru ya ulimwengu".
Kumbe ipo nuru moja katika ilimwengu huu;nayo ni Yesu Kristo.
Hebu jiulize wewe katika maisha yako unatumia nuru ya namna gani?
Nataka uwaze juu ya nuru hii,#NURU YA UZIMA.
Kumbe siyo kweli kwamba unapompokea Yesu,umepokea hasara.‪‎HAPANA‬!
Ila umepokea nuru ya kukumlikia katika ulimwengu huu na kukuonyesha njia yako ya kupita ili ufike mbinguni.
Ukimpokea Kristo umepokea nuru ya kukuongoza na kufika mbinguni ukiwa salama.


Ukimpokea Kristo umepokea nuru katika maisha yako,umepata nuru katika mipango yako,umepata nuru katika uhusiano (uchumba) wako, umepata nuru katika ndoa yako,umepata nuru katika masomo yako,umepata nuru katika biashara yako.

 *Kumbukumbu la Torati30:19-20* imeandikwa:-
"Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo,kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti,baraka na laana;basi chagua uzima,ili uwe hai,wewe na uzao wako;kumpenda BWANA,Mungu wako,kuitii sauti yake,na kushikamana naye;kwani hiyo ndiyo uzima wako,na wingi wa siku zako;upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako,Ibrahimu,na Isaka,na Yakobo,kuwa atawapa".
Mimi hili jambo nalipenda sana,hapa ninaona ni jinsi gani Mungu asivyoweza kusema uongo.Kama hapa anawakumbusha Waisrael juu ya ahadi ile aliyowaapia baba zao(Ibrahimu,Isaka na Yakobo) ya kuwapa nchi waishi kwa amani kama tu watafuata maagizo yake.


Kumbe basi mpaka leo Mungu hajasahau ahadi yake kwako wewe ambaye umekubali kuitii sauti yake (Ahadi ya uzima).
Ki ukweli ni kwamba anachotarajia akione Mungu kwa mwanadamu wa leo ni maamuzi sahihi ya kumjua yeye ili apate uzima.
Katika Yohana17‬colonthree emoticon imeandikwa:-
"Na uzima wa milele ndio huu,wakujue wewe,Mungu wa pekee wa kweli,na Yesu Kristo uliyemtuma".
Hili ni jambo la kuangalia sana.
Kama andiko linaniambia ya kwamba "uzima wa milele ni kumjua Mungu wa kweli";basi vile vile tutambue ya kwamba ukimjua Mungu wa uongo basi mauti inakuhusu.
Bado nashauri kuchunguza uamuzi wetu ili tusije tukaishia kwenye mauti.
Utambue ya kwamba chanzo cha uzima siyo kuwa maarufu,siyo kuwajua waganga wengi,siyo kuwa maarufu kwa uzinzi bali ni kuitiisha nafsi yako imjue Bwana,Mungu wako aliye wa kweli yeye aliyemtuma Yesu Kristo ili wote tuokolewe kutoka kwenye dhambi.
NB‬: Hakuna kingine chenye kukuokoa wewe na mauti(laana) isipokuwa kumjua Mungu wa kweli nawe ukakubali kuitiisha nafsi yako kwa kushikamana na mwokozi wako ambaye atakuokoa na mauti isikupate.
***MWISHO****.
Mawasiliano ni:-
0753-305957;
0789-628226;
0717-624035.

Comments