SIKU YA KUTOKA KATIKA NYUMBA YA UTUMWA

Utangulizi: Andiko la KUTOKA 20:2… [Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.]… Tukiyaangalia maisha yetu kama Wakristo na kama Watanzania, ni dalili tosha ya kwamba kuna mahali  hapajakaa sawa, kwa sababu hali ya utumwa inajidhihirisha.  Utumwa ni  hali ambayo, ukomo wa mtu unawekwa ili kwamba asiweze kufikia mahali fulani zaidi katika maisha. Yapo mengi yanayofanya mambo kutokwenda. Hata wale watu wenye kazi, matatizo bado yanaibuka ili  kwamba hata huo mshahara haufanyi lolote zaidi ya kutumika kugharamia matibabu ya magonjwa,  mahitaji mbalimbali, shida na taabu zinazotokea maishani baada ya kuupata mshahara.
NYUMBA YA UTUMWA
Siku ya kutoka kwenye hiyo nyumba ya utumwa ni leo. Farao wa Misri anafananishwa na shetani kwa maisha ya leo. Siyo kwamba mtu hapendi kuja kanisani, au  hataki kuomba, au hataki kuacha uvutaji sigara. Yote haya hayawezi kutokea hadi pale huu utumwa utakapoondolewa.


Haijalishi hiyo nyumba ya utumwa imewekwa na nani. Ni saa ya kuondoka katika  nyumba ya utumwa. Ni saa ya Tanzania kufunguliwa kutoka kwenye Nyumba ya Utumwa. Tanzania siyo maskini, wala watu wake siyo maskini. Shetani ameiweka nchi katika hali ya umaskini. Siyo mpango wa Mungu kuwa jinsi  ulivyo.wapo watu waliokuendea kwa waganga wa  kienyeji.unaweza kuwaangalia watuwa nyumbani/familia yako na kusema, hawa hawawezi  kuniendea kwa waganga wa  kienyeji kwa sababu ni watu wanaoenda kanissani.kwenda kanissani siyo  hoja, bali hoja ni mtu  kuwa na Yesu moyoni  mwake.
Ukiwa umefungiwa kwenye nyumba ya utumwa ujue kuwa yupo pia mwenye nyumba hiyo ya utumwa.  Maisha hayaanzii kwenye ulimwengu wa mwili, bali kwenye ulimwengu wa roho usioonekana. Haijalishi adui zako walikufunga lini au mwaka gani. Ni saa ya kutoka kwenye nyumba ya utumwa. Vipo  vifungo tofauti tofauti, kwa sababu vingine havifai hata kuwemlezea mtu. Shetani anawatumikisha watu.ndiyo maana wapo watu wanaitwa walevi, lakini binafsi hawapendi  kuwa walevi. Kile kifungo ndicho kinachomtumikisha mtu kuwa mlevi au kufanya jambo asilopenda kufanya. Unapoitwa  mtumwa, ni  sharti kufanya kadiri anavyotaka ufanye bwana wako. Shetani ana watu wake (mawakala) anaowatumia ili kuweka wengine magerezani.
Kila mahali waliponifunga nisioe au nisiolewe, walionizuia nisipate kazi,walionizuia nisiwe tajiri leo ni siku  ya kutoka kwa ushindi wa Jina la Yesu. Upo kama ulivyo lakini siyo kwa mpango wa Mungu. Wapo  watu  waliotengeneza huo ugumu  katika  maisha yako. Kila nyumba ya utumwa ina tofauti na nyingine kutokana na aina ya kafara iliyotolewa na adui yako. Yupo adui anayetoa kafara ya njiwa au kuku, na ikeshatolewa kwa mganga wakienyeji damu ya hawa ndege husababisha ufukuzwe kazi au ndoa yako isitulie. Wapo  wengine wanaotoa mbuzi au ngo’mbe au hata roho ya mtu. Aliyetoa kafara ya kuku au njiwa ni tofauti na aliyemtoa mtu / mwanane wa kuzaa. Mashetani waliopewa chakula (damu) kwa ajili hii, husimamia majukumu yao kwa umakini kuhakikisha kwamba kile walichoamuriwa kufanya kinafanyika barabara.
Yesu Kristo alitolewa kafara iliyo kuu kuliko zote na ndiyomaana inanyamazisha kafara zingine zote.  Imeandikwa YOHANA 3:16..[Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.]… Maana yake ni  kwamba,  Damu ya Yesu ambaye hakuwa na dhambi ina UWEZO kuliko damu zote za wanyama na wanadamu wenye dhambi waliotolewa kafara kwa ajili  yako.
Mafanikio ya mtu huanzia rohoni. Akiwepo Mbunge au  mtu yeyote mashuhuri na ambaye anaonekana amefanikiwa, ujue aidha amepata hayo mafanikio kutoka kwa Mungu aliy hai (Jehovah) au kwa Shetani.
KUOKA 6:9…[Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.]… Mtu  anapokuwa katika hali ya utumwa, hawezi kuelewa kitu chochote. Ugumu  wa maisha ya utumwa uliwafanya wana wa Israeli wasiweze  kumsikilisza Musa. Usiwe na huzuni, kwa sababu yupo Yesu Kristo awezaye kukuondoa katika huo utumwa. Hakuna jambo gumu asiloliweza Baba Mungu wa Mbinguni.
Imeandikwa “Kila pando  asilolipanda Baba wa Mbinguni litakwenda kung’olewa”.  Hizi ni kazi za shetani. Wote waliokaa na kuleta mapando yao ya kuonea watu lazima leo yakang’olewe kwa Jina la Yesu. Wote waliopanga mipango yao ili maisha yangu yasifanikiwe lazima wapigwe kwa Jina la Yesu.
Shetani ana sifa moja kubwa ya kujigeuza geuza. Imeandikwa katika LUKA 13:11….[Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.]…Huyu pepo wa udhaifu ndiye aliyepindisha huo mgongo. Huyu mama angeenda hospitalini angeonekana mgongo umepinda.shetani kwa hiyo anaweza kuingia ndani ya mwili wa mtu na kugeuka kuwa pepo la udhaifu,  aidha kwenye tumbo,mgongoni n.k. na kufanya tatizo lako liwe la kugeuka geuka. Ukienda hospitaliniwataliona tatizo lakini ukipewa dawa hauponi. Kila kitu kwa hiyo huanzia rohoni. Nampenda sana Yesu Kristo kwa sababu popote  alipopita akakutana na utumwa alikuwa anawaweka watu wale huru. Yesu Krsito amekuja hapa leo kuzikata kamba za utumwa kwa Jina la Yesu.

