CHANZO CHA FURAHA YA KUDUMU KATIKA NDOA NI HIKI.


Mimi Peter Mabula na Mke wangu Scholar siku tunafunga ndoa.
BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Leo tunaangalia kuhusu chanzo cha furaha katika ndoa.
Ndoa ni taasisi huru ambayo inatakiwa ilindwe na wanandoa wenyewe.

Waebrania 14:4-6 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu. Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, BWANA ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? ''

Kuna mambo mengi sana hufanya ili ndoa yako iwe na furaha siku zote.

-Furaha katika ndoa hutokana na wanandoa kuwa wacha MUNGU.
-Furaha katika ndoa hutokana na wanandoa wote kuwa na hofu ya MUNGU. Danieli 6: 26-27 '' .....    
maana yeye ndiye MUNGU aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho. Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani,    ...''

Siku ya Birthday ya Scholar Mabula.
-Furaha katika ndoa huja kutokana na wanandoa kuwa na mawazo ya kwenda uzima wa milele na sio jehanamu. Wafilipi 3:20 '' Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, BWANA YESU KRISTO;   ''
-Furaha katika ndoa huja baada ya wanandoa kuikabidhi ndoa yao kwa BWANA YESU ili awatawale na kuwaongoza.
-Furaha katika ndoa ni matokeo ya MUNGU kuwa sehemu ya ndoa hiyo baada ya wanandoa kumtii MUNGU tangu enzi za uchumba wao, au kumheshimu MUNGU tangu walipotubu na kurejea na kuacha dhambi za uasherati na uzinzi na kuanza na BWANA kwa kumtii na kuliishi neno lake.

Furaha katika ndoa huja baada ya kila mwanandoa kuutambua wakati, maana kuna wakati mwingine ni vizuri kujua kwamba kila jambo lina wakati wake.  Mhubiri 3:1,4,5 ''  Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;  Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;   ''   
Sio baba kumuona mama hafai kwa sababu tu mtoto amechelewa kupatikana, Sio kufukuzwa kazi kwa baba ndio kuwe chanzo cha mama kumuona baba hafai tena. Sio kufiwa na watoto au ndugu ndio iwe chanzo cha wanandoa kuwa na matatizo.

-Furaha ndani ya ndoa huja baada ya wanandoa kuwa wana maombi, maombi ni maisha na maombi ni silaha ya kummaliza adui anayewafuatilia.
Biblia inasema  ''ombeni bila kukoma;1 Thesalonike 5:17 ''  .
Ni kweli kabisa shetani anaweza akaizika ndoa yenu lakini kwa nyie kumwita BWANA YESU kupitia maombi lazima tu ndoa yenu itafufuka.
- Furaha katika ndoa huja baada ya wana ndoa wote kuwa na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.  Wagalatia 5:16 '' 
Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. ''.

Peter na Scholar., Kigamboni
ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana katika ndoa ya wacha MUNGU maana ROHO MTAKATIFU akipewa nafasi katika ndoa yeye huweka matunda yake Tisa(9) ndani ya kila mwana ndoa. hapo lazima tu ndoa hiyo iwe na furaha maana inaongozwa na MUNGU.  Wagalatia 5:22-26 ''  Lakini tunda la ROHO ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa KRISTO YESU wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa ROHO , na tuenende kwa ROHO. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana. ''

Matunda 7 ya ROHO MTAKATIFU humfanya kila mwanandoa kuwa na

-Uvumilivu katika yote.
-Upendo kwa ndoa yako.
-Uaminifu ambao ndio mtaji wa baraka na amani.
-Utu wema kiasi kwamba hawezi kumsaliti mwenzake.
-Upole kiasi kwamba huwezi kumtenda mabaya mwenzi wako wa ndoa.

Kama mkiwa na ndoa inayoongozwa na MUNGU hakika utakubaliana na mimi kwamba '' NDOA NI PARADISO YA DUNIANI'

Ndoa nyingi leo zina matatizo makubwa kwa sababu ya wana ndoa kumruhusu shetani kupanda magugu ndani ya ndoa hiyo.
Kama mama siku hizi umeanza kumchukia tu mmeo bila sababu tambua kwamba shetani hakutafuti tu wewe bali anaitafuta ndoa yako ili iwe na mgogoro mkubwa. kama baba siku hizi hata huoni kama mkeo anakulidhisha kama zamani na hadi mawazo ya kumsaliti yanakujia tambua tu kwamba shetani hakutafuti tu wewe bali anatafuka kuangamiza ndoa yako, shetani anatafuta uende jehanamu na pia anatafuta ufe na ukimwi na kuacha tatizo kubwa zaidi kwa familia yako.  Waefeso 4:27 Biblia inasema ''
wala msimpe Ibilisi nafasi. ''

-Kama wanandoa tambue kwamba hamtakiwi kumpa shetani nafasi hata dakika moja katika ndoa yenu. Kuna wakati baba anaweza kuja nyumbani amechoka  na majukumu ya kazini au amekwaruzana na wafanya kazi wenzake kazini, ni wajibu wako mama kumfariji na kumuombea  lakini wamama wengi siku hizi badala ya kuwa msaada kwa mmewe kwa kumuombea ndio kabisa baba anafika na mama anaondoka muda huo huo kwenda kufanya umbea kwa jirani.

-Mama kama mtu muhimu zaidi kwenye ndoa kuna wakati anachoka au kuumwa, sio vizuri wewe baba kumpelekesha kwa kutaka akutendee utakacho hata kama hali yake sio nzuri kwa wakati huo kuhusu jambo hilo. 2 Petro 1:5-8 ''
Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua BWANA wetu YESU KRISTO. ''

-Furaha katika ndoa huja baada ya wanandoa kutubu kuhusu yote ya nyuma waliyomkosea MUNGU. Matendo 3:19 ''
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA; ''
-Furaha katika ndoa huja baada ya kila mmoja kukaa kwenye nafasi yake kwenye ndoa.
-Furaha katika ndoa huja baada ya kila mwanandoa kuwa na hofu ya MUNGU.
-Furaha katika ndoa huja baada ya wanandoa kuwa wavumilivu, wewe mama sio kila baba akikukwaza tu kidogo unabeba vyombo na kwenda kwenu, je wazazi wako wangekuwa na tabia hizo nadhana hata  kuzaliwa tu wewe usingezaliwa.

Ni vizuri wana ndoa wakafuata kanuni ya Biblia kuhusu ndoa
Nina mengi sasa ila kwa leo inatosha lakini muhimu zaidi kwa ndoa ili iwe na furaha ni kumruhusu BWANA YESU akawa sehemu ya ndoa yenu, kuwa wana maombi na kuliishi neno la MUNGU huku mkiwa na hofu ya MUNGU.


Warumi 12:1,9-21 ''  Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya MUNGU yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia BWANA; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili. Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya MUNGU; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena BWANA. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. ''
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments