NI KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO? ( 6

Na Abel  Suleiman Shiriwa


 Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA
Wakati naingia kwenye fensi ya msikiti, Nikakutana na Imamu Abdallah Panya, nikasema, “Yes, naanza na huyu Kumuuliza swali, nikamsalimia, ;Assalaam Aleykum” Nae akaitikia, “ Waalaykum Salaam, kaifa Haaluka?” Nikamjibu, Al-hamdulillahi, namshukuru Allah ananipa uzima” Akawa anataka kuondoka, nikawambia, Nina shida nawe, Akasema, “Shida gani?” Nikamwambia, “Nahitaji kufahamu, ni kwa nini sisi Waislamu, tumaswalia (Kumtakia Huruma) Mtume, na badala ya yeye kutuswalia sisi?” Akacheka, akaniambia, ‘Umefikiria nini?” nikasema, “Nataka tu kujua ni sababu ipi?” Akasema, “Mambo mengine katika Imani, si yakutaka kufahamu hakika yake, Hakika yake itajulikana siku ya Kismamo (Qiyamu)” Alla ameshasema, tumatakie Rehema, Mtume wake sasa tutamuhoji Allah?” Nikasema, Sawa, nitaendelea kujifunza, nikaondoka zangu, akili yangu ikinikatalia kuyakubali Majibu ya Imamu Abdalah Panya,, nikajiuliza, kama ni kweli huyu tunaemwabudu kama ndiye Kweli, ni kwa nini atulazimishe sisi tumuombee Rehema, wakati yeye ndiye mtoaji wa Rehema? na sitoshe mpaka leo Mtume amekwisha kufa, hizo rehema tunaendeea kumuombea mapaka lini? Na hukumu ya kutokumuombea Rehema Mtume, inakufanya usiwe mfuasi wake, Nikajiulza ni kwa nini Yesu yeye awe muombezi na mpatanishi wa wanadamu, halafu Mtume wangu Muhammad ambae nilifundishwa kuwa, ni mbora kuliko Yesu, yeye ndo tumuombee, ina maana huyu hajui hakika yake itakuwaj?, na kwa nini Imamu anaimbie kuwa mambo mengine siyo ya kuuliza, hakika yake itajulikana huko huko” Ina maana kama jambo lina mashaka, niache kutafuta hakika yake? Nikasema, hapana, nikaenda zangu nyumbani, Nikaanza kutafuta hela, ili nikanunue Kile kitabu cha Mkweli Mwaminifu, ambacho nilikisikia kikisomwa na Wakristo, na kweli hela nilipata, nikaenda kuuliza tena, kwa bahati nzuri nikakuta kimebaki hicho hicho, nikakichukua, nikarudi nacho Home, nikaanza kujisomea, nikaanza kupitia Utangalizi wa Milango, ndipo nikaona Mlango wa kumtakia Rehema Mtume, nikafungua, kisha nikasoma, Nikakutana na Hii Hadithi
Kasema Mtume (S.a.w)
“Atakaesali sala ya Alasiri siku ya Ijumaa, Basi akasema kabla kuinuka alipokaa: Ewe Mwenyezi Mungu Msalie Muhammad Nabii asiyejua kusoma ala kuandika na juu ya wafuasi wake, na umsalimu (Amani ya) Milele mara thamanini, (Basi) Anafutiwa madhambi ya mika tamanini” (Mkweli Mwaminifu, Juzuu ya 1-2 Hadithi Na. 347, Uk. 160)

Nikaanza kupata wasi wasi, inakuwaje Mtu ufutiwe madhambi ya mika 80 kwa kumuombea Rehema Mtume? Kama mtu hujafikisha miaka thamanini ya kufanya hiyo madhambi, yaani kama una mika 30 Ukamswalia mtume, madhambi ya miaka uliyoanza kubaleghe, au kuvunja ungo, yaani tuchukulie miaka 12, Hapo ndo umeanza kuhesabiwa dhambi, kama una mika 30 maana yake hapo, Una msamaha wa mika 18 Iliyopita, na ili itimie miaka 80, Inabidi uende mpaka miaka 92 Ndo uanze kuhesabiwa tena dhambi, nikasema, hapana, haya siyo mafundisho kabisa, ndiyo maana Waislamu, tunafanya maovu mengi, tunafanya matukio ya kinyama ya kuua watu ovyo, kwa sababu tunamsamaha, wa dhambi, kwa kumuombea rehema Mtume,,, hapo nikapata hamasa zaidi ya kuanza kuhudhuria mikutano ya Kikristo zaidi kuliko Mihadhara ya Kiislamu, maana kule kwa waislamu niliona hawafundishi undani wa uislamu, zaidi ya kuishambulia tu Biblia, nakiri wazi kwamba, Wahubiri wa Kikrsto walinipa mwangaza mkubwa sana wa kuweza kuchambua imani hizi mbili, lakini niliendelea kuuliza maswali kama kawaida, huku nikiendelea kusoma, Quran na Biblia, na kitabu changu kimoja cha Mkwelin Mwaminifu, Kila nikisikia Ernest ameandaa Mkutano, mimi huyo naenda kuuliza maswali, kama kawaida, kipindi cha awali, kabla sijaanza kuchumbua, nilikuwa natoa matusi sana kwenye Mkutano wa Ernest, kiasi kwamba Wakristo wakawa hawataki kabisa, me kuuliza maswali, lakini Ernest akawa anawaambia kuwa, ‘Mwacheni tu, kwani sisi tumeambiwa tuwe tayari kumjibu kila mtu atuulizae habari ya tumaini lililo ndani yetu, lakini kwa upole na hofu” Alitoa Andiko la 1 Petro 3:15, kwa hivyo akawa ananipa hamasa ya kuendelea kuuliza, nikizidiwa, naondoka kwa AIBU, wakati huo naitwa Ustadhi mdogo, nyumbani walinipenda sana, kiasi kwamba Mother, akawa ananipa mpaka Nauli niende kuuliza maswali, Ki ukweli nilipata sapoti ya kutosha, siku moja nimeenda pale kwenye Mkutano wa Kina ERNEST, Nikakutana na Somo la UUNGU wa Yesu, alikuwa anafundisha Myahudi, baada ya kumalizika, wakahitisha maswali, me nikasema, Kwenye UUNGU WA YESU, hapo ndo tutachengana na Wakristo, nikaenda kukaa, na swali langu likatoka kwenye
1 Timotheo 2: 5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
Ni andiko ambalo nilichukua kwenye Muhadhara wa kina Mazinge, nami nikaona ni nzuri kweli, kuwa Kumbe Mungu ni mmoja, na Yesu ni Mwanadamu, nilipooa lile andiko nikauliza, “Mmesema Yesu ni Mungu, sasa inakuwaje katika andiko hili Yesu ni mwanadamu?” Ernest aliinuka na kusema, “Umeuliza swali nzuri sana, na umetoa andiko la Mtume Paulo, na kwa bahati mabaya, hakuna muislamu hata mmoja mwenye elimu ya kuweza kuzifundisha nyaraka za Paulo” Akatoa andiko hili.
2 Petro 3: 15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
17 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.
18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.

Niliposomewa nilipolisikia, nikaanza kuelewa, kwa ni kwa nini maandiko ambayo walikuwa wanayatoa Wahadhiri wa Kiislamu, nilikuwa nabawana nayo, kumbe walikuwa wanaapotosha, sasa Ernest akasema,, ili ujue kuwa umekurupuka, Umetoa andiko linasema, Yesu ingawa ni mwanadamu, lakini peke yake ndiye mpatanishi kati ya wawanadamu na Mungu, sasa Muhammad amefuata nini wakati Yesu peke yake ndiye Mpatanishi baina ya Mungu na Wanadamu, kwa sababu akili yangu niliiruusu kujifunza, nikasema, kumbe maandiko huwa tunayaandika na kisha kwenda nayo kwa Wakristo bila kujua, hakika yake, inamaana hata andiko hilo, Waislamu hatulichukulii kwa uzito kwa habari ya Yesu kuwa mpatanishi, tumeshilia tu umwanadamu, Ernest siku hiyo alinifungua, sana tena maandiko haya ambayo aliyaongezea katika Mafundisho yake, niliyapenda nayo ni haya.
Luka 24: 45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
Akasema, Ili maandiko ya Biblia uweze kuyaelewa, basi unatakiwa umruhusu Yesu aifungue akili yako, ili uweze kuyaelewa maandiko, maana ni Yesu tu ndiye mwenye kuwapa watu akili ya kumjua Mungu wa kweli,
1 Yohana 5: 20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Akaniambia tena kuwa, Abubakari huko uliko hakuna Mungu wa kweli, kwani Mungu wako unaemwabudu mwisho wake ni motoni, akatoa hadithi hii
Hadithi ya Anas Ibni Malik (r.a) kuwa Mtume
(s.a.w) amesema jahanamu itaendelea kusema,
“Je, kuna nyongeza”? Mpaka Allah atakapoweka
humo unyayo wake na hapo utasema, Qat Qat
(inatosha inatosha) naapa kwa nguvu zako na
zile sehemu zake nyingine zitakaribiana na kuwa
pamoja” (Bukhari Hadithi Na. 654, Juzuu ya 8)

Hapo ndipo kwa mara ya kwanza, nikasikia Allah mwisho wake ni motoni, nikajiuliza, Kwa nini Masheikh huwa hawatufundishi haya?, tunasomeshwa kiar abu kwa wingi bila hata kufasiriwa kwa kiswahili, na ambayo tunafasiriwa ni yale mazuri mazuri, Ernest akafafanua kuwa,
kwa mujibu wa Biblia, atakaae kuwa wa Mwisho kuingia, motoni, ni Ibilisi shetani. Akatoa andiko hili,

Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Kwa kweli nilipata fadhaha kubwa sana, nikamwambia Nimekuelewa Ernest, nikainuka mezani, Waislamu niliokuwa nao, wakaniambia, :Sasa ndo nini unaanya?” Mbona unaondoka bila kufafanua hayo ambayo yamesemwa”? Nikawaambia, niacheni kwanza, niende nyumbani, nikatulie, kweli nikashuka zangu, mapaka Stendi nikaenda nyumbani, nikafika mapema, mpaka wakashangaa, imekuwaje nimewahi wakati Muhadhara kule ufanyka mpaka usiku, Nikawaambia, “leo nimechoka,” Nikaingia zangu ndani, Nikachukua Biblia yangu ya agano Jipya ambayo nilikuwa nayo, nikaifungua, ili nirudie kuisoma hiyo Ufunuo 20:10, Nikaona ni kweli Ibilisi atatupwa katika moto, alimo yule mnyama na yule nabii wa Uongo, nikaikumbuka na Ile Hadithi, ambayo ilisomwa, yaani hii
Hadithi ya Anas Ibni Malik (r.a) kuwa Mtume
(s.a.w) amesema jahanamu itaendelea kusema,
“Je, kuna nyongeza”? Mpaka Allah atakapoweka
humo unyayo wake na hapo utasema, Qat Qat
(inatosha inatosha) naapa kwa nguvu zako na
zile sehemu zake nyingine zitakaribiana na kuwa
pamoja” (Bukhari Hadithi Na. 654, Juzuu ya 8)

Nikaanza kusema moyoni, hapa Waislamu tutakuwa tunamwabudu Ibilisi aliyekuja kwa sura ya ki UUNGU, nikakumbuka kuna andiko nilisawahi kulisoma, katika Mathayo 25:41, ngoja nilinukuu
Mathayo 25: 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Nikawa nawazyoni mwangu, hapa si mwabudu Mungu wa kweli, hapa nimeuziwa mbuzi kwenye Gunia, Iweje mungu aende motoni, tena sehemu zake nyingine zikaribiane, ziwe pamoja, kama unavyouunguza mfuko au plastic, huwa zinakaribiana na kuwa pamoja, ndivyo ilivyo kwa Allah, halafu nikatafakari mle nimeona pia yumo Nabii wa Uongo, huyu Nabii wa UONGO atakuwa nani kama siyo Muhammad?
Nikasema, kumbe ndiyo maana tunalazimishwa kumuombea Rehema, Mungu amuhurumie, Kumbe Allah anajua kuwa yeye na Muhamamd mwisho wao, ni motoni, nikapata picha ni kwa nini waislamu tunamuombea Rehema, Kumbe Abdallah Panya, alinipa majibu yale bila kunijuza kuwa Allah mwisho wake, ni motoni, na Yesu amesema, moto umeendaliwa Ibilisi na malaika zake, akilini mwangu nakawa nawaza huyu allah atakuwa nani kwa kuingia kwake motoni? Nikajua pia ni kwa sababu gani Muhammad alisema hajui hatima yake kama ataenda motoni au peponi, ndo maana akakutwisha zigo kubwa, la kumuomba rehema, kwa kutudanganya kuwa, tutapata msamaha, wa dhambi za miaka 80, Pia nikasema, Maandiko ya Biblia, ni hakika, kwa sababu Quran, imekuja baada ya Biblia, kuwepo, ina maana Allah kabla ya kumleta Mtumewe, aliisema maandiko ya Biblia, ili kutuhadaa, akaamua kuyachukua majina ya ya watu Muhimu katika Biblia, ili tuamini kuwa ni mungu kweli, nikasema, leo siende kabisa msikitini, Kumbe napoteza muda wangu, kuswali, na kutapa alama usoni kama kitumbua kilicho ungua, kumbe, namwambudu mungu anaenda motoni? Na kwa wakati naendeea kutafakari, nikasema, ngoja nimalizie andiko la Ufunuo, ili nijue baada ya Ibilisi na huyo nabii wa uongo kuingia motoni, Je ni kina nani ambao hawataingia motoni? Nikaisoma, nayo inasema,
Ufunuo 20:11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Aya ya 15 Ikanifanya nisisimuke, nikajiuliza, hicho kitabu cha Uzima, cha Mwanakondoo, ambacho mtu kama hatoandikwa, jina lake humo, atatupwa katika lile ziwa la moto, na kama ameandikwa hatoenda motoni, ni kitabu gani? Nikasema, ngoja niende kwenye Muhadhara wa Kikristo ili nikawaombe hicho kitabu cha Uzima, nione majina yanandikwaje, Nikatoka zangu chumbani, nikawa waaga kwa kudanganya kuwa naenda kuswali, kumbe lengo langu, ni kurudi kwenye Muhadhara wa Wakristo, brother, Mzee au Said, akaniambia, “Nisubiri twende wote msikitini, Nikamtazama kwa Hasira mzee, nikifikira, mimi lengo langu si kwenda msikitini, bali kwenda huko kuangalia hicho kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo kama wanacho wanipe nisome majina yanasajiriwaje ya watu waingiamo mbinguni, halafu huyu ananiambia kuwa, nimsubiri twende msikitini, anataka kuniharibia lengo langu, kwa sauti ya Hasira, nikakwambia Mzee….. UTAENDELEA
Usikose sehemu ya 7 ya Ushuhuda huu kesho Mungu akitupa uzima.

Comments