HUJAOKOLEWA ILI UNYAMAZE

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze ujumbe mzuri wa kutufanya tulitimize kusudi la MUNGU.
Yeremia 48:13a '' Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; ''
-Ndugu mpendwa, unadhani ni nani anayeambiwa hivyo?
 
-Tunatakiwa tuishi katika matendo mema ambayo MUNGU tangu zamani aliyaumba ili tuenende katika hayo.
-Kusudi la kwanza la MUNGU kukuokoa ni ili usiende jehanamu kama ukivumilia mpaka mwisho wa maisha yako hapa duniani.
-Kusudi la pili la MUNGU kukuokoa ni ili uwe shahidi wake au wakili wake.

Waefeso 2:8-10 ''Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo.''

 Biblia inasema kwamba mtu ukikaa kwenye kusudi la MUNGU  unampendeza sana MUNGU na MUNGU wakati huo anaanza kuifanya kazi yake ya kuwaokoa na kuwasaidia  wanadamu kupitia wewe. Biblia inasema
 ''Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano-Wafilipi 2:13-14''
-Kumbe ukiifanya kazi ya MUNGU ni MUNGU anakuwa anafanya kazi yake kupitia wewe ili kulitimiza kusudi lake jema. wewe ni wa muhimu sana ila unatakiwa tu kujitambua na kubaki kwenye nafasi ambayo MUNGU amekuweka

1 Kor 4:1 '' Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU''.

MUNGU angeweza hata kuwatuma malaika ambao ni mawakili wazuri wa MUNGU lakini kwa upendo mwingi sana BWANA amekuchagua wewe ili dunia nzima wamgeukie MUNGU aliye hai kwa ajili ya uzima wao.

Kazi ya wakili ni kusema jambo kwa niaba ya yule ambaye alitakiwa aseme mwenyewe.

Ndugu mteule,Hatujaokolewa Ili Tunyamaze Kimya Bali BWANA YESU Ametuokoa Ili Tutangaze Wokovu Wake
Matendo 1:8 '' Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.   ''
 -Hatutakiwi Kujitangaza Sisi Au Kutangaza Makanisa Yetu Bali MUNGU Anataka Kutangaze Injili Yake. 
-Hatutakiwi Kuwahukumu Watu Bali Kuwaambia Watu Ukweli Ambao Upo Na Utakuja Kwamba Baada Ya Kifo Ni Hukumu
Waebrania 9:27 '' Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; ''
Hukumu Hiyo Itafanyika Kulingana Na Matendo Ya Mtu Ya Sasa,  BWANA YESU siku hiyo atamlipa kila mwanadamu sawasawa  na matendo yake.
Ufunuo 22:12 '' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. ''
 
Ndio Maana Sasa Tunawaonya Wanadamu.
 Biblia Inatuagiza Kuonya, Kukaripia Na Kuonya 
1 Timotheo 4:13-16  '' Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha. Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee. Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia. ''. 
Pia Neno Ni Upanga Ambao Hukata Kote Kuwili Hivyo Hata Sisi Tujidhadhari Na Dunia Maana Biblia Inasema Kila Alitajaye Jina La BWANA YESU Na Aache Uovu
2 Timotheo 2:19 '' Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu. ''
Tahadhari Ni Kwa Wanadamu Wote Ila Injili Itahubiriwa Kote Na Hakutakuwa Na Mwenye Kutoa Udhuri Siku Ile. 

Ndugu, Shiriki Upendo Wa MUNGU Wa Uzima
Yohana 3:16-18 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.   ''  

BWANA YESU Yuaja Na Atachukua Watakatifu Tu Waliomtii. 

YESU KRISTO ANAOKOA, UKIMWAMINI LEO UNAOKOKA. Kataa Dhambi, Ogopa Dhambi, Ikimbie Dhambi Na Usifanye Dhambi. Dhambi Inaua Ila YESU Anaponya.
Mfuate BWANA YESU ili akufanye mvuvi wa watu. MUNGU anataka awaokoe wanadamu kupitia wewe.

Mathayo 4:19-20 '' Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. ''
Ndugu usinyamaze kama kweli umeokoka.
Usinyamaze wala kusitasita bali hubiri injili ya BWANA YESU.

 Kila Aliyeokoka Ana Wajibu Wa Kuliishi Neno Hili La MUNGU Kulikiri Kwa Uhalisia Wake Katika Maisha Yake. 
Neno Hilo Ni "Nimesulubiwa Pamoja Na KRISTO; Lakini Ni Hai; Wala Si Mimi Tena, Bali KRISTO Yu Hai Ndani Yangu; Na Uhai Nilio Nao Sasa Katika Mwili, Ninao Katika Imani Ya Mwana Wa MUNGU Ambaye Alinipenda Akajitoa Nafsi Yake Kwa Ajili Yangu-Wagalatia 2:20".  
-Ndugu Yangu, Inatakiwa Uusulubishe Mwili Wako Ili Usitende Dhambi. 
-Inatakiwi Usiishi Tu Kwa Sababu Unaishi, Bali Ishi Kwa KRISTO Anaishi Ndani Yako. 
-Enenda Kwa Imani. 
Tambua Kwamba BWANA YESU Alijitoa Kwa Kifo Cha Aibu Pale Msalabani Ili Tu Wewe Na Mimi Tushinde. 
MUNGU Anatutaka Tuishi Maisha Ya Ushindi Dhidi Ya Dhambi.
Warumi 12:2 ''Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya MUNGU yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.   ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili. MUNGU Akubariki.

Comments