MATOKEO YA YA NGUVU YA NENO ANALO TAMKA MTU WA ROHONI. (SEHEMU II)

Na Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu asifiwe!
Hii ni sehemu ya pili ya somo hili, ukitaka kujua tulikotoka ni muhimu utafute tulikoanzia ndipo utaweza kuelewa zaidi.
Au unaweza kwenda kwenye page yangu iitwayo,,(UWATAKASE KWA ILE KWELI; NENO LAKO NDIYO KWELI.Yohana 17:17)Z

Katika ukurasa huo utalipata somo hili na utajifunza zaidi. Lengo lakutoa masomo haya ni kutaka kujenga zaidi.." KANISA" (mwili wa Kristo) , naposema Kanisa namaanisha mtu binafsi aliyeokoka ambaye anapaswa kupata mafundisho akiwa kama kiungo cha mwili wa Kristo.
UNA LITUMIAJE HILO
NENO NA WAPI.

Neno la Mungu linatoa matokeo yanayojidhihirisha katika ulimwengu wa "MWILI" linapo tamkwa na mtu wa "ROHONI" (aliyeokoka) Na si kila mtu anaweza kulitumia "NENO LA MUNGU" katika madhingira yoyote mpaka awe mtu wa "ROHONI".
Unaweza kuuliza, "inakuwaje Emmanuel mpaka aliyeokoka?" Nisikilize, Swala la "NENO LA MUNGU" si swala la kimwili bali ni swala la kiroho. Ukisoma Warumi 10:17 anasema hivi,"Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo"
"IMANI" ni jambo la rohoni, ndiyo maana anasema,,"LAKINI PASIPO IMANI HAIWEZEKANI KUMPENDEZA MUNGU; KWA MAANA MTU AMWENDEAYE MUNGU LAZIMA AAMINI KWAMBA YEYE YUKO, NA KWAMBA UWAPA THAWABU WALE WAMTAFUTAO" (Waebrania 11:6)
Kwa mantiki hiyo,ukiunganisha mistari hiyo miwili unatafuta kujua kwamba, ili umuone Mungu lazima uingie kwenye "IMANI" na imani inaletwa ndani yako kwa Neno, na hilo Neno utalitumia ukiwa "ROHONI" na si "MWILINI" ukijaribu kutumia Neno la Mungu na hauko katika Imani ya Neno hilo uwe na huakika halileti majibu.
CHANZO CHA NENO NI
NINI?

Yohana 1:1 "Hapo mwanzo kulikuwako Neno,naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Soma na Yohana 4:24 "Mungu ni Roho,nao wamwabuduo imweawapasa kumwabudu katika roho na kweli" Hivyo utaona "NENO" ni Mungu,na Mungu ni "ROHO" kwa hiyo Neno ni asili ya Roho. Yesu alisema,,ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA,MWILI HAUFAI KITU; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, TENA NI UZIMA" (Yohana 6:63)
Kama Neno la Mungu ni Roho lazima na wewe uingie rohoni, ndiyo maana anasema,,"...NAO WAMWABUDUO IMEWAPASA KUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI" na hapo lazima uwe katika ulimwengu wa Roho umekitishwa pamoja na Kristo Yesu.,Bwana Yesu asifiweee!!
CHANZO CHA MTU WA
ROHONI.

Mtu wa "ROHONI" ni yule aliyetolewa katika hari ya "KIFO CHA KIROHO" Na mtu huyo anapewa maisha mapya katika ulimwengu wa Roho.
Waefeso 2:1,5-6 "Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu...hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani mmeokolewa kwa neema. Akatufufu pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho,katika Kristo Yesu"
Kwa hiyo angalia madhinga ya chanzo cha Neno kiliko na ulinganishe na chanzo cha mtu wa "ROHONI" mahari aliko, utaona lazima wawe eneo moja la "ULIMWENGU WA ROHO"

Kama unasema wewe na "MTU WA ROHONI" hakikisha uwe na uhakika umeketi pamoja na Kristo katika ulimwengu wa Roho, kama hujaketi itakuwa vigumu kulitumia "NENO LA MUNGU" na likawa na "NGUVU MAENEO ANAPOTAKA LIFANYE KAZI" katika madhingira ya unayoishi kwa sababu hauko katika "ROHO" yaani hujaketishwa pamoja na Kristo. Kawaulize wana wa Skewa Kuhani Mkuu,wao si wa "ULIMWENGU WA ROHO" (hawajaokoka/kuketishwa) wakajaribu kuingia katika vita ya kukemea pepo, biblia inasema yule pepo alisema,,"YESU NAMJUA NA PAULO NA MFAHAMU,LAKINI NINYI NI NANI" maandiko yanasema walipigwa na kuvuliwa nguo.
Kwa hiyo si kila mtu anaweza kutumia Neno katika vita ya ulimwengu wa roho kama yeye hajulikani ulimwengu wa roho, maana ulimwengu tunatambulika. Ufalme wa giza unatujua kabisa tuna mamlaka hivyo tukitamka "NENO LA MUNGU" wanajua mwana wa mfalme katamka Neno wanakimbia..
Nikupe hushuhuda huu utaelewa nini nasema juu ya "NGUVU YA NENO ANALOTAMKA MTU WA ROHONI"

Mara nyingi nafany huduma za maombozi kwa njia ya simu na Mungu amekuwa akiwafungu watu. Niliomba na dada mmoja amefungwa na wachawi kwenye jeneza na yuko makaburi makaburini, nilipoliitia JINA LA BWANA anasema aliona mtu mweupe anamtoa kwenye Jeneza na wale waliomfunga walikimbia. Nini maana yake, maana yake hii, Mimi nilikuwa ulimwengu wa ROHO nilipotamka lile Neno lilifanya kazi kwa sababu ni mwana wa Mfalme najulikana katika "ULIMWENGU WA ROHO"...ooh! Glory to God. Hakikisha umeokoka sawasawa na umeketishwa ili uwe nguvu ya kulitamka Neno na likatenda kazi.
EZEKIELI ALIPOIONA
MIFUPA MIKAVU ALIKUWA WAPI?

fuatana nami.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA,BAADA YAKUFA NI HUKUMU (Waebrania 9:27)
MUNGU AKUBARIKI.
ekamalamo@gmail.com

Comments