SIKU YA BWANA I KARIBU, JE UNAFANYA NINI SASA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifnze Neno la MUNGU.
 Mathayo 3:2 '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''
-Huu Ni Mwaka Wa Kutubu. 
-Ni Mwaka Wa Kugeuka Kutoka Dhambini Na Kuingia Nuruni. 
-Ni Mwaka Wa Kusajiliwa Jina Lako Kwenye Kitabu Cha Uzima. -Ni Mwaka Wa Kuokoka. BWANA YESU Anaokoa, Ukimpokea Leo Unaokoka. Hii Ndio Agizo Nililopewa Kumwambia Kila Mtu. Tubuni Kwa Maana Ufalme Wa Mbinguni Umekaribi
 Marko 1:14-15 '' Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya MUNGU, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.   ''

  -Vitu Vinavyosababisha Watu Wengi Wamwache MUNGU Ni Pamoja Na Kiburi
.Kama Kuna Dhambi MUNGU Anaichukia Ni Pamoja Na Dhambi Ya Kiburi, Kiburi Ndicho Kilimshusha shetani Kutoka Mbinguni. Kiburi Namba Moja Ni Kumkataa YESU. 

Mambo Mengine Yanayosababisha Watu Wasimtii BWANA MUNGU Aliyewaumba Ni Pamoja Na 
-Madaraka, 
-Elimu, 
-Kazi, 
-Ujuzi, 
-Teknolojia,
- Utajiri N.k. 

Vyote Hivyo Chanzo Chake Ni Kupumbazwa Na shetani. 
Ndugu, Duniani Tutapita Wote, Tutaondoka Watupu. 
-Kuna Tutakaokwenda Mbinguni Maana Tumeokoka Na Kuna Watakaokwenda Jehanamu Maana Wamemkataa BWANA YESU Na Wala Hawakuliishi Neno La MUNGU.

 -Ndugu Unayekataa Kuokoka Leo Kumbuka Neno Hili Kuzimu Hakuna Cha Profesa Wala Mnajimu Wote Kwa Sababu Wamemkataa YESU Watateseka, Hakutakuwa Na Mtu Maarufu Wala Mtoa Mimba, Wote Watateseka Kwa Sababu Wanakataa WOKOVU Wa BWANA YESU Leo. Hata Leo YESU Anawaita Akisema Njooni Kwangu Ninyi Nyote Msumbukao Na Dhambi, Nami Nitawapumzisha
Mathayo 11:28 ''  Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. '' 
-Ukiisikia Sauti Yake Kupitia Ujumbe Huu Usiufanye Moyo Wako Kuwa Mgumu.

- Haihitaji Maono Kuhusu Kujua Kwamba Hizi Ni Siku Za Mwisho. Dalili Moja Wapo Ya Kwamba Hizi Ni Siku Za Mwisho Ni Upendo Wa Wengi Kupoa. siku za karibuni  Nilikuwa Kwenye Costa Kutoka Gongolamboto Kwenda Kariakoo, Njiani Kuna Mama 1 Alikuwa Amekaa Siti Ya Mwisho Nyuma, Gari Ile Ilikuwa Na Watu Wengi Wakiongea Mambo Mbalimbali. Ghafla Yule Mama Akapigiwa Simu, Alipopokea Alianza Kucheka Kama Sekunde 30, Wakati Akicheka Tena Kicheko Cha Kawaida Tu, Ghafla Zaidi Ya Nusu Ya Abiria Wakafyonza Kwa Nguvu Kwa Pamoja Kisha Wakaguna Huku Wote Wakimwangalia Yule Mama. Nilishangaa Tukio Lile Sio Mimi Tu Niliyeshangaa Bali Hata Waliofyonza Walianza Kushangaana Wao Kwa Wao Maana Hawakutegemea Kufyonza Pamoja, Baada Ya Hapo Kila Mtu Alibadilika Usoni, Kila Mtu Akavaa Uso Namba Mbili Yaani Uso Wa Hasira, Story Zote Kwenye Gari Zikakoma. Ilikuwa Ni Chuki Ya Wazi Kwa Yule Mama Ila Ikuwa Ni Chuki Ya Bure. Moyoni Mwangu Nikasikia "Upendo Wa Wengi Utapoa".Kwangu Ilikuwa Ni Ajabu Maana Zaidi Ya Watu Kumi Wamekwaza Na Kicheko Cha Yule Mama.
1 Timotheo 3:1-7 ''Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda MUNGU; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.   ''

