SABABU YA BIBLIA KUANDIKWA KWA LUGHA YA KIEBRANIA ,KIYUNANI NA KIGIRIKI,

BWANA YESU ASIFIWE NDUGU ZANGU karibu leo tusifunze kidogo chimbuko la neno la MUNGU. MUNGU aliejuu na akubaliki unapoendelea kujifunza pamoja nami.Roho wa BWANA atusaidie, karibu.....
BIBLIA ni maktaba ya NENO LA MUNGU iliyosheeni ujumbe na mapenzi ya MUNGU kwa wanadamu hiyo ni pumzi ya ni PUMZI ya MUNGU 2Timothio 3;16-17. Biblia ina vitabu sitini na sita vilivyo­andikwa na waandishi arobaini, kwa muda usiopungua miaka elfu moja mia sita. (1600). Karibu Agano la Kale lote liliandikwa kwa lugha ya Kiebrania isipokuwa mafungu machache kwenye kitabu cha Danieli,EZRA na yerimia yaliyoandikwa kwa lugha ya Kiaramu Danieli 2:4 sehemu zilizoandikwa katika kiaramu ni hizi: Ezra 4:8 – 6:18:7:12 – 26 Danaeli 2:4 – 7:28 Yeremia 10:11 . Agano Jipya limeandikwa kwa lugha ya kiyunani na pengine Kigiriki kwa kuwa ilikuwa lugha iliyojulikana kwa karibu na watu wote ingawa katika nchi hiyo ya Israel kiaramu kilikuwa ni lugha ya nyumbani zamani za Bwana Yesu kristo.
Waandishi baadhi yao walikuwa wafalme kama Daudi na Sulemani na wengine walikuwa waganga na wataalamu kama Isaya na Luka. Wengine walimu wa dini kama Ezra na Paulo wengine maafisa wakubwa wa Serikali kama Musa, Danieli na Nehemia, wengine wakulima na mafundi Amosi na Yohana , wengine wavuvi kama Petro , wengine watunga muziki kama Asafu na watoto wa Kora wengine manabii kama Ezekiel, Yoeli na kadharika. Wengine kati ya waandishi hawakujuana kabisa, waliishi katika nchi tofauti tofauti wengine palestina (baadhi ya manabii) wengine Babeli kama Danieli na Ezekieli na wengine wakisafiri katika Nchi za mbali Paulo na Mitume wengine na mmoja wapo aliandika akiwa kifungoni katika kisiwa cha Patmo.{Yohana} Kwa kweli Biblia iliandikwa kwa njia ya pekee kuliko vitabu vingine vyote.
Kutokana na kufifia kwa lugha ya kiebrania mpaka kufikia mwaka 200 K.K na lugha hii kusahaulika na wengi na kutotumiwa na wengi ndipo ilibidi Agano la kale litafsiriwe katika lugha za mataifa mengi kama vile Kiaramu, Kisuria, Kigiriki, Kiarabu, Kimisri n.k. SEPTUAGINTI YA KIGIRIKI Mwaka 300 – 200 K.K .

Wataalamu wa Biblia hufanya kazi ya kuchunguza na kuunganisha miaka na nyakati ya wafalme wanchi mbalimbali KWA MFANO Luka 3:1 – 2 “Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake kaisari Teberio Pontio Pilato alipoalipokuwa liwali wa Uyahudi na Herode Mfalme wa Galilaya na Filipo ndugu yake Mfalme wa Itulea na nchi ya Trakoniti Lisania Mfalme wa Abilene wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa.Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria jangwani.” Hii ni kutokana kwamba kila nchi ina hesabu yake yenyewe ya miaka. Theologia hawakubaliani katika mambo yote kuhusu miaka, hivyo katika kutaja miaka tunatumia neno “Kama” kwa sababu hakuna anaejua mwaka kamili ila hufanya makisio baada ya kufanya utafiti kwa kina. Kalenda tunayotumia sasa iligunduliwa na mtaalamu mmoja mtawa anaeitwa Dionysius Exiguus. Warumi walihesabu miaka tangu kujengwa kwa Rumi. Miaka kabla ya kuzaliwa kwa Kikristo huhesabiwa kwa kurudi nyuma toka kwa Yesu Kristo kurudi nyuma na inaitwa K.K / BC na baada ya kuzaliwa kwa Yesu huhesabiwa toka kwa Yesu kwenda mbele na inajulikana kama BK/AD Agano la kale lilitafsiriwa kama lugha ya Kigiriki iliitwa Septuaginti. kwa sababu inasemekana ilitafsiriwa na watu 70. 

SABABU HIYA HAPA. MUNGU akitaka kuzungumza na watu hatumia lugha wanayoijua wenyewe hatumii lugha ngeni hutumia lugha inayofahamika kwa eneo hilo kwa waliojazwa na roho mtakatifu nathani wananielewa ukisoma Petro ameandika:...... Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2PET 1:20-21).hivyo walipata ufunuo kwa lugha rahisi waliokuwa wanaifahamu.Kiebrania kilikuwa kimeenea na kutambulika mahali pengi ndani ya Islael kipindi cha Agano la kale pia katika kipindi cha Agano jipya lugha kama kiaramu kiyunani na kigiliki ni lugha ambazo hata YESU ALIZOKUWA AKITUMIA na hata mitume wake na alivyopaa agano jipya likaandikwa LUKA 1;1-3 kwa lugha niliokunyesha hapo juu.

SIKILIZA ....MUNGU ameleta neno lake duniani kwa ajili ya uthamani wako mwanadamu anakupenda zaidi unayofikili anakuthamini zaidi ya unavyodhani harakati zote amefanya kwa ajili yako amemtuma YESU ili akukomboe aingie na neno la uzima kwako ili huishi maisha ya furaha yasiyo ya uzuni kamwe anakuomba kwa upole ndani ya moyo wako tazama niko mlangoni nabisha odi mtu akifungua mlango nitaingia kwake na kuka pamoja nae.chagua kuwa na YESU NA UMPINGE SHETANI.KARIBU KATIKA MAISHA YA WOKOVU.ONGERA YAKO UNAEENDELEA KUDUMU KATIKA IMANI.
UBARIKIWE ULIESOMA UJUMBE HUU MUNGU NA AKUHUDUMIE
SAWASAWA NA ITAJI LAKO
kwa msahada zaidi wa kiroho wasiliana nami
GODFREY MAKOKO
NO 0752508662 au
0782362588
email;g.makoko@yahoo.com au
makokogodfrey@gmail.com

Comments