TAMBUA MADHALA YA KUCHANJA CHALE



 Biblia Katika Kitabu Cha "Mambo ya walawi 19:28" Kimetuonyesha Madhara Ya Kuchanja Chale Nanukuu Walawi 19:28  "Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA. ."

 *Damu Ina sauti..Inaweza kunena Mema Au Mabaya{Walawi 19:26,Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.  } Ndio maana MUNGU Aka Wakataza Wana Wa Israel Wasichanje Miili Yao. 

                     MADHALA YA CHALE

 1. -->    Chale Ni Mlango Mmoja Wapo Wa shetani Kumtesa Mtu Katika Maisha Yale

 2.   -->   Utakuwa mtumwa wa mapepo muda mrefu

 3. -->   Chale inakufanya wewe kufunga maagano na mapepo..

 4.   -->  Unakuwa umeweka laana juu ya mwili wako..maana Biblia imetufundisha thamani ya miili yetu katika "1kor 3:16-17,Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la MUNGU, na ya kuwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la MUNGU, MUNGU atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la MUNGU ni takatifu, ambalo ndilo ninyi. "

5.  -->    Zinakufanya uishi maisha ya taabu,kutokuwa na amani moyoni mwako,maishani mwako hata kwenye ndoa yako.

6.   -->   Zinakuzuilia mafanikio yako maana tayari umechafua mwili wko

 7.   -->    Pia zitakukosesha uzima wa milele maana Hakuna mwabudu sanamu,mzinzi,mwasherati,wala mlevi atakae urithi ufalme wa mbinguni.
 MUOMBE MUNGU LEO AKUONDOLEE LAANA YA CHALE KATIKA MWILI WAKO LEO.
Kama hujawahi kuchanjwa chale usikubali kuchanjwa chale maana utamkosea MUNGU na kama umewahi kuchanjwa chale futa maagano yote yaliyotokana na chale, yafute kwa damu ya YESU KRISTO.
MUNGU akubariki.

Comments