Saa ya Bwana kuyaangalia maisha yako na yangu imefika. Ni saa ya Bwana Yesu anayekaa ndani  yangu kushuka na kutembea na kuondoa kila utumwa mlionivisha. Kwa mateso  yale nimemfahamu Mungu wa kweli zaidi. Wote walionitesa ni saa ya Bwana kuwashughulikia. AYUBU 23:10….[ Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.]… Leo ni saa ya kuondoka kwenye lile jaribu tena kwa ushindi. Aliyesimama kinyume na wewe asikutishe kwa sababu walioko upande wako ni wengi kuliko hao maadui zako.

ISAYA 14:3....[Tena itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa;]… Ni saa ya Bwana kunisimamisha tena,ni saa ya Bwana nkunipa raha tena.kila  walichokipanga kwenye ndoa yangu au katika maisha, yangu imekwisha. Jemedari  wa kweli Yesu Kristo yupo ndani ya Nyumba hii leo kubadilisha mipango  yote ya maadui zako ili uwe na uzima tena uwe nao tele.
Huwezi kutoka utumwani kama bado hujampokea Yesu Kristo.kama hujaokoka ni vyema ufanye maamuzi  leo ili uweze kutoka kwenye hiyo Nyumba ya Utumwa.
                          © Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)

Mtaa wa Nguvu Kazi, (Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.

 /or

Contact our Senior Pastor:

 Dr. Godson Issa Zacharia

 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

Comments