KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO? SEHEMU YA 8

Na Mtumishi wa MUNGU, Abel Suleiman Shiriwa.
Ushuhuda wa ajabu sana unaendelea, na kama kukusoma sehemu zilizotangulia basi Sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA Na Sehemu ya pili FUNGUA HAPA Na kwa sehemu ya tatu FUNGUA HAPA.
Kwa sehemu ya 4 FUNGUA HAPA
Na kwa sehemu ya 5 FUNGUA HAPA na sehemu ya 7 ni FUNGUA HAPA

Nikazunguka nyuma ya kanisa kumwangalia Ernest, lakini sikumuona, nikawafuata wale waliokuwa wanafunga vyombo pale, na kuwauliza,”Muhubiri yuko wapi?” Wakasema, bado hawajafika, wakaniuliza, “vipi bado tu hujampa Yesu maisha?’ Nikacheka, nikawaaambia baada jamani” Nikaondoka zangu, Nikamwambia Ahmad jamaa ndo wanafunga vyombo mpaka waje kuanza sijui itakuwa saa ngapi, akasema, ngoja me niende zangu mpirani, nikamwambia, sawa, akaondoka, nami, huyo nikaenda kuketi pale dukani kwa mama Mariamu, nikamkuta anahudumia wateja, nikampa hi, kisha nikachukua kiti kilichokuwa pale nje, nikakaa, wateja walipomalizika, akaniambia, “Vipi Ustadhi mdogo, jana ulikuwa wapi? Maana wenzio jana wamekuja hapa, wamebawa, hatari, yaani Almanusra, Waislamu watembezee Bakora” Nikacheka ana, nikasema, “Tatizo wengi wanapenda sana kukurupuka, mtu hajui maandiko anakuja hapa kuuliza unategemea nini kama si kubanwa?” Akanipa soda, nikawa nakunywa, huku nasubiri Mkutano uanze, walikuwa wanapiga nyimbo za Choir, baada ya kama dakika arobaini hivi, nikasikia sauti ya ya Mjuni (Msomaji wa Ernest) akiwaita watu waje kwenye mkutano, nikasema, ngoja kwanza waanze kufundisha, ndipo niende, baada ya muda fulani hivi, Somo likaanza kupelekwa, basi nikatega sikio langu kusikiliza, lilikuwa ni somo la Yesu siyo Issa, Katika kuwatenganisha, Ernest akasema, kwa Mujibu wa Biblia, Yesu alianza kufundisha akiwa na umri wa mika 30
Luka 3:23 Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,
Akauliza swali, “Ni andiko gani kwa mujibu wa Quran Issa ameanza kufundisha akiwa na mika 30, ili awe ndiye Yesu?”
Alifundisha mengi, na nikawa sina shaka na Somo hilo, ila point yangu mimi ikawa ni kwenye umri wa Yesu, Nafsini mwangu, Uislamu umeanza kuondoka, baada ya yale maandiko niliyo yaeleza katika sehemu ya 8 ya ushuhuda huu, niliyo yatafakari, Mwishoni, akaitisha maswali, nikawahi kwenda kukaa, Akasema, “Ustadh mdogo karibu sana” Nikamwambia “Ahsante” Akasema, “Somo la leo umelisikia?” Nikamjibu, “Ndiyo nimelisikia” Akasema, “Una swali katika somo hilo?”
Nikamjibu, ‘Katika utofauti wa Issa na Yesu, sina swali, kwani somo nimelielewa, ila tu kuna andiko ulilitoa, ambalo nataka nitoe andiko jingine, kisha nijenge swali” Akasema, “Haya unaruhusiwa” Nikamwambia msomaji, anifungulie Kitabu cha Ayubu 36:26

Ayubu 36:26 Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
Nikamwambia, ‘Kwa mujibu wa andiko hili, hesabu ya miaka ya MUNGU haitafutiki, yaani hakuna ajuae, hesabu ya miaka ya Mungu, tangu kuwepo kwake, sasa ninyi mnasema Yesu ni Mungu, na umetoa Luka Luka 3:23, Kuwa Yesu ameanza kufundisha akiwa na mika 30, huoni kwa mujibu wa andiko hilo Yesu hana sifa ya kuitwa Mungu kwa kuwa Hesabu ya miaka yake imetafutikana?” Ernest akasimama, na kusema, “Aboubakar umeuliza swali zuri sana, swali la Ufahamu, ambalo unapaswa kufahamishwa, ili siku nyingine usiwe na shaka na swali hilo, Miaka hiyo ambayo wewe umeiona katika Luka 3:23, siyo mika ya mwanzo na mwisho wa maisha ya Yesu, bali hiyo ni miaka ambayo Yesu alianza kuhesabiwa, baada ya kushuka duniani kwa Jinsi ya mwili akazaliwa na mwnamke bikira, tangu alipozaliwa, ndipo watu wakajua ndo mwanzo waa kuwepo kwake, lakini kabla ya hapo Yesu alikuwepo, Msomaji soma, Wafilipi 2:5-8
Wafilipi 2:5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Kwa hivyo Yesu baada ya kuja duniani, Watu wakajua kuwa, Umri wake huo alionza kuonekana nao baada ya kuzaliwa, basi ndo umri wake, hapana, Yesu, alikuwepo hata kabla ya umri huo uliotajwa katika Injili ya Luka, kwani Hata Wayahudi nao vivyo hivyo, walikuwa wakimuona Yesu, mdogo ki umri kama ambavyo ninyi leo mnamchukulia Yesu, Msomaji, soma Yohana 8:56-58
Yohana 8:56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?
58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

Unaona hapo sasa, Yesu alipowaambia wayahudi kuwa, Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu, nae akaiona, akafurahi, Wayahudi kama mlivyo ninyi waislamu, mnamtazama Yesu kwa jinsi ya Mwili, wakamwambia, Wewe Yesu bado bwana mdogo kabisa, hapa tuna wazee wetu, wana zaidi ya miaka 100 na wala hawajamuona Ibrahimu, wewe bwana mdogo tu, umezaliwa juzi juzi tu, hapo, hata miaka 50 Hujafikisha, unasema umemuona Ibrahimu? Yesu jibu lake likwa la kushangaza, yaani pamoja na hao wazee wenu kuwaona wakubwa kwangu, lakini mimi nawaambieni, Ibrahimu, kabla hajafikiriwa, kuzaliwa, Mimba yake haijatungwa, wala baba na mama yake, hawajajua kama watampata mtoto aitwae Ibrahimu, Mimi Yesu nipo (Hapo makofi kwa Wakristo yakaskika) Sasa unadhani ni umri kiasi gani? Msomaji soma tena Yohana 17:5
Yohana 17:5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
Hapo Yesu, anasema, yeye anao utukufu pamoja na Baba ambapo yeye Yesu pamoja na huo Utukufu wake, ambao tumeambiwa katika Wafilipi kuwa, alipotwaa Umbo la mwanadamu, Mwana wa Adamu, huo utukufu alijifanya kana kwamba hana, alikuwepo nao kabla hata ya misingi ya Ulimwengu kuwepo, Yesu Yupo, Duniani na vyote vilivyomo havijakuwepo Yesu yeye yupo, Sasa Aboubakari, tutajie umri wa Yesu, kabla ya Kuumbwa Dunia, mpaka sasa ana miaka mingapi?”
Msomaji akanipa Microphone, Ili nijibu, nikabaki nimeduwaa, nikasema, Kumbe Yesu yupo hata kabla ya Ulimwengu kuwepo, Ki ukweli nilishindwa kutaja Umri wa Yesu kabla ya Ulimwengu kuwepo, Wakristo wakawa wakishangilia sana, Nikamwambia Ernest,”Kwa hapa sina swali kabisa sina uwezo wa kutaja Umri wa Yesu kabla na baada ya kuumbwa kwa dunia” Akaniuliza “Una swali Jingine?” Nikamjibu “Hapana” Watu walishangaa sana kuona ustadhi mdogo nikiishiwa maswali, mpaka waislamu niliokuwa nao wakaanza kuniambia, “Vipi leo mbona hivyo?” Nikainuka akakaa muislamu mwingine, kabla hawajampa Nafasi ya kuuliza maswali, wakaitisha sadaka kwa ajili ya kuendesha mkutano, wakati Music unaimbwa, me nikaenda pale katika meza aliyokuwepo Ernest, nikamwambia, “Nataka kuongea nawe faragha” Akasema, “Vipi unataka kujitoa muhanga?” Nikawambia “Hapana” Tukatoa pembeni, nikamwambia, “Me nimefuatilia sana mafundisho yako na majibu yako, na pia mimi mwenyewe nimesoma vitabu vyote viwili, nimegundua kuwa, Uislamu siyo imani ya kweli, kwa hivyo Leo nimeamua kuwa Mkristo” Ernest akastuka, akaniambia. Acha utani Aboubakari, Hivi uko sirous?” Nikamwambia “Yeah tuingie kanisani unionyeshe kitabu cha Uzima, watu wanasajiliwaje, ili nami niwe miongoni mwa watu waliomo katika kitabu hicho”
Akacheka, Akasema, “Kitabu hicho hakuna mwanadamu ye yote mwenye kuwa nacho, bali kipo Mbinguni, kwa hivyo leo hii unapoamua kumpokea Yesu Kristo, na kisha ukaishi kama ambavyo Yesu anataka uishi, basi utakua tayari umeshasajiliwa kwenye kitabu cha Uzima”
