JE UNAPANDA NINI SASA?


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
Huu Ni Wakati Wa Kupanda, Wakati Wa Mavuno Ni Baada Ya Kufa. 
Ndugu Wewe Unapanda Nini Sasa?
 Biblia Inasema Kuhusu Wapandaji(wanadamu) Wote
 "Maana Yeye Apandaye Kwa Mwili, Katika Mwili Wake Atavuna Uharibifu; Bali Yeye Apandae Kwa ROHO , Katika ROHO Atavuna Uzima Wa Milele-Wagalatia 6:8"
-Je wewe unapanda kwa mwili au kwa Roho?
-Kupanda kwa mwili kuna mavuno yake ambayo ni uharibifu.
-Kupanda kwa Roho kuna mavuno yake ambayo ni uzima wa milele.
Kupanda kwa Roho ni kumpokea YESU KRISTO kama MWOKOZI wako binafsi kisha ukaanza kuishi maisha matakatifu yanayoongozwa na ROHO wa MUNGU.

Ndugu Je Wewe Unapanda Nini?
- Wanaopanda Dhambi Kwa Kufanya Watavuna Uharibifu. -Wanaopanda Maisha Ya Wokovu Kwa Kuyaishi Watavuna Uzima Wa Milele. 

Ndugu, Je Unapanda Kwa Mwili Au Kwa ROHO? 
-Wanaopanda Kwa Mwili Watavuna Uharibu Lakini Wanaopanda Kwa ROHO Katika ROHO Watavuna Uzima Wa Milele. 
-Hakuna Anayeweza Kupanda Karanga Akavuna Mahindi, Kila Mtu Atavuna Kile Alichopanda Wakati Akiwa Duniani. 

BWANA YESU Atamlipa Kila Mtu Sawasawa Na Alichopanda.
Ufunuo 22:11-13 ''Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.''. 

Ndugu Panda Kitu Sahihi.
- Panda Matendo Mema Na Kuishi Maisha Ya Wokovu Maana Utavuna Uzima Wa Milele. 
BWANA YESU Anakuita Leo Ili Uamue Vyema.
Ufunuo 3:20 ''  Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. '' 

Ndugu Kama Hujaokoka Nakuomba Mpokee YESU Leo Na Hakika Utakuwa Wa Uzimani.
Matendo 4:12 '' Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ''
-Wokovu ni kwa BWANA YESU tu.
-Uzima wa milele ni kupitia BWANA YESU tu.
-Ndugu naomba ujue kwamba BWANA Wetu Yu Karibu.

Ukitenda Mema Ni Kwa Faida Yako Na Ukitenda Mabaya Ni Kwa Hasara Yako. 
 Mema Kwa Faida Yako Ni Kuishi Maisha Matakatifu Ya Wokovu. Na Mabaya Ni Kumkataa YESU na Wokovu wake.
Obadia 1:15 ''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.''

Ndugu yangu, neema ya wewe kuokoka bado ipo.  BWANA YESU Aliamua Kuwa Ndugu Yetu Ili Kutusaidia, Angependa Kubaki Na Mamlaka Yake Kuu Mbinguni Lakini Alituhurumia Wanadamu Na Kuja Kutuokoa. 
YESU Alikuwa Na Uwezo Wa Kuwaangamiza Wanadamu Wote Na Kisha Kuumba Wengine Watakaomtii Lakini Kwa Neema Yake Alipenda Tu Kuchukuliana Nasi Sisi Wadhambi Ili Atusaidie. 

Ndugu Unayemkataa YESU Leo Tambua Kwamba Unakataa Uzima Wa Milele, Hakuna Uzima Wa Milele Nje Na YESU
Yohana 14:6-7 '' Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. ''
-Kumwona YESU ni kumwona MUNGU mwenye nguvu.
-Kumpokea YESU ni kumpokea MUNGU aliyeumba mbingu na nchi.
-Kukubali kuokolewa na BWANA YESU ni kuuchagua uzima wa milele ambao hakuna atakayekuondolea kama tu ukishi maisha matakatifu baada ya kuokoka.

YESU Ni Zaidi Ya Malaika Na Viumbe Wote, Lakini Alijishusha Na Kuwa Kama Mwanadamu Wa Kawaida Ili Kutuokoa. 
Alikuja Ili Tu Mimi Na Wewe Tukimpokea Na Kutubu Dhambi Zetu Zitaondoka Kwetu Na Kwenda Msalabani Golgotha Huku Sisi Tukibaki Huru. 
Ndugu Zangu, Duniani Tunapita Hivyo Usikubali Kuisha Bila Kuokoka, Kumbuka Dini Wala Dhehebu Halimpeleki Mti Uzima Wa Milele Bali Anayepeleka Watu Uzima Wa Milele Ni BWANA YESU
Warumi 6:23 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu. '' 

Masaa Ya Kuamua Kuwa Kwa YESU Uzimani Ni Haya. 
Ndugu, Amua Vyema Na Hakika Utakuwa Umefanya Vyema Sana.
Mathayo 4:16-17 ''Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia. Tokea wakati huo YESU alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.   ''
-Hata leo BWANA YESU kupitia neno lake hili anahubiri kwa kila mwanadamu kwamba atubu maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
-Kumpokea YESU leo ni kupanda uzima.
-Ndugu panda uzima leo kwa kuokoka. 
- BWANA Wetu Atakuja Siku Moja.

Kuna watu wanahangaika na dunia huku wakihitaji tu baraka wakati matendo yao ni maovu.
 Wewe unayesema MUNGU amekuacha au amekusahau naomba tu ujue kwamba MUNGU hajakuacha wala hajakusahau, kama MUNGU angekuacha au angekusahau hakika usingekuwepo.
Lakini kuwepo kwako hai leo kuna maana uamue kupanda uzima wa milele na sio kupanda jehanamu.

 Kama unataka sana MUNGU akupiganie ni lazima kwanza ujifunze kuwaona wengine kuwa ni bora kuliko wewe.
Je unapanda nini sasa?
 BWANA anasema kwako leo kwamba ''Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.-Mithali 3:1''

 Tarajio lako la milele ijayo ni nini?
Je Unazijua njia na taratibu za kukufikisha kwenye tarajio lako?

Binafsi nakushauri tu umpokee YESU maana hapo ndio utakuwa unapanda uzima wa milele. 

Ndugu yangu siku ile hutaondoka na elimu yako
wala utajiri wako bali utaondoka mikono mitupu.
Mimi nakuonya na kukuomba kwa upendo
mwingi sana mpokee BWANA YESU na uishi
ukimpendeza MUNGU. Kumbuka hakuna uzima
nje ya BWANA YESU.
YESU KRISTO anakupenda sana na yuko tayari
kukupokea leo na jina lako litaandikwa mbinguni
kwenye kitabu cha uzima.
Wagalatia 5:18-21 ''Basi matendo ya mwili ni
dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu,
hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi,
ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika
hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha
kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo
ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.''

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments