MADHARA YA MAHAKAMA YA KADHI TANZANIA.

Mtume Peter Rashid Abubakar enzi hizo akiwa shehe.
Mtumishi wa MUNGU Mtume Peter Rashid Abubakar anafafanua kila kitu kuhusu hatari na madhara ya makama ya kadhi.
Fuatana nae ndio utajua kwanini mahakama hii haihitajiki Tanzania.

Mtume Peter Rashid Abubakar anafafanua MAANA YA NENO 'KADHI'.
Neno Kadhi limetokana na neno la Kiarabu Al-Qadhi maana yake hii;
AL-SULTWAN-Yaani mtawala na Al-Hakim yaani Hakimu.
'Ukadhi ni kufafanua hukumu za Sharia na kuzitekeleza. Pia Neno Kadhi linafafanuliwa ifuatavyo:
1. Kadhi ni hakimu wa kiislamu mwenye madaraka ya kuanua daawa za sheria.
2. Hakimu; Mwamuzi; Jaji(Neno daawa linamaana ya; 1. Mashitaka yaliyofikishwa mahakamani ili kutolewa hukumu ;kesi; 2. Mambo yanayoleta ugomvi au kutosikilizana; utesi)JINSI SHARIA'H ZILIVYOANDIKWA NA KUFAFANULIWA NA ULAMAA WANNE(4).
kunako mwaka Kama 200 hadi 300 hivi- baada ya Hijra(Hijra ni tendo la mtume Muhammad kuhama toka Makka kwenda Madina Kama mwaka wa 622 BK) walitokea Ulamaa wanne ambao kwa kutumia IJIHAD YAANI HEKIMA YA UPEMBUZI Walitoa tafsiri za Shari'ah ambazo ndizo zinazokubalika na leo. Kwa maana hiyo kuanzia miaka 1.100 iliyopita hapajatokea ruhsa ya kutoa tafsiri ya Shari'ah iliyotofauti na tafsiri za Ulamaa hao 4. Isipokuwa Waislamu wa madhehebu ya Shia wao wanao utaratibu wao wa Fiqh. Ulamaa hao 4 ndio chanzo cha madhehebu makuu hayo manne ya Kiislamu.


 Hebu nifafanue madhara ya mahakama ya Kadhi ni Kama ifuatavyo: Neno adhabu kwa kiarabu linaitwa Huudud; Sharia zinazoambatana na makosa ya Adhabu yaani Al-Huduud ni zile zenye makosa ya aina 8 ambayo ni;
1. Kuacha dini ya Kiislamu na unyang'anyi adhabu yake ni KIFO.
2.Zinaa;Ulevi; na kumsingizia mtu kuwa amezini adhabu yake ni VIBOKO.
3.Wizi adhabu yake ni KUKATWA MKONO ULOIBA.
4. Uasherati adhabu yake ni Kupigwa kwa mawe hadi Kifo.
5.Adhabu ya mauaji ni kulipa Kisasi (Qisas) Kifo kwa Kifo au jino kwa jino.
6. Kila mtu mwezi mtukufu wa Ramadhani wote kufunga uwe mpagani au mkristo.
7. Kuhakikisha kila mtu aingiapo chooni aanze na mguu wa kushoto na wakati wa kutoka atoke na mguu wa kulia
8. Ni kuhakikisha wanaume wote wapagani kwa wakristo ambao hawajatahiriwa (Magovi yao) lazima watahiriwe.
Makadhi wa Kiislamu pia watatuzuia wakristo Kujenga makanisa. Wakristo hawataruhusiwa kurefusha nyumba zao zaidi ya nyumba za waislam. Pia watapiga marufuku uuzaji wa nguruwe na kula nguruwe(Akina Masawe) n.k. Yapo mengi saana hayo ni kwa ufupi tu. NDIO MAANA TUNAIPINGA MAHAKAMA YA KADHI KUINGIZWA KWENYE KATIBA YA NCHI YETU TANZANIA. Kama upo nami to a hoja zako.



Katika moja ya huduma za Mtume Peter Rashid Abubakar
Mtume Peter Rashid Abubakar anafafanua kuhusu na Ulamaa 4 (Shari'ah) ndio chanzo cha madhehebu makuu hayo manne ya Kiislamu.
1. FIQH(SHARI'AH) YA HANAFI.
Hii imekusanywa na Abu Hanifa Bin Nu'man Bin Thabit. Mtu huyo alizaliwa mwaka 80 baada ya Hijra (s.a.w.a na mwaka wa 699 A.D) Naye alikufa mwaka 150 wa Al-Hijra(s.a.w.a na mwaka wa 767 A.D). Hadi mwaka 1995 madhehebu ya Hanafi yalikuwa na wafuasi 340 milioni duniani. Wafuasi wa madhehebu hayo wapo ktk nchi za Uturuki;Pakistan;Jordan;Indonesia;China na Urusi.
2. FIQH(SHARI'AH) YA MALIK.
Hii inatokana na Malik Bin Anas Asbahi. Mtu huyo aluzaliwa mwaka 93 wa Al-Hijra(s.a.w na mwaka wa 714 A.D.) Naye alikufa mwaka 179 wa Al-Hijra (s.a.w na mwaka wa 798 A.D). Hadi mwaka 1995 madhehebu haya yalikuwa na wafuasi wapatao 45 milioni duniani. Wengi wa wafuasi wapo ktk nchi za Morocco; Algeria;Tunisia ; Sudan;Kuwait na Bahrein.
3.FIQH(SHARI'AH) YA SHAFI'I.
Hiii ilianzishwa na Muhammad Bin Idris Al-Shafi'i. Mtu huyo alizaliwa mwaka 150 wa Al-Hijra(s.a.w na mwaka wa 767 A.D.) na akafa mwaka wa 240 Al-Hajra(s.w.a na mwaka wa 854 A.D.) Madhehebu haya hadi mwaka 1995 yalikuwa na wafuasi wapatao 100 milioni duniani. Wengi wa wafuasi wapo ktk nchi za Palestina; Lebanon; Misri;Iraq;Saudi Arabia yaani Hijaz; Yemen na Indonesia.
4. FIQH(SHARI'AH) YA HANBAL.
Hii ikianzishwa na Ahmad Bin Hanbal. Mtu huyu alizaliwa mwaka wa 164 Al-Hajra (s.a.w na mwaka wa 780 A.D ) na alikufa mwaka wa 241 Al-Hajra (s a.w mwaka wa 855 A.D.) Hadi kufikia mwaka 1995 madhehebu haya yalikuwa na wafuasi wapatao milioni tatu duniani. Wengi wa wafuasi hao wapo ktk nchi za Saudis Arabia yaani Hijaz; Lebanon na Syria. 


Mtume Peter Abubakar baada ya Wokovu Wa BWANA YESU, Hapa akihubiri na kuombea huko Bujumbura Burundi.

Comments