USIKUBALI KUTAWALIWA NA DHAMBI.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU aliye hai milele.
Leo nataka ujue umuhimu wa kukataa kutawaliwa na dhambi.
Mwanzo 4:7 '' Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde ''
-Yakupasa dhambi kuishinda,  dhambi inakuotea lakini hakikisha unaishinda. ujumbe huu ni kwa kila mtu kujua na kutendea kazi hiki atakachikijua. 
-Maana ya dhambi ni uasi dhidi ya MUNGU.
Dhambi Na Shetani Ni Sawa. 
-Anayetenda Dhambi Ni Yule Ambaye Anamtii Shetani.
- Aliye Na Shetani Huyo Moja Kwa Moja Ni Mtenda Dhambi. -Anayetumikishwa Na Shetani Huyo Lazima Ni Mtenda Dhambi Tu.
- Wateule Hawatakiwi Kutawaliwa Na Dhambi
Warumi 6:14 '' Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema. ''
-Dhambi Ni baba Mzazi Wa Mauti Tangu Anguko La Adamu. -Dhambi Ni Uasi Dhidi Ya MUNGU. 
-Dhambi Inatakiwa Ikemewe Popote. 
-Dhambi Ndio Kizuizi Cha Uzima Wa Milele. 
Ili Uishinde Dhambi Maana Yake Mtii MUNGU. 
 Yakobo 4:7 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. ''

-Usipoamua Kumtii MUNGU Maana Yake Dhambi Imekuteka. -Usipomtii MUNGU Maana Yake Unamtii Shetani. 
Biblia Inakushauri Umtii MUNGU Huku Ukimpinga Shetani
Kama Hutampokea YESU Na Kutubu Maana Yake Dhambi Zako Hazitafutwa Hata Kama Umezifanya Miaka 55 Iliyopita. Hata Kama Dhambi Umeifanya Miaka 20 Iliyopita Kama Hujatubu Maana Yake Hiyo Dhambi Iko Na Inaweza Kukukosesha Uzima Wa Milele. Unapompokea YESU Na Kutubu Maana Yake Dhambi Zako Zote Zinafutwa Na Unakuwa Mtakatifu Mbele Za MUNGU Hata Kama Ulifanya Dhambi Kubwa Kiasi Gani. Saa Ya Kutubu Ni Sasa. ''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote-1 Yohana 1:9''

 =Mshahara Wa Dhambi Ni Mauti
Warumi 6:23'' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.   ''. 
-Mshahara Wa Dhambi Ni Mauti, Ni Kuzimu, Ni Jehanamu. Huo Ndio Mshahara Wa Dhambi Lakini Andiko Hilo Hilo Linasema Zawadi Au Karama Ya MUNGU Ni Uzima Wa Milele Katika YESU KRISTO BWANA Wetu. Ndio Maana Biblia Anatushauri Kwamba "Msiache Dhambi Itawale Miili Yenu, Hata Mkaiitii Katika Tamaa Zake- Warumi 6:12"
-Dhambi Haitakiwi Kukutawala, Ukitawaliwa Na Dhambi Maana Yake Unaelekea Kubaya Sana. 
-Wengi Hawataki Kuonywa Ila Wanapenda Tu Kufarijiwa. Ndugu Yangu, Anayekupenda Zaidi Ni Yule Anayekuonya Ili Usiondoke Katika Ukweli Uliopo. Biblia Hapo Juu Imesema Kwamba Dhambi Ina Mshahara Na Mshahara Huo Ni Mauti. Ndugu Yangu Kwanini Ukatae Maonyo Ambayo Ukiyatii Huwezi Kulipwa Mshahara Uitwao Mateso. Hakuna Anayetaka Kulipwa Mshahara Asioupenda. Mshahara Wa Dhambi Ni Mauti Au Mateso Ya Milele. Ndugu Ikatae Dhambi, Iogope Dhambi, Ikimbie Dhambi Na Usifanye Dhambi. BWANA YESU Anakuita Leo Kwenye Uzima Wa Milele, Ni Jukumu Lako Tu Kumpokea Na Kuanza Kuishi Maisha Matakatifu.
 Zaburi 62:8 ''Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; MUNGU ndiye kimbilio letu.''
-MUNGU ndiye kimbilio la uzima wa milele.


 -Hatutakiwi Kumuogopa Shetani , Tunatakiwa Tujue Kwamba Shetani Alishashindwa Na BWANA YESU. 
BWANA YESU Alimshinda Shetani Kwa Ajili Yako Na Yangu
Warumi 16:20 '' Naye MUNGU wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya BWANA wetu YESU KRISTO na iwe pamoja nanyi. [Amina.]   '' 
 -Kazi yetu  Ni Kumpinga tu Shetani Na Yeye Atakimbia. Biblia inasema
Yakobo 4:7-8 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. ''.
- Sio Kwamba Tukimpinga Shetani Atajaribu Kukimbia Bali Atakimbia. Ukiona Hajakimbia Maana Yake Hujampinga. Tatizo Kubwa Ni Kwamba Wakristo Wengi Ni Watakatifu Kwa Baadhi tu Ya Vitu Lakini Kwenye Maisha Yao Ya Wokovu Kuna Vitu Kiuhalisia Wanavikumbatia Huku Vitu Hivyo Shetani Yuko Ndani Yake. Maana Yake Hawa Wanamkumbatia Shetani Wakati Wanatakiwa Wamkemee Na Kujitenga Na Vitu Hivyo. 
Ndugu Mpinge shetani na vitu vyake vyote. wewe ni mteule na unatakiwa uishi maisha matakatifu tu siku zote.
 -Tunaitwa Wateule Wa KRISTO Kwa Sababu Tuna ROHO MTAKATIFU. ROHO MTAKATIFU Akikuacha Hautakuwa Na Tofauti Yeyote Na Wachawi, Walevi Na Makahaba. 
Ni Hatari Sana Kuachwa Na ROHO MTAKATIFU. 
Na ROHO Ataondoka Kwako Kama Ukikataa Kuongozwa Nae Au Kama Ukitenda Dhambi.
Hapo najua kabisa umeona madhara ya dhambi yalivyo, lakini BWANA anasema ni lazima tuishinde dhambi.
Hakikisha unakuwa kanisa lenye ushindi siku zote maana hutaendeshwa na dhambi na wala hutaacha kumtii ROHO MTAKATIFU.

 BWANA YESU Alisema Kuwa Milango Ya Kuzimu Haitalishinda Kanisa
Mathayo 16:18 ''Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.''.  
-Lakini Kumbuka Kwamba Kanisa Sio Jengo, Kanisa Sio Dhehebu, Kanisa Sio Taasisi. 
-Kanisa Ni Wewe Na Mimi Tuliookolewe Na BWANA YESU. -Milango Ya Kuzimu Haitakushinda Wewe Na Mimi.
- Shetani Hana Utawala Juu Ya Kanisa. Mpinge Kwa Maombi Hakika Atakimbia. 
-Mwite BWANA YESU Utashinda. 
-Wewe Ni Kanisa Na Kanisa Ni Mshindi Daima
-Kama kanisa la MUNGU hakikisha hutawaliwi na dhambi yeyote. kama kuna dhambi inakutesa hakikisha unaomba na hata kufunga na kuomba, pia unaweza kumwambia mchungaji wako ili akusaidie na kukuombea. kuna watu husema kwamba wanatamani kuacha uzinzi lakini wanashindwa kumbe tatizo kuu ni mazingira na tabia mbaya ya kuangalia picha au filamu za ngono. ndio maana nimesema kwamba ukiteswa sana na dhambi hakikisha unamuona mchungaji wako ili akusaidie, hakuna dhambi ambayo haiwezekani kuiacha. dhambi ni mbaya na haitakiwi dhambi ikutawale, ishinde dhambi kwa kutubu na kuacha dhambi hiyo.

''Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu-Mithali 16:5''.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments