HATARI SABA(7) ZA MKRISTO ASIYEKUWA NA MAOMBI.



 


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Leo tunazungumzia maombi jambo ambalo ni la lazima kwa kila mteule wa KRISTO.

Maombi ni maisha na maombi ndio mkono mrefu zaidi wa kupokea kutoka kwa MUNGU.
 ''BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia-Zaburi 5:3''


Hata kama huwa hufundishwi kuhusu maombi lakini naomba utambue leo kwamba maombi ni jambo la lazima tena la kila siku katika maisha yako ya wokovu.
 ''Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa BWANA.-Yakobo 1:6-7'' 

Usipoomba wakati uko salama tambua kwamba ipo siku utaomba tena kwa kufunga siku kadhaa baada ya kupatwa na magumu ambayo kama ungeomba muda huu badi hakika mabaya hayo yangekuja kwako hiyo baadae.

Maombi ni kuzungumza na MUNGU.
 ''Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao-Waebrania 11:6''.


Maombi huboresha uhusiano wako na MUNGU muumbaji wako.

Kinachoonekana kwako kwa nje ni matokeo ya kile kilichoko ndani.
BWANA YESU anasema '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.-Yohana 14:13-14''

Maombi huzalisha utulivu na amani hivyo maombi ni muhimu sana.

Usipopenda kuomba basi jiandae na magumu ya kiroho maana shetani na watoto wake hapendi wewe uwe salama tena ukiwa katika wokovu.
 ''Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu-Marko 11:24''.
-Maombi hayatakiwi kuwa ya kipindi fulani tu bali siku zote.
Biblia inakushauri.

ombeni bila kukoma;-1 Thesalonike 5:17 ''


HATARI 7 ZA MTU ASIYEKUWA NA MAOMBI.

         1.  Usipoomba  unawaimalisha adui zako.

 ''Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.-Yohana 15:7'
 
        2.  Usipoomba unakaribisha maadui zako kukutesa.
 ''Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.-Zaburi 63:1''
 
      3.  Usipoomba  maana yake unafurahia kushindwa kwako.
''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.-1 Yohana 5:14'' 
 
         4.  Hatima ya maisha yako iko katika maombi yako.
Usipoomba  utabaki kufedheheshwa siku zote.
‘’ Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.- Mithali 18:21 ‘’


           5.  Maombi yanaweza kukuwakilisha mahali huwezi kufika kwa njia ya kawaida. Usipoomba hutaweza kufika huko
''Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;-Waefeso 3:20'' 


            6.  Kama unataka kufanya mabadiliko ya jambo lolote katika maisha yako kwanza ni lazima uombe kubadilishwa kwanza wewe kabla ya kuyapokea mabadiliko hayo unayoyataka. Usipoomba badiliko litachelewa sana kufika.
''Na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.-1 Yohana 3:22'' 


           7.  Usipoomba hutaweza kuwa na macho ya kiroho hata uweze kuwatambua na kuwashinda adui zako.



''Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.-Waebrania 4:16''

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments