JINSI MTU ACHUKULIWAVYO MSUKULE-Na: ADRIANO MAKAZI (RP)



RP  Adriano akihubiri katika ibada  Bonde la Maono  Morogoro. 
 
Utangulizi: Somo letu  leo linaitwa Jinsi Mtu Achukuliwavyo Msukule”. Huwezi kulikuta neno ‘msukule’ katika Biblia, na hii imewafanya watu wengi wanavyolikosa katika Biblia wasikubaliane na mafundisho hayo wakidhani  ni imani potofu. Hata hivyo kutokuwepo kwa neno hili katika Biblia hakumfanyi shetani asiwachukue watu katika msukule.  Biblia hata hivyo inatukumbusha kwamba yapo mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya lakini katika Biblia hayapo kwani hayakuandikwa.
YOHANA 21:25….[Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.]….Kumbe ni mengi  sana yale ambayo hayajaandikwa katika Biblia, ikiwemo mambo ya “msukule”. YOHANA 20:30….[Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki.]…. Maana yake ni kuwa, yapo mengine ambayo hayajaandikwa, lakini haimaanishi kuwa kutoandikwa hayawezi kutuathiri leo  hii. Mathalani, hata kama Yesu aliwaweka huru misukule, na haijaandikwa katika Biblia, si kigezo cha kubisha na kusema misukule haipo.
Maneno kama vile upako, nayo hayapo katika Biblia, ila ni neno linalotaokana na ‘mpakwa mafuta’. Wamiminiwa mafuta katika Biblia ni kama vile Wafalme na Manabii,  vyombo  vya Bwana kwa ajili ya matumizi ya Bwana.
1WAFALME 19:15-16 … [Bwana akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu. 16 Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa AbelMehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.]….

Mtu aweza kuchukuliwa msukule  mzima mzima,au kwa kuchukuliwa mikonoyake,au  miguu yake,  au macho n.k.   mikono kama imechukuliwa huwezikufanikiwa,kwani  Mungu  amesema atabariki kazi zamikono  yako.  Endapo wachawi wamekuwekea mikono yap aka,si  rahisi  ubarikiwe kwani mikono hiyo si yako.
Kichwa endapo  kimeibiwa,  na pengine mtu huyo kawekewa kichwa cha paka au cha kuku, si  rahisi kusonga mbele kwa mafanikio.  Leo lazima turudishe kichwa chako kwa Jina la Yesu.
Mwingine anakuwa amewekewa tumbo la bandia,   matokeo  yake tumbo la aina hiyo lililopaswalizae marais,  au  mawaziri linashindwa kuzaa. Kila mara uvimbe unatokea tumboni.leo ni siku ya kuamuru matumbo  yote yaliyochukuliwa yarudi kwa Jina la  Yesu.

UKIRI
Kila mchawi anayetumia tumbo,  miguu,mikono,  kichwa changu, nawaponda wachawi,kwa kuwa imeandikwa usimuache mwanamke mchawi kwa Jina la Yesu, nawaponda wachawi owte,kwa kuwaimeandikwa mimimni rungu  la Bwana na silaha za Bwana za  vita. Leo navua uso bandia, navua tumbo bandia kwa Jina la Yesu. Amen
 

Majeshi ya Bwana ndani  ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima, Bonde la Maono Morogoro,
wakati wa Ibada ya Jumapili  iliyoongozwa na RP Adriano. 
Mtu anaweza kuwekewa sura bandia.  Katika mashindano ya Miss Tanzania au Miss University,  unaweza kushangaa kuwa anayechaguliwa kama mshindi wala si Yule aliyetarajiwa, na wala hafananii kupata nafasi  kama hiyo.
AINA ZA MISUKULE
Msukule  ni mtu aliyekufa au aliyechomolewa ndani ya mwili wake na kwenda kutunzwa mahali pengine bila ridhaa yake. Lipo  shimo kubwa sana la kuzimu ambalo ndiko makao makuu kwa shetani. Wachawi nao wametengeneza mashimo  yao madogomadogo  ya kuhifadhia watu humo ndani. Mashimo kama vile  ‘gambushi’ ni mfano mmojawapo.
Zipo biashara za miili  ya watu. UFUNUO 18:11-2…[ 11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; 12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; 13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.]… Baada ya malikia wa mbingu kupigwa, wafanyabiashara wa nchi walilia na  kumuombolezea. Miili na Roho za wanadamu ni miongoni mwa bidhaa hizi zilizokosa wateja. Katika Biblia,wana wa Yakobo walimuuza ndugu yao kwa Waishmaeli, naye akapelekwa hadi kwa nyumba ya  Potifa.  MWAZO 37:27…[ 27 Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. 28 Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri.]…. Waishmaeli ni Waarabu, na baada ya kumnunua Yusufu walienda  na kumuuza tena. Tama ya mali inaweza kumfanya mtu kumuuza mwingine.  Yesu naye aliuzwa na mwanafunzi wake, Yuda Iskariote.
MWANZO 39:1…[Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko.]… Inawezekana hata wewe hapo ulipo ulishauzwa na hauna habari. Wanachosubiri ni ule mtego wao wa kugonngwa na bodaoda, ili mwishowe madktanri waseme kwa ajali hii damu imevunja sana huwezi kupona. Endapo  mtu hana Yesu, atakuwa na shetani wake anayemtegemea. Si vyema kkutamani vitu au aina ya maisha ya mtu fulanii kwa sababu kwa kufanya hivyo utamtamani ha  ta Yule  aliyempa. Ni kweli kuwa shetani anaweza kumpatia mtu vitu, fedha, utajiri, na ndiyo maana shetani katika kumjaribu Yesu, alimwambia ‘endapo utanisujudia nitakupa vitu vyote hivi kwa sababu vipo mikononi mwangu’.
UKIRI

Bwana Yesu, Ninaomba leo unipe neema ya kutoka kwa Jina la Yesu. Ninakataa kukaa utumwani, ninakataa kuonewa mimi kwa Jina la  Yesu, Ninaamuru  leo  mikono yangu kama imeibiwa na inatumiak  na mtu yeyote namnyang’anya leo kwa Jina la Yesu. leo  macho yangu kama yameibiwa na inatumika  na mtu yeyote namnyang’anya leo kwa Jina la Yesu. Amen
 

SOMO HILI LITAENDELEA JUMAPILI IJAYO YA TAREHE 29/03/2015. USIKOSE KUFUATILIA MWENDELEZO HUU:-
 
                          © Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)

Mtaa wa Nguvu Kazi, (Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.

 /or

Contact our Senior Pastor:

 Dr. Godson Issa Zacharia

 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

Comments