Nikamwambia, “Sasa nawezaje kuwa Mkristo kama ikiwa Kitabu hicho ninyi hamna?” Akasema, “Sisi tutakuongoza Sala ya Toba, na hapo utakuwa tayari umeshampokea Kristo na kufanyika Bwana na Mwokozi katika maisha yako” Nikamwambia, “Tuingieni Kanisani, kwani sitaki Waislamu, wajue kama Leo nimeamua kuwa Mkristo, maana kwa jinsi wanavyoniamini, wanaweza kuniua” Ernest akasema, ‘Usiogope Aboubakari, Yesu amesema, mtu ambae atamkiri mbele za watu, yeye nae atamkiri mtu huyo mbele za Baba yake, na atakaemkana basi nae atamkana siku hiyo, Kwa hivyo jitokeze hadharani iwe ushuhuda kwa wengine” Kwa hofu nikakubaliana nae, huku nikijua, wakati wowote panaweza kusanuka…
Basi nikarudi kule mezani ambako wanakaa waulizaji wa maswali, nikawa nimesimama, Ernest akasema, “Leo tuna habari njema, Abubakari a.k.a Ustadhi Mdogo, leo ameamua kumpa Yesu maisha yake, Tutakuwa nae katika Imani ya Kikristo” Walifurumuka watu kuja kushuhudia kama ni kweli, watu walijaa, me nikatoka pale, nikaenda kule mbele kuongozwa Sala ya Toba, Ikafika kipindi cha kumkana Allah, nikaambiwa, niseme, allah (mungu muabudiwa na waislamu) ni shetani, Nikasitiza, nikawa nawatazama waislamu, nikajisemea, “Allah shetani tena?” Nikaambiwa sema, Ikaidi tu niseme. Waislamu wakawa wanasema, “Huyo Mwana haramu, leo hatoki, ama zake ama zetu”
Baada ya Sala ya Toba, Wakristo walikuja kunipa mkono, wengine wakanipa hela kama zawadi, Hapo mimi natetemeka, Macho yangu yapo kwa waislamu, hatima yangu itakuwaje? Maneno yao yameshanitisha, nikawa nasema, Lazima wataniua hawa jamaa, Nikanunuliwa zaidi ya Soda 6, Moja yenyewe sikuimaliza kwa sababu ya hofu, nipo natetemeka, Nawatazama Waislamu, wanavyo ninyooshea vidole, na kuniita Mwana haramu, Baada ya shamla shamla za Ustadhi mdogo kumpokea Yesu, baadae nikaambiwa, “Aboubakari, Shika Microphone, uwasalimie watu wajue kuwa kweli Wewe umeshakuwa mwana wa Mungu” Nikashika, Maiki, kisha nikasema, “Kama kuna kidume ye yote wa Kiislamu anajiamini, akae mezani hapo (Wakati huo mapigo ya moyo yanaenda kasi kwa uoga)” Baadae nikarudisha Microphone nikaenda kukaa, Nikaambiwa twende ndani kwa Mchungaji, Nikaingia mle, huku wakifurahi, Wakasema, “Usiwe na hofu, kwani kuna vijana wa Kikristo watakusindikiza kwenda nyumabani” Nikakaa mle na kina Ernest, Mida ya saa 3 Usiku, Tukatoka huku tukiwa na Mabaunsa wa Wakristo, wakatusindikiza,
Tukapitia njia ya Makaburini, tukatokezea Barabara ya kuelekea Kona ya Bwiru, kufika kona ya BWIRU wale wakarejea zao Ibungilo, mimi, Mjuni na Ernest tukatembea zetu kuelekea Ghana, kufika Green View, Ernest na Mjuni, nikawaambia, ninyi nendeni zenu, me ngoja nijivute mpaka home, GHANA, mtaa wa kifua wazi, Wakaniambia ‘Kesho usikose kuja” Nikawaambia “Pouwa” Me nikafika home, Nikakuta mlango umefungwa, nikaanza kuingiwa na hofu, nikasema, wameshapewa Taarifa nini?” Nikagonga mlango, Mama akafungua, akaniangalia kwa hasira, me nikapitiliza kwenda chumbani, nikawaza leo hapa kumesha sanuka, Nikasikia Naitwa kwa sauti ya Ukali, nikasema watakuwa wameshaambiwa, Nikafungua mlango ili nikajue nini naitiwa, nikatoka huku natetemeka…. UTAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 9 YA USHUHUDA HUU, UJUE KILIJIRI NINI BAADA YA KUTOKA NDANI.

Comments