KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?:ABELI SULEIMAN(Sehemu ya 2)

Na Abel Suleiman Shiriwa.
Ushuhuda unaendelea, kama hukuusoma sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Baada ya kufuka ule moshi nami kusita kufukia, na kumtaka Ustadh mwenyewe afukie, AHMAD Said, akaniambia, "Abubakar acha uoga mbona ni jambo tu la kawaida, moshi huo ni ishara ya dua kusikiwa, لا تخف (Usiogope)" Nikawa sina namna, ikanilazimu nifukie, kisha ikaletwa CEMENT tukachanganya na mchanga, tukapasafakia vizuri, kisha ikawekwa NILU, wakaambiwa kuwa pakikauka waweke Zulia, Kiwili wili cha yule mbuzi, sisi hatukuruhusiwa kukila, wala wahusika wa nyumba ile pia nao hawakuwa na idhini hiyo ya kula nyama ile, wakapewa watu wengine kama nyama ya msaada.. (Mkristo uwe na tahadhari na nyama mpewazo na waislamu bila kujua hakika yake) Tulipoondoka, (Ilikuwa saa 12 Jioni) Njiani nikamuuliza Ustadh hivi ile nini? Akaniambia, "Ukitaka kuwa sheikh hupaswi kuwa mtu mjinga mjinga, ni lazima uwe mjanja, tulia kijana wangu, nitakufundisha ili utengeneze maisha, maana usione tunajenga nyumba ukadhani ni mishahara tu ya ufundishaji wa Madrasa, vitu hivi vinalipa sana lazima uwe na علم الجن (Elimu ya majini) Nikamuuliza اي? (Ipi)? Akasema اصبر (Subiri) Tukatawanyika yeye akaenda zake kwake, MIMI na Ahmad tukarejea zetu GHANA, (Huyu Ahmad Saidi) Kwao ni GHANA mtaa wa kifua wazi nyumba ya nyumba ya FARAI mwarabu, baba yake mkubwa ni mganga, (FUNDI) anatibu kwa kutumia qur'an na mambo mengine, Wakati tunatembea nikamuuliza, "Kulikoni jambo hilo mbona me sielewi? "Akaniambia, zingatia kauli ya Ustash, Hakuna Sheikh mjinga" Ustadh kwa tukuo hilo ameshapewa MILIONI 2 kikubwa tu tuendelee kukaa karibu nae" Basi tukafika maneno ya home, mawazo yamenijaa nikifikiria nijifunze hiyo علم الجن
Au niachane nayo? moyo wangu haukumisukuma kabisa kujifinza Elimu hiyo, niliona itakuja kuwa na athari kwangu, japo majini ni sehemu ya uislamu, na ni maislamu na yenye kufundisha uislamu, sikutaka kabisa kudili nayo, maana ni wengi yameshawakausha kwa kutofautana nayo katika maagano.

Kwa hivyo kesho ilipofika nikaendelea na ufuatiliaji wa mihadhara, nikitoka tu shule basi huyo naenda zangu kwenye mihadhara, na Mazinge nikabahatika kumuona kwa mara ya kwanza kesho yake baada ya tukio akipeleka somo la UKIMWI kwa mujibu wa BIBLIA, maandiko alivyokuwa anayatoa nikawa nayaandika uzuri nilikuwa mwepesi sana kuhifadhi maandiko, ki ukweli nilimuona ni mtu mmoja wa ajabu ambae hakuna mwenye uwezo wa kushinda nae (Lakini nilivyoachana na uislamu nimejadiliana nae na nikamgalagaza katika mada, UBUNGO) Hiyo nitaieleza kwenye mwendelezo, kwa hivyo nikampenda sana, maana Mpaka Wachungaji wakawa wanamkimbia, nikazidi kumfuatilia, akienda viwanja vya FURAHISHA nipo, wakati huo akiwa na msomaji wake aitawe YAHYA HOSEA KIHANDO, somaji yake ya kichwa bila kufungua kitabu, ili nivutia sana, nami nikajiapia kuwa ni lazima siku moja niwe kama yeye kwenye usomaji, au niwe mwalimu kama MAZINGE. akienda Mkuyuni nipo, Nyamoro, KILIMAHEWA, na sehemu zingine nikawa nao nawafuatilia na kuendekea kujifunza.
Tukirejea upande mwingine nje na mihadhara, kulikuwa na wanafunzi ambao nilikuwa nilikuwa nawafundisha QURAN maana kwenye uislamu unasoma na huku unafundisha, kwani ni mwendo wa kukaririshana, kile ambacho najifunza THAQAAFA basi mimi nami pia nikawa nawafundisha wanafunzi hao, pia hata siku za J'mosi na J'pili katika madrasa aliyokuwa anafundisha Ustadh Thuqmali, siku akiwepo najifunza kwake, nami siku ambayo hayupo basi nikawa najukumu la kuwafundisha walio chini yangu, kwani Madrasa hiyo, walikuwa wanafundishwa quran tu, AHMAD yeye alipendelea kwenda nyumbani kwa USTADH akajifunze Elimu ya majini ambayo mimi niliikataa, THAQAAFA kulikuwa na masomo mengi, kama vile.
لغة (Lugha)
سيرة الرسول(Maisha ya Mtume)
قراء (Kusoma)
فيقه (Mambo ya kisharia)

Na masomo mengine mengi, kwa hivyo mimi nikawa na upeo kwa kiasi fulani kuliko wale wengine, Niliendelea kufuatilia Mihadhara, nikamshawishi na AHMAD tuwe tunahudhuria, akakubali, kwa hivyo yale ambayo tunayachukua, tukifika nayo mtaani kwetu, basi tunawatafuta Wakristo na kuanza kuwaambia kuwa wamepotea, wapo baadhi walisimu, (Kuna wengine walirejea baada ya mimi kuachana na uislamu) Wale ambao sikubahatika kuonana nao roho huniuma sana, pia Naomba ifahamike kuwa mtu aliye mkristo anaposilimu tu, nguvu ya majini humtawala vilivyo kiasi kwamba kutoka huko bila neema ya KRISTO ni vigumu, huumbiwa namna ya kuwa na hasira kwa mtu anaeusema uislamu, pia roho ya kuua inakuwa karibu nae sana kuliko mtu aliezaliwa akiwa muislamu..... harakati zangu zikaendelea, kipindi ambacho kina Mazinge wanaondoka nabaki kuendelea vizuri na masomo wakirudi naendelea kuwafuatilia,
Kuna siku moja Kina Mazinge akiwa na wenzie kina Yahya, Musa Pascar, IDD Pengo, Omary Mussa, Waliomba kibali cha kufanya muhadhara pale FURAHISHA, wakapewa, Muhadhara ukafanyika kwa muda wa wiki mbili, akaja Jamali GERMANUS, akasema yeye alikuwa Padre, alisilimu baada ya kutambua kuwa uislamu ni dini ya kweli, alijenga hoja mpaka Wachungaji wakawa wanaikimbia meza ya maswali, nikamuona nae ni msomi wa LEVEL ya juu sana, (Lakini baada ya kuachana na uislamu, Jamal, nilimburuza katika hoja mwanza mwaka 2009 Nikiwa na Cecil Simbaulanga, pia kubwa zaidi ni mkoani Ruvuma, Wilaya ya MBINGA, mwaka 2012 Mwezi wa 3 Ndani ya siku 5 Jamal alionekana hafai mbele za Waislamu waliomkodi kwa mbewembwe baada ya kumpa kibano, Mtu alie MBINGA habari hizi anazijua na pia Waulizeni wachungaji watakuambieni)....... Kwa hivyo wachungaji wale wa MWANZA walivyokimbia Jamali, nikazidi kujipa moyo kuwa nitawasilimisha wengi sana, Kibali kilipoisha waislamu Wakaendelea na muhadhara kibabe, Wakatutangazia kuwa kesho tutafanya mchango kwa ajili ya kumleta DR. SULE, kumbe CHRISTOPHER Mwakasege, nae ameshapewa kibali baada cha waislamu kuisha, kesho yake tunaenda pale tukakuta uwanja umezungushiwa vyuma kwa ajili ya mahema, tukakaa kikao tufanye nini ili muhadhara uendelee, tukaazimia kuving'oa vyuma vile, tulipokuwa wengi tukafanya hivyo, POLISI wakaarifiwa, hatuna hili wala lile tukastukia gari za Polisi hizo, watu wakaanza kukimbia wengine wakashikwa, mimi wakati nakimbia kanzu ikanipigisha mweleka, nikaanguka vibaya, Ile kuinuka tu....... UTAENDELEA.

Comments