NI WENYE WOKOVU WA KWELI TU, NDIO WATAINGIA MBINGUNI

Na Mtumishi  Geofrey Mwanza, Mombasa Kenya.
Bwana Yesu asifiwe sana?Karibu ujionee ujumbe huu (UFUNUO 20:11-12 "Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa cheupe,na yule aketiye juu yake.Dunia na Mbingu zikatoweka mbele ya macho yake na hazikuonekana tena.Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo,wamesimama mbele ya kiti cha enzi,na vitabu vikafunguliwa.Halafu kitabu cha uhai,kikafunguliwa pia.Wafu wakahukumiwa kadri ya matendo yao,kama vile ilivyoandikwa kwa vitabu hivyo

Biblia inaonyesha kuwa matendo yetu ya kila siku yanaandikwa kwenye vitabu fulani na ambavyo kuna siku ya mwisho ambayo vitabu hivyo vitakuja kufunguliwa na kila mmoja kusomewa hukumu yake kulingana na matendo yake hapa duniani.Kabla ya hukumu hii kuna usingizi ambao kila mmoja atalala

(Ufunuo 14:13"Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema'Andika heri watu ambao tangu sasa wanakufa wakiwa wameungana na Bwana .....".

Ni vizuri kukaa kwa utayari wa kwenda mbinguni kwa kumkubali YESU KRISTO akuokoe na uishi maisha ya kuitenga dhambi.Watu wengi utawapata kwa pombe,masengenyo,kiburi,wivu,uasherati wakiufanya na ukitaka kumuonya mambo haya atakwambia ameokoko maana aliombewa wokovu na mchungaji wake.Wengine wataishia kukwambia "Wanambia nini kuhusu wokovu? Nikiokoka hata hukuwa umezaliwa!" Na ukiwaangalia unaona mienendo yao ikiwa kando na wokovu.Basi ninao ujumbe mzuri kwa watu kama hao,"Rekebisheni mienendo yenu maana hamna mbingu ya watu wenye tabia kama hizi".Pia ukienda katika mikutano ya mazishi na hata pia  kwa facebook utapata maneno kama: R.I.P,Tutakutana mbinguni n.k. Je,unapomwambia huyu aliyekuacha heti Rest In Peace(R.I.P) atapumzikaje kwa amani kama hakuwa ndani ya YESU KRISTO? 

Huwezi pumzika kwa amani ukiwa nje ya Yesu,maana Yesu mwenyewe ndiye "AMANI".Ningewaomba watu wa MUNGU kila mmoja wetu tuzichunguze njia zetu na tumkaribie YESU atupe pumziko la uzima wa milele.Huwezi ingia mbinguni ukiwa na uchafu wa dhambi heti unaenda kanisani kila siku.
 Barikiwa sana na uokoke kama bado hujaokoka na kama umeokoka ambia Mungu azidi kutupa funuo zaidi.
"THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES- Kenya  Call 0724 656 653.

Comments