SIRI PEKEE YA MAOMBI YAKO NI HII.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuijua kweli kutakufanya ushinde, ndio maana ujumbe huu umekuja kwako leo ili ujue jinsi ya kushinda na ushinde.

'' Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;-Waefeso 3-20'' 

Yawezekana Ulimuomba MUNGU BABA Akufanyie 1,2,3 Lakini MUNGU Akafanya 4,5,6. 
Jambo La muhimu Kujua Ni Kwamba Sio Lazima MUNGU Akupe Kama Ulivyoomba Ila MUNGU Siku Zote Hukupa Lile Lililo Jema Zaidi Na Sahihi Kwako Kwa Wakati Huo. 
MUNGU inawezekana asikupe ulichoomba ila akakupa unachostahili. kinachostahili ni muhimu zaidi kwako kuliko ulichoomba maana kinachostahili mara nyingi huwa ni kikubwa na cha muhimu zaidi ya kile ulichoomba.

''Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa, Asiyadharau maombi yao-Zaburi 102:17''. 

Usiache Hata Siku Moja Kuomba Bali Pokea Akupacho MUNGU Hata Kama Hukukiomba Kwa Wakati Huo. Ngoja Nikupe Mfano. Binti Mcharuko Ambaye Anafunga Na Kuomba Ili BWANA Ampe Mme Mwema. MUNGU Anaweza Kumjibu Kwa Kutengeneza Kwanza Moyo Wake Huyo Binti Ili Aache Dhambi Ndipo Atapewa Mme Mwema Hayo Ndio Majibu Ya Kuomba 1,2,3 Harafu Majibu Yakaja 4,5,6. Haiwezekani wewe ni Mzinzi na  Uombe Kupewa Mke/mme Mwema Wakati Wewe Ni Mzinzi. 
je itawezekana vipi?

 1 Yohana 5:14 ''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.''

Biblia Inasema "Tukiomba Sawasawa Na Mapenzi Yake Atatusikia". Je Ulishawahi Kujiuliza "Kama Tukiomba Sawasawa Na Mapenzi Yake Atusikia Je? Tukiomba Nje Na Mapenzi Yake Inakuaje".
Je umeomba nje ya mapenzi/Matakwa ya MUNGU mara ngapi?
 Kaufunuo haka Kagumu Ila Tafuna Hivyo Hivyo Ili Upone, Dawa Zingine Chungu Ila Ukimeza Unapona.
Kuna watu hulaumu kwamba hawajajibiwa mahitaji yao waliyoomba na kufunga,  kumbe wao ndio wanatakiwa walaumiwe kwanini waliomba vibaya au kwanini waliomba kwa tamaa au kwanini waliomba ili wawakomeshe akina fulani ambao waliachana nao zamani.
 Yakobo 4:2-4 ''  Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU. ''
 Hatuombi tu na kupokea bali tunatakiwa tuombe sawasawa na mapenzi ya MUNGU ndipo tutapokea.
Kuyajua mapenzi au matakwa ya MUNGU ndio mtihani kwa walio wengi lakini napenda nikuambie kwamba ROHO MTAKATIFU ndiye wa muhimu wa kwanza kwa kila mwanamaombi, maana ROHO yeye ndiye anajua tuombe vipi na kupokea. asilimia kubwa ya waombaji ni wale ambao wanaongozwa tu na tamaa kuomba na sio wale wanaoomba kwa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.

Warumi 8:26-27 ''Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya ROHO ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo MUNGU''.

 Kuna Njia Nyingi Tunaweza Kumkaribia MUNGU Wetu. 
Hapa Nataka Tujifunze Aina 3 Za Maombi. 

     1.   MAOMBI YA KUTAFAKARI. 
Maombi Haya Unaweza Kuyaomba Kwa Njia Ya Kutafakari Mfano Kuna Mpendwa Wako Yuko Mbali Na Wewe, Unakuwa Ukitafakari. Unakua Ukifikiria Kupona Kwake, Unafikiria Jinsi Mtakavyoonana Baada Ya Yeye Kupona. Hayo Ni Maombi Ya Kutafakari Wakati Unayemtafakari Unajua Kabisa Yuko Hoi Sana Lakini Tafakari Yako Inakuwa Inatamka Uzima. 

   2.  MAOMBI KUPITIA VITABU VYA MAOMBI VILIVYO NDANI YA BIBLIA. 
Ni Maombi Kupitia maandiko ya Biblia, Mfano Zaburi N.K. Kwenye Zaburi Kuna Sehemu Nyingi Za Maombi. Unaweza Pia Ukatumia Maombi Ya Hana Katika Samweli Wa Kwanza. Unaweza Ukaomba Ukitumia Maandiko Kama Hayo. Unaweza Ukasoma Maombi Hayo Ya Kwenye Biblia Huku Ukijiunganisha Na Neno Hilo La MUNGU Kujiombea Mwenyewe Maana Vitabu Vya Biblia Vimevuviwa Na ROHO MTAKATIFU. 

   3.   MAOMBI YALIYOELEKEZWA. 
Maombi Haya Yanaweza Kuandaliwa Na Mtu Mmoja Na Wengine Wakayarudia Au Kiongozi Anaweza  kuandaa na wengine wakaomba wakiyatumia lakini pia katika maombi yeyote ukimruhusu ROHO MTAKATIFU kukuongoza lazima tu atakuongezea vitu ambavyo ndiovyo sahihi zaidi kwako kuviomba kwa MUNGU na hivyo ukiviomba hakika ushindi ni lazima kwako.
Maadui ni wengi na siku zote unahitaji msaada wa MUNGU lakini pia  unaweza ukaomba sana lakini imani kikawa ndio kikwazo kwako. kumbuka kipimo cha imani yako kukua kina MUNGU hivyo jifunze neno la kuomba na wengine ili kuimarisha imani yako. kumbuka kwamba dhambi hukufanya usijiamini na kukupoteza kabisa kutoka kwenye kusudi la MUNGU.
Lazima uwe mtu wa imani na muombaji makini haijalishi umepitia katika jaribu au uhitaji gani.

 Vitisho Vya Adui Zako Ni Dalili Ya Kwamba Umewashinda Kiroho Na Sasa Wamebaki Na Kukutisha Tu Ili Ujichanganye. 
 Lakini waombaji wengi hukwama kwenye eneo hili la vitisho vya adui.
Ndugu Yangu, Endelea Na Maombi Na Ushindi Kwako Ni Lazima Kwa Jina La YESU KRISTO. Wewe Ni Shujaa Omba Tu, Mfano katika maombi yako ya leo Tumia  Zaburi 34:17, Isaya 54:15 Na Mithali 30:5.  Kesho unaweza kuomba ukitumia maandiko mengine pia na siku inayofuata unaweza kutumia tena mengine.
BWANA YESU Ameachilia Ushindi Wa Ajabu  Kupitia Jina Lake. Una Heri Wewe Maana Utashinda Kwa Kishindo.
Natamani sana niendelea kukupa vitu vya kukusaidia ila kwa leo tafakari sana ujumbe huu na itakusaidia.

Waefeso 6:18 ''Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika ROHO, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;'' 

 -Ndugu,Naamini umejifunza na utachukua hatua
njema ya kumpokea BWANA YESU kama
hujaokoka ili awe BWANA na MWOKOZI wako
tangu leo na utaanza kuishi maisha matakatifu


KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO
HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO
UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA
MATAKATIFU.



''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele
zako mimi mwenye dhambi, lakini leo
nimetambua kosa langu na naomba unisamehe
dhambi zangu zote, nisamehe dhambi
ninazozikumbuka na pia zile ambazo
sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu cha
hukumu na uliandike jina langu katika kitabu
cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10
Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa
sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya
kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka.
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata
haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu
'' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na
hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na
hakika nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga
ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa
matendo mema na matakatifu. BWANA nipe
ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda
dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo
mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU
mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila
roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa
jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU
linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza
mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana
kwa kuniokoa. Yote haya kwa imani nimepokea
na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU
kunitumia. Katika jina la YESU KRISTO
nimeomba na kupokea .
Amen.''
Kama umetubu toba ya kweli hakika wewe
kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa. Kwa sasa
naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza
tena siku nyingine. ulishindwa kumpokea
BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa
kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima
na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho
kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende
uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU
akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments