KUWA SINGO SIO UGONJWA.

 
Askofu Mkuu Dr Josephat Gwajima.

Tatizo la watu wengi duniani ni mahusihano. Watu wengi wanafikiri kuwa single ni kuwa nusu kipande kinachotakiwa kipate kipande cha kuunganisha na mtu anapokuwa single kwamaana hajaoa au hajaolewa ni mtu kipande lakini Mungu hashadadii sana kuwa single. kuwa single sio kuwa na ugonjwa,
Mtu wa kwanza kuumba alikuwa single.
TALAKA.
Talaka au kupewa tralaka ndio janga kubwa kuliko kitu chochote kwenye mahusihano, talaka ni mauti ya mahusihano, talaka ni mbaya kuliko kifo cha kufariki. Ni rahisi sana kushughulikia kifo cha kawaida kuliko kifo cha talaka, talaka ni mbaya sana kwasababu yule mliyepeana talaka unaweza kuonana naye mahali popote iwe ni sokoni, benki, kwenye daladala, kanisani, njiani n.k na kila mkionana lazima uingiwe na hasira kutokana na kukumbuka mambo aliyokufanyia kipindi kile hamjaachana mpaka mkafikia kupeana talaka.

Mungu hajasema anachukia kifo lakini amesema anachukia talaka. Afadhali kukaa peke yako kuliko kuwa na mtu na kuja kupeana talaka baadaye. Vijana wengi siku hizi wanaona kuoana ni vizuri hivyo wakiwa bado hawajaolewa au kuowa wanakuwa hawana amani na kushindwa kujiendeleza kimaendeleo sababu ya kuwazia talaka.
Kama hujaoa au hujaolewa acha kwanza ujiendeleze kielimu, biashara au kikazi na kama ni mjane tulia kwanza mpaka utakapompata anayekufaa na unamfahamu fika. Fikiria mtu ulikuwa unaamka naye na kula naye halafu baadaye unakuja kuachana naye, inauma sana.
Kama uko kwenye ndoa ile shela uliyovaa au suti siku ya harusi ilimaanisha ulikuwa unaingia kwenye matatizo na maumivu makubwa sana ya kupata talaka. Watu wengi wanafikiri kuoa ni suluhisho la upweke walio nao au ni suluhisho la matatizo walio nayo. Ukioa matatizo ndio yanaongezeka. Ni waliondani ya ndoa tu ndio waliokuwa na wasiwasi wa talaka. Siku ukioa unakuwa mtahiniwa wa talaka kama usipofanya vizuri.
Ulipokuwa single hakuna mtu aliyekuwa anajua hujui kupika, unakula chips na kulala, hakuna mtu aliyekuwa anajua wewe sio msafi lakini ukioa yule unayempata unaanza kujianika kwake, hakuna mtu aliyekuwa anajua unarundika nguo chafu na baadaye unazitupa na kuzichoma, hakuna mtu aliyekuwa anajua huwa unagombana ukiamka asubuhi, hakuna mtu aliyekuwa anajua ukikasirika uhuwa huongei na mtu wiki nzima unanuna ingawa wewe ni mwanaume, hakuna mtu aliyekuwa anajua hupigi mswaki lakini ukioa/olewa utakuwa unaambiwa darling safisha usafi wa sebule, hakuna mtu aliyekuwa anajua huwa unakoroma usiku lakini kunamtu atajua huwa unakoroma usiku. Kimsingi kuolewa/ kuoa ni kwenda kujianika uasilia wako kwa mtu mwingine na yeye atakuvumilia kwa mambo hayo.
Kwenye vitu vya muhimu hapa duniani cha kwanza ni wokovu na cha pili ni kuolewa/kuoa. Ukioa/olewa hutasema nipishe nivae, hutasema kaka unafanya nini huku chumbani au usinisogelee na mambo mengine kama hayo.
Kama mtu angekuwa ana uwezo wa kujichumbia kwa tabia uliyo nayo je ungejioa?
Ukiwa single unaweza kupeta na kulala popote utakapo
NDOA.
Yesu naye aliongea kwa habari ya talaka. Ndoa inaitwa ni kile kitu alichokiunganisha Mungu.

"Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani. Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko. Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini." Mathayo 19:1-12
Kilicho washtua wanafunzi wa Yesu ni kwamba ukishaingia kwenye ndoa hakuna kuachana mpaka mwenzako azini afanye uasherati. Mtu wa kwanza kwenye Biblia alikuwa Adamu na alikuwa single.
Jambo linalowapoteza watu wengi ni matarajio ya jinsi mtu anavyoonekana kabla hujamwoa/olewa na wakishaingia kwenye ndoa wanajikuta wanaishia kusema “sikujua kama ulikuwa na kiburi namna hii”, “sikujua ulikuwa na tabia hii”, “nimekumbuka maneno ya marehemu Baba alivyonikataza kuhusu wewe” n.k. Mwanaume au mwanamke unayetafuta mambo mazuri sana ili umwoe/olewe naye kwa taarifa yako unayemtafuta hutampata na hayupo hapa duniani isipokuwa Mungu huruhusu uoleewe/owe na mtu anayekufaa ili umtengeneze unavyotaka awe. Ukioa usitegeme utavipata vile vitu unavyoviona kwa nje kabla hujamwoa ni kama mashariki iliyo mbali na magharibi, utashangaa vile ulivyovikataa kwa wengine kwamba sio vizuri utashangaa anavyo na muda wakati huohuo kilichuunganishwa na Bwana mwanadamu asikitenganishe.
Ndoia ni taasisi na unaposema umefunga ndoa maana yake mmeingia wawili halafu Mungu akawafungia humo ndani akatupa funguo. Kuwa single ni msingi wa utu wa mtu ulioanzia kwa Adamu. Hauoi au hauolewi ili ukamilike. Kuwaza kwamba uolewe ili Baraka zije huo udanganyifu wa dunia hii, sio lazima uoe ili utimize ndoto za maisha yako mfano mzuri ni Yesu Kristo hakuowa na alitimiza lengo lake hapa duniani akiwa single.
Unaweza ukakosea vyote kwenye maisha yako lakini kowa/olewa ndio mwisho, swala la kuoa ni swala la pili kwa umuhimu ukioondoa swala la kuokolewa, unatakiwa uolewe na mtu wa aina yako (akiwa ndani ya wokovu).

JINSIA
Kuna tofauti ya kuwa na jinsia ya kiume na kuwa mwanaume. Mwanume ni majukumu, ni kazi, ni kufanikiwa na ni kiongozi. Mwanaume asiyefanya hayo huyo sio mwanaume isipokuwa ana jinsia ya kiume. Watu wengi wanafikiri kinachofanya ndoa iwe imara ni upendo, kumkiss mpenzio,kumfulia nguo lakini hicho sicho kinachofanya ndoa idumu na iwe imara, kule kuitana darling, sweat heart haiimanishi kutafanya ndoa iwe imara bali kuwa na maarifa ya kumjua na kumfahamu uliye naye ndicho kitakachofanya ndoa iwe imara na idumu.

"Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu." Mwanzo2:21 - 22
Biblia inasema kutoka kwa Adamu Mungu akamtengeneza mwanamke. Kuna tofauti kati ya mwanaume na mwanamke. Mwanaume ameumbwa kama mfano wa tofali lilo fyatuliwa lakini mwanamke amejengwa kupitia tofali hilo. Ukiwa kama Mwanaume unatakiwa ufahamu kwamba wanawake wameumbwa na Bwana kwa staili yao ili unawajali na kuwapenda si kwasabu ni wadhaifu la, bali ni jukumu lako mbele za Mungu kama Mwanaume.
"Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Mwanzo2:7, 15
Mtu wa kwanza ni alikuwa single na alitoka mavumbini. Watu wote duniani mtu aliyetoka mavumbini ni mmoja tu. Eden maana yake kwa kiebrania ni malango ya mbinguni, ni uwepo wa mbinguni, ni pamoja naye. Mungu alipomuumba single wa kwanza alimweka pamoja naye. Adamu hakuwahi kuimba wala kuomba sababu alikuwa mbele za uwepo wa Mungu tayari. Mwanadamu wa kwanza alikuwa anakaa pamoja na Mungu na alikuwa Mwanaume. Hitaji la kwanza la mtu ambaye ni single ni uwepo wa Mungu, Mungu alimuumba mwanaume single akampa maelekezo.
Ukiwa mwanaume single unatakiwa kukaa kwenye uwepo wa Mungu na chapili kufanya kazi. Binti mtu akija kukuoa muulize yupo na Mungu cha pili ana kazi? Kazi ya tatu ya mwanaume ni kutunza, Binti mwanaume akikufuata kukuchumbia kama ana Mungu na kazi kitu kingine muulize ana uwezo wa kutunza? Kabla haujaingia naye kwenye ndoa.
Single wa kwanza kwa wanadamu tumeona alikuwa na Mungu, pili alikuwa anafanya kazi, tatu alikuwa anatunza na alikuwa na mipango. Mungu tangu alipoanza uzao wa mwanadamu alianza na single na kutoka kwenye single eva akatokea, mtu asikudanganye kwamba huwezi kuzalisha ukiwa single huo ni upotofu bali unaweza kuzalisha ukiwa single bila shida yeyote, mabinti msidanganyike kwamba ukiolewa utavikuta kule kule kwenye ndoa, Soma shule, Jenga nyumba, Safari, jiendeleze usije ukakutana na manyanyaso kwenye ndoa utakapoolewa na kuumizwa bure.
Enyi mabinti mnapotaka kuolewa kwanza muulize mwanaume kama yupo kwenye uwepo wa Mungu, cha pili muulize ana kazi/biashara, cha tatu muulize utanitunza, unaweza kuniendeleza unaweza kunitunza muulize hayo maswali baada ya kumfahamu fika.
Mara nyingi watu wanapokuwa ndani ya ndoa hali ya rohoni inatofautiana kati ya mtu mmoja na mtu mwingine. Watu wanapooana yule wa juu kiroho anaweza kushuka chini sana au yule wa chini anaweza kupanda juu na kwenda pamoja na aliye juu kiroho. Watu baada ya kuwa wameoana utaweza kuona maendeleo yao. Kama wakirudi nyuma hakuna namna nyingine ya kuwatenganisha ndio imeshatokea wameoana wapo ndani ya ndoa na kilichounganishwa na Bwana mwanadamu asikitenganishe.
Hakuna kitu kizuri kwenye ndoa kama kuo na mwanamke anayekusikiliza au mwanaume anayekusikiliza ukipata hivyo mshike usimwache. Mtu unayeoana naye haitajalisha utakuwa nani baadaye, utalia au utacheka, utakuwa na huzuni au utafurahia.
Neno moja ambalo ni zuri kulishika ni kumwoa mtu unayemwelewa, mwanamke ni msaidizi wa mwanaume, Mungu amempa mwanaume kusudi la Baba wa familia ili atumie kusudi alilonalo, maono aliyo nayo kuendesha familia na mwanamke awe msaidizi wake kwenye kutimiza kusudi hilo, kuna wanaume wenye jinsia ya kiume ambao hawana maono au kitu cha kufanya kazi yao ni kukaa nyumbani kuangalia video, kutembea na kukaa vijiweni, unaweza ukamkuta mwanamke kwenye ndoa anashindwa cha kumsaidia mwanaume sababu Mumewe hana maono ya kuendesha familia, yupo mtupo na huyo mwamka unakuta anachukua jukumu la mumewe anaanza kutafuta huku na huko ili familia iendelee na Mwanaume wa aina hiyo huyo siyo mwanaume bali ni mtu mwenye jinsia ya kiume sababu hajatimiza vigezo vya kuitwa mwanaume kama Adamu. Kama mwanaume uwe unatakiwa uwe na maono ya kujenga na kuendeleza familia yako.
"Singleness is not a disease"

Comments