WATOTO WACHANGA MNAOKULIA WOKOVU MSIOGOPE VITISHO/CHUKI TOKA KWA FAMILIA AU JAMII


Na Moses Chapa.
Mmechaguliwa toka misingi ya ulimwengu muulithi uzima wa milele,nanyi mlipendwa nanyi mkakubali upendo wa Kristo kufa kwa ajili yenu basi mmechagua fungu jema,na wale ambao bado hawajaokoka na wamekataa kuokoka wamebakia ktk kuchagua fungu baya ndo maana hawakupendi wewe uliyepata kibali cha kupendwa,wewe umekuwa kipenzi cha baba kwani wote waliompokea wamepewa uwezo kuwa watoto wa Mungu.Basi wewe umefanyika mtoto wa Mungu hao wasiopata kibali hicho watakuchukia,chuki inakuwa kubwa si kwa ndugu,marafiki na jamii pia,watakuita kila aina jina la zihaka ili kukutoa ktk njia ya kuendea mafanikio yako..Wakati ulipokuwa gizani pamoja nao walikuwa wanakupenda ila ulipotoka kuja nuruni wanakasirika kwakuwa adui anajua unaenda kufanikiwa hvy anapandikiza chuki ndani yao.Mungu wetu anawapenda wale wampendao ili awaonyeshe wema wake,sasa sisi tunapendwa na baba yetu tunapata chuki kwa wenzetu kwanin tunapendwa kuliko wao.Kwan ukianza kuonyeshwa upendo na mzazi wenzio watakukasirikia.Maana upendo wa Mungu kwetu unaenda kutuandalia meza tukila mbele yao,adui hapendi kutuona tunafanikiwa tukiandaliwa meza mbele yake,hata Daudi wakati anaandaliwa meza na Mungu ndipo Sauli akaanza kumchukia.kwani Upendo wa Mungu kumchagua Daudi kuwa mfalme kulileta matatizo kwake,Sauli alimchukia sana.
Unapookoka nawe umechaguliwa kuwa mfalme na kuhani ktk dunia hii,utavilithi ulivyotakiwa upewe maana wewe kipenzi cha Mungu basi atakupa thawabu.Usiogope chuki nayokujia sababu ya wokovu wako Daudi ktk safari yake ya kumuua Goliath akaanza kupata umaarufu watu walimsifia,na hapo Sauli akaanza kumchukia 1SAMWELI 18:8 Basi Sauli akaghadhibika sana na maneno haya yakamchukiza,akasema wamempa Daudi makumi elfu na mim wamenipa elfu tu.Kuna nin tena awezayo kupata isipokuwa ufalme!.Sauli aliingiwa na wivu kuona anapendwa,wewe nawe unapendwa na Mungu adui anaingiwa na wivu akitaka kukuzimisha.Wakati watu wanakuchukia usiofu ujue unapendwa nao wamejua.
..Mungu alikuwa anampenda sana Daudi,Sauli akaingiwa na wasiwasi kuona Upendo ule utakuja kumketisha katika kiti cha ufalme,naye atachukua nafasi yake,hivyo akamchukia sana akitaka kummaliza..Lakini katika chuki ile Daudi hakuteteleka kiimani ndo kwanza alizidi kumtegemea Mungu,chuki ile iliimarisha imani ya Daudi...Na katika chuki zote alizozipata Daudi hakuonyesha kulipiza kisasi kwa Sauli alingoja haki ya Mungu mtetee ije kumlipizia kisasi juu ya Yule anayemchukia..Chuki kitu kibaya sana,adui anaitumia kama siraha yake ili kukukatisha tamaa usifikie malengo yako,Daudi alichunga moyo wake usiingiwe na chuki..Siku zote usilipize ubaya kwa ubaya,bali ubaya kwa wema,kwani Daudi katika kutendewa mabaya na Sauli hakuingiza chuki ndani ya moyo wake alijua wivu wa Sauli tu kuona yeye ameachwa na Mungu na Daudi amependwa na Mungu...Daudi alirudisha wema kwa Sauli,KWANI ALIKUWA NA ROHO WA MUNGU hivyo alikuwa na moyo wa ajabu kwani aliushinda ubaya kwa wema,alikuwa mtu mwema hata kwa adui yake.Ingawa Sauli alimchukia kwa miaka 15 akiitafuta roho yake naye akikimbia nyikani,lakini akatafuta kulipiza wema. Biblia inasema katika
2SAMWELI 9:3
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.

Basi siku zote unapofanikiwa vita inaibuka juu yako kwakuwa ni wivu wa adui tu kuona unaenda kuchukua nafasi yake atawatumia watu kukuzuia..
Mambo ya chuki yapo katika Familia,makazini,mashuleni katika jamii watakuchukia kwakuwa tu ni wa tofauti na wao,wewe upo nuruni wao wapo gizani,wewe umepata na wao wamekosa..Ni wivu wa kuona utakuwa juu yao...Usirudishe ubaya wanaokufanyia siku moja Mungu wako atakulipizia...
MBARIKIWE...

Comments