ABEL SULEIMAN:KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?

Na Abel Suleiman Shiriwa

UTANGULIZI:
Hii ni sehemu ya ushuhuda wangu, ambao nitaeleza ni sababu gani ambayo ilipelekea niachane na uislamu, na hatimae kuwa Mkristo, Katika DVD ya ushuhuda wangu, nilieleza kwa kifupi, na mengi sikuyasema, nilieze hasa harakati zangu katiks mihadhara, ila hapa nitachumbua mengi zaidi.
Nimezaliwa miaka 27 Iliyopita, katika JIJI LA MWANZA (Rock city) Jina langu ambalo nilikuwa nalitumia katika uislamu, ni Aboubakar, nimesoma Madrasa Pale THAQAAFATUL ISLAMIYA, Mwanza, karibu na Shule ya msingi Mirongo, shule hiyo imepakana na Lake Secondary School, pia na Ipo karibu na hospitali ya Seketule.
Miongoni mwa walimu wangu wa madrasa, ni:

Ramadhani Maganga
Ustadh Kikatani
Ustadh Hassan Lolo.
Ustadh Kaisy
Ustadh Shekue.

Pia nilisoma Madrasa iliyopo TAQWA, maeneo ya Ghana, chini ya Sheikh Abdallah Panya, pia Ghana mtaa wa kifua Wazi, kwa Ustadh, Thuqmal bin Hussein (Huyu ni ustadh aliyekuwa ana diri na Elimu za dua za kafara, kuchinja mbuzi, kuku na kisha kutuchukya kwenda kufanya zindiko ndani ya nyumba, kwa kutumia vitabu mbali mbali vya kiislamu) Nitaeleza habari zake katika mwendelezo wa ushuhuda wangu....
Katika harakati zangu ambazo nilizifanya katika uislamu, ni ushiriki wa harakati za ujenzi wa Misikiti VIJIJINI, michango ya ujenzi huo ulikuwa ukifanyika ndani ya msikiti wa IJUMAA Mwanza, ambapo michango hiyo, ilikuwa ikifanyika siku ya ijumaa, na J'Mosi au J'pili tunakutanika na kuelekea vijijini, miongoni mwa vijiji hivyo, ni MSIKITI Uliopo Kigongo Fery, (Kwenye Kivuko cha Fery kwa waendaji wa Sengerema, Geita na Bukoba) Unaanza Usagara, pia Misungwi, tulikuwa napo tukifanya ujenzi wa misikiti pia, kubwa zaidi ni Msikiti wa MISASI, huo ni mmoja wa misikiti mkubwa ambao tulichukua muda kuujenga, Mwangalizi wake anajulikana kwa jina la OSAMA kwa Wakazi wa Misasi wanaufahamu, upo nyuma ya Center ya MISASI,
2011 Abel akiwa katika mhadhara Nairobi


Kuna baadhi ya Waarabu ambao walikuwa wakitoa magari yao aina ya FUSO, kwa ajili ya kutubeba, na kutupeleka huko, na pia baadhi ya vijana, tulikuwa tunapatiwa kiasi cha fedha, kwa ajili ya kuwarubuni mabinti wa Kikristo huko vijini, kwa kuwatongoza, na kuwapa ahadi ya kuwaoa, pindi watakaposilimu na kuwa waislamu, na njia kubwa zaidi ambayo ilikuwa ni njia rahisi zaidi ni kuwajaza Ujauzito (Hapo unakuwa umeshamnasa kirahisi) kwani utakataa kumtunza ikiwa bado yu ngali Mkristo, Mabint ambao hawakuwa na msimamo kiukweli walinaswa na mtego huo, kuna jamaa yetu mmoja Anaitwa Rashid, yeye alimeza Suratul Yusuph, (Sura ya 12 ndani ya Quran) kwa njia ya KOMBE, na kusomewa dua nzito, Wanawake wampende kama alivyopendwa na Yusufu na mke wa Firauni, Wanawake hawakuthubutu kumkataa, baadae alikuja kuwa Mfanya mihadhara wa Mwanza, na (kwa sasa ni marehemu, amekufa kwa H.I.V ) Nami nikamuomba anifundishe njia hiyo Ili nipate kuwanasa mabinti wa Kikristo kwa urahisi, Nilipomuambia Rashid anifundishe nami niweze kuimeza surat Yusuf niwe kama yeye, akaniambia nivute subira, ipo siku atanifundisha, nilinywea sana kwa sababu nilihitaji sana nami niwe kama, yeye, ila sikujua ni lini atakuja kunifundisha Elimu hiyo ya kumeza surat Yusufu na kuwa na mvuto kwa wanawake kama alivyokuwa Yusufu, Harakati za ujenzi huo wa misikiti ukaendelea, hatimae tukaanza ujenzi wa vijiji ya Igombe.
baadae niliacha harakati hizo, nikaendelea na mambo ya mihadhara, ambayo niliipenda sana harakati hizo, kwani siku ya kwanza nilishuhudia Kina Anwar, pamoja na Alii Kadogoo, wakifanya Muhadhara katika uwanja wa Mkanyenye, wakiwa wameweka meza mbili, moja wanapokaa Wahadhiri, na nyingine ya msomaji, nilishawishika sana kukaa na kuwasikiliza namna ambavyo walikuwa wakiichambua BIBLIA, Kuwa Yesu sio Mungu, Paulo ni mtume wa uongo, na maneno mengine mengi, ikiwemo utabiri wa Muhammad ndani ya BIBLIA, nikawa kila siku naenda kwenye mihadhara kufuatilia (Wakati huo Wakristo hawakuwa na uwezo wa kukabiliana nao) nikawa naona Wakristo wengi wakisilimu, sikujua kama Walikuwa wakikabaishwa, nilijua Waislamu wale walikuwa wakifundisha kweli, nikatamani niipate elimu hiyo, ili niweze nami kuitumia kuwasilimisha Wakristo kwa urahisi, (tofauti na ile ya mwanzo ya kuwapa ujauzito mabint Wa Kikristo) Kwa hivyo kila siku nikawa muhudhuriaji wa mihadhara, nikawa nachukua kalamu na daftari, nikawa naandika aya za kuwabana Wakristo, ikafikia hatua hata shule nikawa natoroka ili tu niende kwenye Mihadhara, siku moja tukatangaziwa kuwa anakuja muhadhiri mkubwa, MAZINGE, walimpamba sana kiasi cha kunifanya nitamani kumuona, siku ambayo alikuwa anakuja, Ustadh wangu Thuqmal akatuchukua mimi na Ahmad Saidi, twende nae Kirumba kuna kisomo tunaenda kukifanya, mida ya saa 10 JIONI, muda ambao Muhadhara unaanza, ndo siku anayokuja Mazinge, nikawa sina namna ikabidi tu niende KIRUMBA, kufika katika nyumba hiyo, palikuwa na mbuzi dume, tukaambiwa tumchinje, kisha kichwa chake tuingie nacho ndani, nikapewa Sulululu, nichimbe kwenye usawa wa mlango, ili kichwa kile kifukiwe hapo, CEMENT nikaitifua nikachukua panga.na.kuchimba, na kisha Ustadh THUQMAL akakishika kile kichwa akawa anakishusha chini, (Nikawa sielewi elewi) kuna maneno akawa anatamka kiarabu ambayo sikuwa nayafahamu maana yake, akimaliza kusema maneno yale, anasema tena يا الله يا الله يا الله Wakati huo ubani unachomwa, kisha akakitumbukiza kile kichwa, ukatoka moshi mweusi, na kuniamuru mimi niliyechimbua, ndiye nifukie, nikaogopa, wakati nasita kufukia nikamwambia "Unajua Ustadh, hiki kitu ndo kwanza nakiona leo elimu, hii ya kuzindika, tena kwa kumtaja الله سبحان ndo kwanza naishuhudia leo, huu moshi uliotokeza humo ndani wakati hatujaweka moto unatoka na nini? na kwa nini nifukie mimi badala ya wewe uliyesababisha moshi huo utokee? akanikazia macho kwa hasira, Mwenzangu Ahmad akasema......... Utaendelea.

Comments