  -Siku Ya BWANA I Karibu. Parapanda Italia Na BWANA YESU Atachukua Walio Wake, Watakaobaki Sehemu Yao Ni Katika Ziwa La Moto. Atakaowachukua BWANA YESU Sio Wale Wanaoitwa Wakristo Bali Wale Waliomtii KRISTO Hadi Mwisho. Kuwa Na Jina La Kikristo Tu Sio Tiketi Ya Mbinguni Bali Kumpokea YESU Kama BWANA Na Mkombozi Wako, Wokovu Ni Leo Wala Sio Kesho. Masaa Yanakimbia Na Siku Zinakimbia Mchakamchaka, Ndugu Usije Kuachwa Maana Unampangia MUNGU Siku Ya Kuokoka Kwamba Ni Hadi Ukamilishe Jambo Fulani. Kama Utapata Ufahamu Huu Leo Basi Hujachelewa Lakini Ukipata Ufahamu Huu Kesho Utakuwa Umechelewa Maana Inaweza Kuwa Hautakuwa Duniani Hiyo Kesho. Wanaondoka Duniani Ni Watu Kama Wewe Na Walikuwa Na Mipango Kama Yako Na Inawezekana Kabisa Walikuwa Na Mipango Mizuri Kuliko Hata Wewe Ila Wameondoka. Biblia Inasema "Tubuni Mrejee" 
Matendo 3:19  '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;'' 
-Ukijifanya Rafiki Wa Dunia Lazima Tu Utakuwa Adui Wa MUNGU. WOKOVU Ni Sasa Tena Sasa Hivi, Wafuate Wachungaji Wakusaidie. Ukiisikia Sauti Leo Basi Geuka Na BWANA YESU Atakupokea.
Warumi 8:12 ''Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.  ''

  -Huu Sio Wakati Wa Kumanchestalize, Kuliverpoolize Wala Kuarsenolize Bali Ni Wakati Wa WOKOVU. Kuna Watu Wamejaza Tu Mioyoni Mwao Soka Na Wanasoka Kuliko Kujaza Mioyoni Mwao Neno La MUNGU, Hao Nao Ni Pole Kwao Maana Neno La MUNGU Lingewafaa Kuliko Soka. Sikatai Kushabikia Mpira Ila Nakataa Mpira Kuchukua Hadi Nafasi Ya MUNGU Maishani Mwa Mtu. Masaa Unayotumia Kuangalia Mpira Na Kujadili Mpira Ungeyatumia Kwa Ajili Ya MUNGU Usingekuwa Hivyo Ulivyo. Mpe MUNGU Nafasi Ya Kwanza Na Sio Soka. Ya Dunia Yote Yatapita Lakini Neno La MUNGU Litadumu. Na Kama Hujaokoka Ndio Kabisa Hata Hujui Ufanyalo Hata Kama Unawajua Wanasoka Wote Na Wake Zao. Utafuteni Kwanza Ufalme Wa MUNGU Na Haki Yake, Na Hayo Mengine Mtazidishiwa
 
Mathayo 6:33 '' Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. '' 
-Mtafuteni BWANA Maadamu Anapatikana, Mtu Mwovu Na Aache Mawazo Yake Na Arejee Kwa BWANA Naye Atamsamehe Kabisa
Isaya 55:6-7 ''Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU. wetu, Naye atamsamehe 
kabisa. '' 
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
mabula1986@gmail.com
+255714252292.
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments