SAFARI NJEMA SHUJAA APOSTLE JOHN KOMANYA.

Apostle John Komanya enzi za uhai wake.
Siku ya Jumapili hii imekua ya majonzi kwa ndugu jamaa ,marafiki familia na waumini wa Mtume na nabii John Komanywa ambaye alifariki asubuhi ya siku hiyo akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikua akitibiwa matatizo ya kiafya yaliyokua yakimsumbua.
Chanzo kilichopelekea umauti wake kwa mujibu wa dada wa marehemu ameelezea kwamba Apostle Komanywa alipatwa na tatizo la mishipa inayopeleka Oksijeni kwenye Ubongo kushindwa kufanya kazi ghafla na hivyo mwili mzima ukajikuta umeishiwa nguvu na kuanguka ambapo baadae alikimbizwa Hospitali na baada ya vipimo madaktari walieleza kua mishipa hiyo ilifeli ghafla lakini pia kulikua na tatizo la Kisukari ambalo lilikua limeshakua kubwa.
Wimbo bora kabisa ulioimbwa na Apostle Komanya ni huu.

Mwili wa apostle Komanya utazikwa kesho jumatano .

Tazama Video inayomuonesha Dada wa marehemu akielezea kwa urefu zaidi kuhusu chanzo cha umauti huo na mipango ya mazishi

Comments