KWANINI HUWA TUNASALI KANISANI NA SIO KWENYE SINAGOGI?

Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze  Neno la MUNGU.
Kuna ndugu waliniuliza sana kwanini nyie wakristo mnasali kanisani wakati YESU alisali kwenye sinagogi.
Majibu yangu yalikuwa rahisi sana maana Bibllia iko wazi sana kuhusu hilo.
Kwanza naomba tujue kwamba BWANA YESU alienda kwenye sinagogi kwa ajili ya kuwafundisha watu wa kwenye sinagogi maana walikuwa hawaifuati kweli ya MUNGU.
Ona mfano huu
Marko 6:2 ''Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? ''
-Hivyo BWANA YESU alienda kuwasaidia watu wa kwenye masinagogi maana walikuwa hawafuati kile akitakacho MUNGU.

Neno “kanisa”  asili yake ni  neno la Kiyunani ''ekklesia'' ambalo maana ni “kusanyiko” au “walioitwa.”
Kuna wana kanisa wameitwa kutoka katika dhambi na mambo ya kidunia na sasa wako katika MUNGU aliye hai kupitia YESU KRISTO.
Kazi ya wana kanisa ni kwanza kuokoka pili ni kuishi maisha mataktifu na tatu ni kuwa mashahidi wa injili duniani kote.

Maana ya asili ya “kanisa” sio ile ya jengo, bali ni watu.
Waebrania 2:12-13 '' Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya KANISA nitakuimbia sifa. Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na MUNGU. ''
kWANINI SASA SISI TUNASALI KANISANI BADALA YA KWENYE SINAGOGI?

1.   Tunasali kanisani kwa sababu kanisa lilianzishwa na BWANA YESU mwenyewe.
Mathayo 16:18-19 '' Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. ''
-Kanisa lilianzishwa na BWANA YESU na yeye ndiye pekee njia ya uzima wa milele hivyo hatuwezi kujitenga na YESU maana kujitenga na YESU ni kujitenga na uzima wa milele.
Matendo 4:12 ''  Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.''
Mwenye kanisa ndiye anayeandaa makao ya uzima wa milele, yeye BWANA YESU anasema 

Peter & Scholar Mabula, P A G Kawe.
'' Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi.Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. -Yohana 14:1-3 ''
Hivyo tunapompokea YESU tunampokea yeye mwenye uzima wetu wa milele na tunakuwa tunampokea yeye ambaye yuko huko kwenye uzima wetu akituandalia makao.

2. Tunasali kanisani kwa sababu  kanisa ni la MUNGU na ndio mpango wa MUNGU wa wokovu
1 Timotheo 3:15 ''Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.''
-Kanisa ni nyumba ya MUNGU yaani kanisa ni sisi wateule ambao MUNGU hufanya makazi katika mioyo yetu kupitia ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye msimamizi wa wokovu wetu.
-Kanisa ni la MUNGU maana MUNGU ndiye alilileta. Hakuna popote sinagogi linaitwa sinagogi la MUNGU. Siku zote sinagogi ni la wanadamu lakini Kanisa ni la MUNGU.
Sehemu nyingi Biblia inasema neno''Sinagogi la wayahudi'' kumbe sinagogi ni la wanadamu lakini kanisa ni la MUNGU kama Biblia inavyosema
Waefeso 1:22-23 ''Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.''
-Kumbe kanisa ni mwili wa KRISTO na tena kanisa ni ukamilifu wa KRISTO.
Lakini pia naomba tutambue kwamba Biblia inapotaja kanisa maana yake inawataja wale ambao wanamfuata YESU KRISTO na tena wanaishi maisha matakatifu katika yeye.

3.   Kanisa lina mamlaka ya kumshinda shetani.
Matendo 12:5 ''  Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. ''
-Hii ni sehemu ndogo tu ya Mamlaka ya Kanisa maana kanisa lina kibali cha MUNGU hivyo MUNGU hulishindia kanisa maana ni lake. Katka andiko hilo hapo juu kanisa lilomba ili Petro awe huru mbali na kutekwa na shetani na kweli MUNGU alijibu na Biblia inasema
 ''  Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.Mara malaika wa BWANA akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate.Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono.Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba.Naye alipobisha kilango cha lango, kijakazi, jina lake Roda, akaja kusikiliza.Alipoitambua sauti ya Petro, hakukifungua lango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani akawaambia kwamba Petro anasimama mbele ya lango.Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. Wakanena, Ni malaika wake.Petro akafuliza kugonga, hata walipokwisha kumfungulia wakamwona, wakastaajabu. Naye akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi BWANA alivyomtoa katika gereza. Akasema, Kampasheni Yakobo na wale ndugu habari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.- Matendo 12:6-17''
-Kazi ya kanisa hapa inaonekana.
-Kama hadi Malaika wa MUNGU anatumwa ili kuja kuokoa kutokana na maombi ya kanisa je inahitaji nini tena ili kuwajulisha watu kwamba kanisa ndio mpango wa MUNGU na kwamba kanisa lipo duniani kwa kusudi la MUNGU.

1 Thesalonike 4:16-17 '' Kwa sababu BWANA mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya MUNGU; nao waliokufa katika KRISTO watafufuliwa kwanza.Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na BWANA milele.''

Ndugu yangu, naamini kuna kitu umejifunza hivyo nakuomba chukua hatua ya kwenda kanisani na kumpokea YESU KRISTO kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yako na baada ya hapo hudhuria fundisho kanisani ili uimarike na upate nguvu za kuwasaidia na wengine.
MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
mabula1986@gmail.com.
0714252292.

Comments