SABABU TATU(3) ZA MUNGU KUTUOKOA.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze.
''Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa BWANA, au kama tukifa, twafa kwa BWANA. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya BWANA.-Warumi 14:7-8''
Wateule ni mali ya MUNGU. Kabla hatujaangalia Sababu 3 za MUNGU kutuokoa kwanza lazima tuangalie MUNGU anatuokoaje.
MUNGU anatuokoa kupitia YESU KRISTO. Hakuna njia nyingine ambayo kwayo mwanadamu yeyote anaweza kuokolewa ila ni njia ya YESU KRISTO. KRISTO ni siri ya MUNGU(Wakolosai 2:2b)
Maana yake ili umjue MUNGU wa kweli lazima kwanza umjue YESU KRISTO.  
 1 Timotheo 2 Timotheo 2:3-6 '' Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za MUNGU Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu MUNGU ni mmoja, na mpatanishi kati ya MUNGU na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu KRISTO YESU; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.    ''
Tulipokuwa dhambi tulikuwa mali yetu wenye tukiwa na ubia na shetani lakini tulipookoka tulifanyika mali ya MUNGU kupitia YESU KRISTO. Waefeso 1:5 ''  Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya YESU KRISTO, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. ''
-Hakuna mwingine yeyote anayeweza kuokoa wanadamu ila YESU KRISTO.(Matendo 4:12)
-Hakuna mwanadamu anayeweza kupata uzima wa milele nje na YESU KRISTO.(Yohana 14:6)
-Hakuna anayeweza kusamehewa dhambi zake kama sio kupitia kwa YESU.(Warumi 10:9-10)
-Hakuna msaada bila kuutaka kwa YESU KRISTO tu(Warumi 10:13)
-Hakuna mwanadamu anayeweza kujibiwa maombi yake ila tu kama anataka kujibiwa aombe kupitia jina la YESU KRISTO pekee(Yohana 14:13-14)

Hakuna mwanadamu anayeweza kuokolewa ila tu kwa kupitia YESU KRISTO.

          SABABU TATU ZA MUNGU KUTUOKOA.

 Kuna sababu 3 ambazo nimeandaa za MUNGU kutuokoa
Sio kwanza hakuna sababu ya nne na ya tano na kuondelea bali zipo sababu nyingi tu za MUNGU kutuokoa ila mimi nimekuandalia tatu. Sababu hizo ni;

        1.      MUNGU AMETUOKOA ILI TUWE WATAKATIFU:

 Waefeso 1:4  ''kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. ''
-Lazima waliookolewa na MUNGU wawe watakatifu, tulichaguliwa ili tuwe watakatifu. 
2 Petro1:4 '' Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. ''
-Lazima wateule tuwe na tabia ya uungu, tabia ya uungu ni pamoja na utakatifu.

         2. MUNGU AMETUOKOA ILI TUMTAFUTE NA KUMWONA:
Isaya 55:6-7 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa.   ''
-Tumtafute BWANA MUNGU maadamu anapatikana.
-Tukimwita kwa njia ya maombi maana yuko karibu.
-MUNGU ametuokoa ili tumtafute kwa maombi na tutamuona, tumtafute kwa matoleo tutamuona, tumtafute kwa kufunga hakika tutamuona. 
-Hatumuoni MUNGU kwa sura bali kwa matendo makuu atakayotutendea sisi baada ya kumtafuta. 
Matendo 17:27 ''7 ili wamtafute MUNGU, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.   '' .Tumtafute MUNGU na kumwona.

        3. MUNGU AMETUOKOA ILI TUWE MASHAHIDI WAKE DUNIANI.
 Matendo 1:8 '' Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.   ''
-BWANA anataka tuwe mashahidi wake Yerusalemu(Nyumabni mwetu), Uyahudi(Kazini kwetu),Samaria( Mtaani kwetu) na Mwisho wa nchi yaani dunia kote tutakakokua.
-Hakikisha mteule unakuwa shahidi wa BWANA YESU popote uliko iwe nyumbani, shuleni, kazini na kokote.
2 Kor 5:20 ''   Basi tu wajumbe kwa ajili ya KRISTO, kana kwamba MUNGU anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na MUNGU. '' 
-Wateule ni wajumbe wa KRISTO kwa mataifa.
-Tuliokolewa ili tuwe mashahidi wa MUNGU na wajumbe wake.
1 Petro 2:9 '' Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya MUNGU, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;   '' 
-Wateule wanatakiwa watangaze fadhili za MUNGU. 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments