SOMO: NJIA - Na: BRYSON LEMA (RP)


RP Bryson,  ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro -

Utangulizi: Somo letu leo linaitwa NJIA”. Unapotaka kwenda mahali popote, sharti uijue njia. Kila iitwapo leo, mwanadamu  anakuwa amepiga hatua fulani ya njia ya safari  ya maisha yake,  na kuna mahali huyu mtu anaelekea, aidha uzimani au motoni. Zipo pia safari ambazo njia zipo lakini  usafiri haupo. Kilichowafanya wana wa Israeli waliotoka  Misri wasifike Kanaani, nchi ya Ahadi ni  njia. Ni kwa sababu njia waliyopitia ilikuwa na changamoto nyingi, na majaribu mengi. Njia ndiyo yenye uhakika wa kukufikisha unakokwenda.  Kwenye njia ndipo shetani alipoweka makao, na kuwakamata watu na kuwafanya wajisahau.
Children Ministry wakiimba na kucheza mbele za Bwana katia ibada ya Jumapili 29//2015
Nyumba ya  Ufufuo na Uzima Morogoro (Bonde la Maono)

AYUBU 38:18-20…[Umeyafahamu mapana ya dunia?  Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.  19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru?  Na giza pia, mahali pake ni wapi? 20 Upate kuipeleka hata mpaka wake,  Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake?]… Ukielewa hiyo njia inakufanya ujue unapaswa kufanya nini kwa wakati gani.  Zipo njia mbili,kwa mujibu  wa Ayubu,moja ya nuru na ingine ya giza. Shetani yupo kwa ajili ya kupinga na kuzuia. Yapomakao yako ambayo  Mungu alikuandalia uwepo pale. Jinsi ya kwenda kwenye hayo makao, inakupasa uijue hiyo njia.
Usiogope vita kwa sababu hata Samweli  alizaliwa kutokana na Penina kumsumbua Hanna. Vita inapoinuka kazini kwako, kwenye nyumba ya kupanga n.k. ni sababu ya kukupeleka wewe kwenye hatima njema zaidi. Imeandikwa kuwa, ‘Mungu wetu ni mtu wa vita, Bwana ni Jina lake’.
 
Umati wa  Watu  waliofurika katika Bonde la Maono Morogoro Jumapili
HESABU 24:21 …[Kisha akamwangalia Mkeni, akatunga mithali yake, akasema, Makao yako yana nguvu, Na kitundu chako kimewekwa katika jabali.]… Wao wanaweka mitego ili wakuzuie na kukuonea, lakini Yesu Krsito ameshakuwekea njia katikati  ya jabali. Ndiyo maana Yesu alisema katika YOHANA 14:6… [“mimi ndimi njia, kweli na uzima”]… Katika dunia yote tokea uumbaji, hayupo nabii aliyewahi kutamka maneno kama haya ya Yesu. Eliya pamoja na kushusha moto, hakuwahi kusema ni njia. Elisha pamoja na kufufua wafu, hakuwahi kusema ni njia. Musa pamoja na kutenda miujiza yote, hakuwahi kusema ni njia. YESU KRISTO ndiye pekee ambaye ni NJIA. Yupo adui anayezuia njia yako, katika ndoa yako, kazi yako n.k. lakini hakuna atakayeweza kukuzuia.
Huwezi kumzuia mtu aliyetumwa. Kama kweli unaweza, kampigie simu Musa kumuuliza je, waliokuzuia walifanikiwa? La sivyo mpigie simu Farao, je ulipowazuia Israeli, ulifanikiwa? Waliinuka mitume na manabii na wachungaji wengi, lakini  hayupo wa kufananishwa na Yesu Kristo.
 
RP Bryson akiombeawatu  waliamua kuma Yesu Kristo maisha yao kwa Kuokoka,
Jumapili 29/3/2015 katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro.
Yusufu aliuzwa na ndugu zake,  wakidhani wamempoteza, kumbe wamempeleka kwenye eneo la  kumiliki kwake. Endapo ndugu zake hawa wasingemuuza Yusufu, asingetawala. Leo hii tunalitaja jina la  Yusufu kwa sababu ya hao ndugu zake kumuuza. Kile kikao wanachokaa maadui zako, Mungu yupokaatikati yao na najua mpango wao. Mungu anaweza kusababisha uondoke, lakini ukirudi unarudi kwa nguvu mpya na mamlaka mapya. Wasikutishe wale wanoinuka. Ukiona wanga au wachawi wanakuwangia usiku, yapasa ujisifu sana, kwa sababu umeweza kuwafanya watu wasilale usiku huo kwa ajili yako tu.  Ukiona unatengenezewa zengwe kazini kwako, maana yake wewe ni mtu  wa hatari sana, na unapaswa kupandishwa cheo. Ni ushahidi kuwa ndani yako ipo nguvu inayowatisha
Showers of Glory wakati wakiimba na kumsifu Bwana Yesu Jumapili 29/3/2015
Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro. 


MITHALI 24:15….[Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki;  Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;]… Yupo aliyegusa makao yangu, lazima leo nimshughulikie.

ZABURI 55:15…[Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali hai, Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.]…. Wote wanaokuzia kwenye mipango yako, ni saa ya kuwaondoa kwa Jina la Yesu.

                          © Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)

Mtaa wa Nguvu Kazi, (Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.

 /or

Contact our Senior Pastor:

 Dr. Godson Issa Zacharia

 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

Comments