KWA MUNGU WA ISRAELI YOTE YANAWEZEKANA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tena karibu sana tujifunze neno la uzima.
Kama wateule wa MUNGU ni muhimu  mamlaka ya MUNGU unayemuomba na ni muhimu kujua vigezi vya MUNGU kukujibu maombi yako.
Hakuna Jambo Lisilowezekana? 
Kwa JEHOVAH MUNGU Yote Yanawezekana
Yeremia 32:27 ''  Tazama, mimi ni BWANA, MUNGU wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? ''
-Hakuna jambo gumu kwa MUNGU wetu.
-Yeye Ni MUNGU Mwenye Nguvu Zote Za Kukutoa Kwenye Matatizo Yanayokuandama.
Zaburi 68:20 '' MUNGU kwetu sisi ni MUNGU wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA BWANA.'' 
-Mteule lazima ujue kwamba ushindi ni wako kama ukibaki katika kusudi la MUNGU. Mengi hayatokei kwako kwa sababu ya wewe mwenyewe na sio MUNGU. 
MUNGU ana utaratibu wake na ajabu hata ameweka nguvu ndani yetu ili tupokee kwa imani yale tunatakayo na imani hiyo kwa sababu ina macho ya kuona , ni lazima tupokee.

BWANA Ametoa Mamlaka  Kwa Watoto Wake Waliotakaswa Kwa Damu Ya Mwanae YESU KRISTO
Yohana 1:12-13 '' Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU ''
-Kazi Ya Watoto Wa MUNGU Ni Kuamini Na Kuomba Tu
Marko 9:23 '' Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. '' 
-Ukiwa na imani lazima yote yatawezekana kwako. imani ni muhimu sana lakini lazima imani ihusike katka maombi.
-Maombi Sahihi Pia Lazima Yaombwe Kupitia Jina La YESU KRISTO
Yohana 14:13-14 '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. '' 
-Pia kama wateule na waombaji ni Lazima Tutambue Kwamba Tutamuona MUNGU Kwa Matendo Atakayotutendea Ikiwa Tukiishi Maisha Matakatifu
Waebrania 12:14 '' Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona BWANA asipokuwa nao; '' 
-Tukienenda Kama BWANA MUNGU Wetu Anavyotaka Hakika MUNGU Atatushangiliza Na Dunia Nzima ''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote. -Zaburi 83:18).

 -Tutamwita BWANA Kwa Maombi, Naye Atatujibu Na Sisi Kazi Yetu Ni Kumtukuza
Zaburi 50:15 '' Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. ''
-Ndugu Zangu, Tumwite MUNGU Wetu Maadamu Yu Karibu Ila Lazima Mdhambi Aache Dhambi Zake Zote.
Isaya 55:6-7 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. '
-Omba Maana Yote Kwa MUNGU BABA Yanawezekana.
- Maombi Ni Maisha Na Lazima Tuwe Waombaji Siku Zote. -BWANA Wetu Yu Karibu na hujibu maombi ya watoto wake waaminifu.
Luka 1:37 ''  kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU. ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments